Si halali wala haki kwa Serikali ya CCM kuwatoza wananchi fedha ili kutumia Daraja la Nyerere kwenda Kigamboni, ni ubaguzi

Nauli 450 kumbuka kila abiria analipa 50 hivyo kubaki nauli 400 ya serikali .

Abiria wanalipia isipokuwa wamefungwa jinsi ya kujua wanalipaje
Hata wangeweka nauli 400/=, bado ungesema hayo hayo, eitherway, 50/= na kulipa 200/= kivukoni kwenye ferry bado kuna unafuu mkubwa darajani, lipeni watu wapate viiunua mgongo vyao NSSF
 
Ni daraja la serikali.
Hilo daraja sio la CCM wala sio la Serikali, maana hata hiyo 40% serikaki haikuchangia kama walivyokubaliana, hivyo daraja ni la wastaafu wa mfuko wa NSSF ambao wanapaswa kurejeshewa mafao yao yaliyotumika kujenga hilo daraja. Hivyo hoja iwe, ni wapi pesa ya kuwarudishia NSSF plus interest na projected profit iki liwe mali ya serikali.
 
Kila abiria analipia,sema imefichwa kwenye naui mkuuu,450 kwa 400
Kama huna kwanini usipande daladala ambapo hutalipia chochote zaidi ya ile nauli tu ya kawaida? Badala yake utumje gari binafsi halafu uje ulalamikie kulipia daraja lililojengwa kwa pensheni za wavuja jasho waliostaafu na ambao wanategemea wewe ulipe na wao ndio walipwe viinua mgongo vyao?
 
Wenzio hifadh ya jamii wamewekeza hapo hela zetu wapate faida warudishe tena

Yaan unachkua hela yangu unaitumia halaf nailipia tena

Yaan nakupa hela yangu uniwekee .unanikopesha tena hela yangu hyo hyo niliyokupa tena kwa riba...mama.e
 
Makubaliano yao siyo serikali iwarudishie, bali tozo ndiyo zirudishe...

Cc: mahondaw
Hilo ndilo sio halali. Makubaliano ya hivyo yalipaswa kufanywa kati ya wananchi na NSSF. Kisheria, wananchi wanaweza kusema hatukushirikishwa kwenye hayo makubaliano yenu, toeni daraja lenu.
 
Wenzio hifadh ya jamii wamewekeza hapo hela zetu wapate faida warudishe tena

Yaan unachkua hela yangu unaitumia halaf nailipia tena

Yaan nakupa hela yangu uniwekee .unanikopesha tena hela yangu hyo hyo niliyokupa tena kwa riba...mama.e
Hivi kun namna wadau wa NSSF wanashirkishwa kwenye haya maamuzi? Kuna miradi ya NSSF imepata hasara sana, na hiyo ni hela ya wadau
 
Hilo ndilo sio halali. Makubaliano ya hivyo yalipaswa kufanywa kati ya wananchi na NSSF. Kisheria, wananchi wanaweza kusema hatukushirikishwa kwenye hayo makubaliano yenu, toeni daraja lenu.

Daraja kutoa halitatoka...
Na hata pesa zote zikisharudishwa na wananchi kwa njia ya tozo bado tozo zitakua pale pale...

Cc: mahondaw
 
Acha kuzunguka mbuyu, hayo yote tumeshajadili, hatuwezi kugharamia daraja ambalo tayari lipo na linafanya jazi tuache kujenga mapya; unaelewa maana ya vipaumbele?!
Ndio maana uzi unataka serikali isawazishe hili kabla ya kuendelea na mengine. Chanjo ya Corona ikipatikana huwezi kusema kwa wagonjwa kwamba kwa kuwa nyie ni wagonjwa tayari basi tunawaacha sie tunatoa kipaombele kwenye chanjo kuzuia wengine wasipate Corona
 
Daraja kutoa halitatoka...
Na hata pesa zote zikisharudishwa na wananchi kwa njia ya tozo bado tozo zitakua pale pale...

