Si kila kiongozi anafaa kuwa kiongozi na si kila kiongozi ni kiongozi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Si kila kiongozi anafaa kuwa kiongozi na si kila kiongozi ni kiongozi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Salary Slip, Aug 8, 2012.

 1. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #1
  Aug 8, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 24,968
  Likes Received: 37,524
  Trophy Points: 280
  Watanzani tuwe makini sana na watu wanaosaka uraisi kwa udi na uvumba.Watu wanaotumia makanisa na misikiti kuusaka uraisi kwa kutoa misaada ni watu hatari sana.

  Watu wote wanaotangaza nia ya kutaka uraisi mapema na hadharani tuwe makini na vitendo na kauli zao.Wanaweza kuonekana wanafaa sana kwa matendo na kauli zao kwa lengo la kushawishi umma uwakubali lakini kilicho kwenye nafsi zao ni siri kubwa.

  Kiongozi makini ni yule anaesukumwa na shida na matatizo ya jamii inayomzunguka kutafuta uongozi na si yule anaetumia shida na matatizo ya jamii kupata uongozi.

  Si kila kiongozi anafaa kuwa kiongozi na si kila kiongozi ni kiongozi
   
 2. Wamunzengo

  Wamunzengo JF-Expert Member

  #2
  Aug 8, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 810
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 60
  ni kweli tunatakiwa kuwa makini lakini kwa vigezo gani? maana hata Mh. Dhaifu tuliaminishwa kuwa ni chaguo la Mungu, lakini leo tulio wengi tunaangua kilio kwa jinsi anavyoubananga uongozi. DAH!! KAAAZI KWELIKWELI. lakini hata hivyo kiongozi lazima atokane na hao hao unaowaona kila siku, sasa tutatoa wapi wengine? mi nakushauri na wewe ujitokeze kuongoza, kwani inawezekana ukawa kiongozi mzuri, maana inaonesha una hisia za kujali maslahi ya umma, kama uliyoyazungumza hapo juu yanatoka kwenye uvungu wa moyo wako kwa dhati.
  Halafu ukumbuke sio rahisi kujua yaliyomo kwenye nafsi ya mtu na siri zao, hapa kikubwa tumuombe Mungu atunusuru kwa hili.
   
Loading...