Si katika CDM, CCM,CUF, WALA VYAMA VINGINE HAKUNA MWANASIASA MKWELI WOTE NI KWA AJILI YA MATUMBO YAO | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Si katika CDM, CCM,CUF, WALA VYAMA VINGINE HAKUNA MWANASIASA MKWELI WOTE NI KWA AJILI YA MATUMBO YAO

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by matunge, Apr 10, 2011.

 1. m

  matunge JF-Expert Member

  #1
  Apr 10, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 346
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 60
  Inasikitisha: Ni umbali wa km kama 2 tu, toka ukumbi wa BUNGE la JMT, ambapo wabunge wa CCM, CDM et al. na mawaziri hukutana, kuna Hospitali ya mkoa wa Dodoma ambapo wanawake wazazi hulala chini, ama wawili katika kitanda kimoja. Lakini sijawahi sikia mwanasiasa yeyote yule kutoka katika vyama tajwa akikataa mpango wa kukopeshwa zile mil 100 kwa ajili ya kununua gari. Miongoni mwa waliopokea fedha hizi ni wale ambao walikuwepo katika Bunge lililotangulia; kimsingi hawa bado wana magari yale ya awali. Pia wanasiasa hawa kila kukicha hujipitishia nyongeza ya malipo ya kila mwezi na posho ya vikao.Ingelikuwa vema kama sehemu ya fedha hizi zikapelekwa katika Hospitali hii, kuokoa maisha ya akina mama na watoto wao katika Hospitali hii.
   
 2. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #2
  Apr 10, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,515
  Likes Received: 1,686
  Trophy Points: 280
  mkuu hao wabunge kweny majimbo yao kuna matatizo zaidi ya hayo uliyoyataja. wakianza kushughulika na matatizo ya jimbo lingine matatizo ya kwenye majimbo yao yatashughulikiwa na nani?
   
 3. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #3
  Apr 10, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,010
  Likes Received: 1,815
  Trophy Points: 280
  Yaani haya nido mambo ya kuongelea ndani ya hii forum. Nakuunga mkono kwa asilimia mia mbili!! Tanzania hakuna watu wanasiasa wakweli hata kidogo na kama wapo basi ni wachache sana kila mtu anapigania tumbo lake! Vyama vya siasa ni makundi tu ya watu wanaotaka kujishibisha hakuna cha kutetea wanyonge wala nini. Bungeni kunashangaza, inapofika kuhusu masilahi yao basi wote husau tofauti zao na kuwa kitu kimoja na kujinyakulia maslahi manono. Kama mtu unawakilisha watu masikini inakuwaje unaenda kuchukua mijiposho na mijikopo minono minono (ambayo sijui kama hulipwa yote) ilihali hospitalini hakuna madawa wala vitanda. Kama kweli wana uchungu na masikini wa nchi hii watoe sehemu ya posho zao kusaidia huduma za jamii. Hospitali zipo nying zinazosikitisha kaka!
   
 4. M

  Mike 1234 JF-Expert Member

  #4
  Apr 10, 2011
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 1,634
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Heading tofauti na maelezo,watu wazuri wapo na hata ndani ya ccm
   
 5. Papa D

  Papa D JF-Expert Member

  #5
  Apr 10, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 687
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Nakupinga kwa nguvu zote ndugu!!!!!
  CHADEMA kupitia Katibu mkuu wake aliwahi kusema Mishahara na marupurupu ya Wabunge ni mikubwa mno!!! Bunge zime lilirindima!!!!
  Sera ya CDM kwenye uchaguzi mkuu ni kupunguza marupurupu ya watu wa aina hiyo!! HAWAKUFANIKIWA KUUNDA SERIKALI [ WATANZANIA TULIWAKATALIA KWA KUWAPA CCM VITI VINGI VYA UBUNGE PAMOJA NA URAIS].
  Mbunge wa Ilemela katoa sehemu ya fedha yake ili kununua Gari la wagonjwa [hadi sasa limeshaanza kutumika]. Ni mbunge wa chama gani ulishawahi kumsikia au kumuona anafanya hiyo???!!
  JAMANI TUACHENI USHABIKI NA TUUKUBALI UKWELI KWAMBA HATA kama CDM wana uchu wa madaraka na njaa, lakini angalua wanaonyesha kutoa mgawo kwetu walala hoi!!

  THINK AGAIN ABOUT YOUR ALLEGATIONS!!
   
 6. kipindupindu

  kipindupindu JF-Expert Member

  #6
  Apr 10, 2011
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 1,051
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Naunga mkono hoja!ndo maana unakuta mwanasiasa anahamahama vyama,hana msimamo au sera anayoiamini.
   
 7. only83

  only83 JF-Expert Member

  #7
  Apr 10, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Wamekusikia mkuu......................................wapo wengi tu humu JF...
   