Cc: mahondaw
Na hilo ndilo kosa lililofanyika. Kwa ninavyomfahamu Magufuli, hata tozo litakapokuwa limerudisha fedha ya NSSF, sio rahisi kwamba atasimamisha tozo - ataliona daraja kama bata mzinga anaetaga mayai ya dhahabu, na hawezi kumwachia kirahisi. Sasa hii inatoa precedent mbaya. Seikali inaweza kuona ni kamchezo ka kuingiza fedha kiualini. Kuna siku watasingizia NSSF, au kufanya makusudi, kujenga daraja la Wami na hivyo kila gari linalopita pale litozwe fedha!
 
Daraja kutoa halitatoka...
Na hata pesa zote zikisharudishwa na wananchi kwa njia ya tozo bado tozo zitakua pale pale...

Cc: mahondaw
Na usisahau kwamba, katika kila lita ya petroli au dizeli unayonunua, kuna tozo kwa ajili ya Tanroads kujenga vitu kama haya madaraja, flyover na barabara na kuzifanyia ukarabati, juu ya fedha inayotengwa na serikali na misaada kwa ajili ya miradi ya Tanroads.

Hivyo kimsingi, kuyatoza tozo magari yanayotumia daraja hili ni kuwafanya walipie toll ya barabara mara mbili. Sheria zetu wenyewe zinasema si halali kwa mwananchi kutozwa kodi mara mbili kwa kitu kile kile.
 
Ndio maana uzi unataka serikali isawazishe hili kabla ya kuendelea na mengine. Chanjo ya Corona ikipatikana huwezi kusema kwa wagonjwa kwamba kwa kuwa nyie ni wagonjwa tayari basi tunawaacha sie tunatoa kipaombele kwenye chanjo kuzuia wengine wasipate Corona
Unaelewa maana ya kipaumbele?
 
Mleta mada inaonekana serikali ikija na mpango wa barabara za PPP utakuwa wa kwanza kupinga. Kwamba serikali iruhusu watu binafsi wajenge barabara halafu watumiaji walipe toll. Bado utalalamika wakati ndio utaratibu unaotumika nchi nyingi kupunguzia mzigo serikali. Kwanza nani kakuambia kuwa kwenda kigamboni ni kwa ferry na darajani tu? Kapite kule Mbagala kuna daraja la nchi kavu bure kabisa
 
Ufaransa kipindi inatawaliwa na king louis xvi walikua na kodi kama hii iliyofahamika kama bridge tax, hiyo ni moja ya sbb mfalme huyo kupinduliwa
MKuu hizi kodi za kutumia miundombinu ya serikali tulikuwa nazo kama Road toll. Tatizo TRA. KUlikuwa na vibanda vya kutozwa road toll ambapo hata nyumba za wafanyakazi wa road toll zilijengwa kama pale Chalinze.

Sasa tatizo ikawa watu wa TRA/Road Toll wakawa wanazipiga sana hizi hela. Walikuwa wnachapisha hadi risiti zao wenyewe kukawa na wizi sana. Ndipo wazo likatolewa kwamba waondoe vibanda vya road toll barabarani na iwekwe kwenye dizeli na petroli. Japo watu walilalalmika kwamba roadtoll ni kwa ajili ya highway za kwenda mikoani sio mijini, na kwamba mafuta kama ya generator au matrekta au mashine za nafaka hayapaswi kutozwa road toll tax serikali ilikomaa ikaweka road toll kwenye dizeli na petroli. Matokeo yake serikali ikawa inakusanya road toll kwenye mafuta karibu mara 100 ya road toll iliyokuwa inakisanywa barabarani! Wakawa wamegundua kamchezo.

Kwa hiyo kimsingi, wananchi tunalipia roadtoll mara mbili kwa kutozwa tozo la kuvuka daraja.

Ndio maana hata suala la road license ya kila mwaka kuwekwa kwenye dizeli na petroli serikali ililishangilia sana tu pia, japo nakiri kuwa limekuwa jambo zuri kupunguza usumbufu wa TRA kutoza watu road license fee kwa magari ambayo hayapo tena barabarani.
 
Mleta mada inaonekana serikali ikija na mpango wa barabara za PPP utakuwa wa kwanza kupinga. Kwamba serikali iruhusu watu binafsi wajenge barabara halafu watumiaji walipe toll. Bado utalalamika wakati ndio utaratibu unaotumika nchi nyingi kupunguzia mzigo serikali. Kwanza nani kakuambia kuwa kwenda kigamboni ni kwa ferry na darajani tu? Kapite kule Mbagala kuna daraja la nchi kavu bure kabisa
Mkuu, naelewa sana suala la barabara za PPP. Hizo hutolewa kama alternative roads, ambapo kunakuwa na barabara ya serikali na ile ya PPP. Nilikuwa Turkey nikataka kusafiri kwa gari toka Ankara kwenda Istanbul. Unakuwa na choice - kutumia barabara ya PPP ambayo ni fenced road three lanes kila upande na haina speed limit na ina vibanda vya road toll kila umbali fulani, au ile ya serikali ya free ambayo ni single lane. Kama huo ndio utakuwa mpango sina tatizo.

Na kama ukileta suala la kusema kuna barabara za PPP sijui, basi ondoa tozo la kujenga na kukarabati barabara kwenye dizeli na petroli.

Bila hayo ni kweli nitapinga. Angalia hapa chini sehemu ya mkeka wa Ankara-Istanbul ambao ukitumia unalipia. Sasa ukiweka huu kwa ajili ya Dar - Arusha ukasema tulipie na hauna tochi wala spidi limit, leta fyombo tu!

1604585730922.png
 
hili ndilo jambo la msingi linalonifanya nisivutiwe na kuenda kujenga kigamboni. sijawahi kuona iko sawa kila siku utenge kielfu mbili cha kuvukia kwenda nyumbani kwako. ikitokea siku huna huvuki.. imagine kuna siku mtu biashara au mishe zinakua ovyo unabaki na uteni tu wa kuweka mafuta kwenye gari urudi kwako

Niliwahi kaa huko zamani, ila sijui pesa ya kulipa kuvuka nilikuwa naitoa wapi, mana sikuwahi kosa hata siku moja wala kuliwazia hilo, nilipohama huko nakuamia pasipo na kivuko mpaka pesa ya wese ilikuwa ya mazabe. Au nilikuwa fisadi, mana ndiyo msemo wao.....
Kwa sasa Mungu ni mwema sanaaaaaaa.... japo nasikia jamaa aliyesema tupige mbizi eti karudi tena
 
Mkuu, naelewa sana suala la barabara za PPP. Hizo hutolewa kama alternative roads, ambapo kunakuwa na barabara ya serikali na ile ya PPP. Nilikuwa Turkey nikataka kusafiri kwa gari toka Ankara kwenda Istanbul. Unakuwa na choice - kutumia barabara ya PPP ambayo ni fenced road three lanes kila upande na haina speed limit na ina vibanda vya road toll kila umbali fulani, au ile ya serikali ya free ambayo ni single lane. Kama huo ndio utakuwa mpango sina tatizo.

Na kama ukileta suala la kusema kuna barabara za PPP sijui, basi ondoa tozo la kujenga na kukarabati barabara kwenye dizeli na petroli.

Bila hayo ni kweli nitapinga. Angalia hapa chini sehemu ya mkeka wa Ankara-Istanbul ambao ukitumia unalipia. Sasa ukiweka huu kwa ajili ya Dar - Arusha ukasema tulipie na hauna tochi wala spidi limit, leta fyombo tu!

View attachment 1620141
Mkuu ndio maana kwenda Kigamboni kuna options 3. Sio lazima ukalipie ferry au Daraja la Nyerere. Ukitaka the shortest distance basi lipa hapo Darajani. Madaraja mengine uliyoyataja kama Wami huwezi lipia kwa sababu kwanza ni mali ya serikali na pili hakuna other option.

Hata ingetokea flyover ya Ubungo wamejenga NSSF lazima tungelipia maana kama hutaki panga foleni chini.

Hata hostel za UDSM zile za Mabibo,kodi yake sio sawa na hostel za Main Campus maana NSSF anataka chake ASAP
 
Back
Top Bottom