 8. n

  niweze JF-Expert Member

  #8
  Apr 10, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 1,008
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  I got you point na fustrations ulizonazo lakini ukae kujua kubadilisha utaratibu au bill yeyote ile lazima vitoke kwa hawa majambazi ccm. Ni kitu cha kusikitisha kwamba serikali inatoa hongo kwa wabunge na wanajeshi nafasi za juu kwa kutumia pesa za wahisani na kodi ya watanzania. Let's no give up hope kwamba wabunge wote hawajali wananchi, wabunge wa cdm wamezungumzia hili swala kwa kirefu na kuonyesha jinsi gani wanakerwa na siasa za hongo za ccm. Ukweli ni kwamba cdm wakikataa hizi pesa zitarudi kwa makinda na kikwete atampa mtoto wake anunue gari jipya. We have to be truthful tunapozungumzia nafasi ya cdm katika bunge na uzembe wa huyu mwanamke makinda.
   
 9. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #9
  Apr 10, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,010
  Likes Received: 1,815
  Trophy Points: 280
  Kaka umenena. Hakuna aliyehama na akasema kwamba anahama kwa kuwa hakuridhishwa na sera za chama, wengi wao hawazijui sera za vyama vyao wao kwao ni kupata ubunge tu na kujinufaisha! Ndio maana mimi sipendi chama chochote kwa kuwa ni magenge tu ya wasaka tonge!!! Hakuna ubishi kuwa kuna watu wazuri ndani ya vyama hivyo lakini kwa ujumla wao (chama) ni kundi tu linalosaka tonge kupitia kodi za wavuja jasho. Naamini mimi nitajikomboa mwenyewe toka kwenye mikucha hii ya wasaka tonge.
   
 10. mwanaone

  mwanaone JF-Expert Member

  #10
  Apr 10, 2011
  Joined: Apr 2, 2011
  Messages: 635
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 180
  huo ndio ukweli wa mambo. hadi sasa hakuna mwenye nia thabiti ya kuwatetea wanyonge wa nchi sio chadema, wala ccm wote nia yao ya kwanza ni kutaka kuwa popular, kutafuta utajiri na wengine malengo yao kupata vyeo ili wawaonee au walipize kisasi dhidi ya watu fulani. hawa wanaojitia ni wapinzani kwa kweli ni wababaishaji wanchofanya ni kututumia sisi wananchi kufanikisha malengo yao.
   
 11. m

  matunge JF-Expert Member

  #11
  Apr 10, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 346
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 60
  wala sina hii kitu yenye rangi nyekundu..............ni maoni tu Mkuu
   
 12. Chakunyuma

  Chakunyuma JF-Expert Member

  #12
  Apr 11, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 811
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  lema alipinga hukusikia
   
 13. mangi waukweli

  mangi waukweli JF-Expert Member

  #13
  Apr 11, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 246
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kupinga kwa maneno haisaidi na NI UNAFIKI WA HALI YA JUU, WAO CHADEMA SI CHAMA CHA KUSUSA TUNGEWAONA WA MAANA KUSUSIA HIZO FEDHA NA KUZIELEKEZA ZIPUNGUZWE KWANZA MAJIMBONI KABLA YA KUPOKEA. NDIYO MAAANA WENYE AKILI ZAO WAMESHAONA HAKUNA MWANASIASA MKWELI WOTE WEZI TU "HATUWEZI KUTEMA BIGIJII KWA KARANGA ZA KUONJA" KUITOA CCM NA KUIWEKA CHADEMA,WOTE WASHE................
   
 14. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #14
  Apr 11, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,688
  Likes Received: 410
  Trophy Points: 180
  siasa ni mchezo mchafu na ukweli ni mchezo hatari
   
 15. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #15
  Apr 11, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,267
  Likes Received: 19,407
  Trophy Points: 280
  ????????
   
 16. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #16
  Apr 11, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,267
  Likes Received: 19,407
  Trophy Points: 280
  matunge nalkubaliana na wewe ,sema hata hivyo matatizo yote hayawezi kumalizwa na viongozi wetu,lazima na sisi tu play part tunayoiweza
   
 17. N

  NZURI PESA JF-Expert Member

  #17
  Apr 11, 2011
  Joined: Mar 25, 2011
  Messages: 4,034
  Likes Received: 1,246
  Trophy Points: 280
  Hilo halina ubishi.Jamaa wapo kwa maslahi binafsi! Hapa unani kumbusha mbali sana,pale nilipo kuwa mwanasiasa muaminifu,mpenda amani,maendeleo na mabadiliko ya kidemokrasia ktk nchi yangu kwa Miaka 19 hadi kufikia mwaka 2010.Niliyojifunza ndani ya vyama hivi ni mengi.Kubwa kuliko yote WANAFANANA MALENGO YAO HAKUNA WA AFADHALI.MKUNJO KWANZA, MENGINE BAADAE
   
 18. N

  NZURI PESA JF-Expert Member

  #18
  Apr 11, 2011
  Joined: Mar 25, 2011
  Messages: 4,034
  Likes Received: 1,246
  Trophy Points: 280
  Kauli kama hizo nizakawaida ktk Propaganda. Mbona HAWAACHI KUPOKEA
   
Loading...