Si halali wala haki kwa Serikali ya CCM kuwatoza wananchi fedha ili kutumia Daraja la Nyerere kwenda Kigamboni, ni ubaguzi

Ndio maana nikasema, hoja yako iwe ni namna gani pesa zinaweza kutengwa kwa ajili ya kuwalipa NSSF, lakini pia tambua kuna vipaumbele, kweli tuache kuboresha wodi za wamama wajawazito tuanze kutafuta bilioni 200 za kuwapa NSSF ili wewe ulieenda kuishi Kigamboni na kuacha kwingine kote kwa hiari yako, na unagari lako binafsi, usilipe 3,000/= kwa siku wakati umeweza kuweka mafuta, na kama ungepanda daladala hulipi kitu
Mkuu acha kuwa na roho ya kimasikini kiasi hicho(samahani lakini), so unataka wakazi wa kigamboni wote wawe kama wewe(maskini)? Kama wodi za wamama na zinginezo ni kipaumbele je tuna sababu gani ya kujenga daraja la pale salenda?
 
Kwa sababu Salender bridge halipo bado ila Kigamboni bridge lipo tayari, hivyo ni bora tukajenge wodi pale zinapohitajika au tukajenge pale linapohitajika (Salender) kuliko kutumia hizo pesa kwenye daraja ambalo tayari lipo na linafanya kazi
 
Mkuu ndio maana kwenda Kigamboni kuna options 3. Sio lazima ukalipie ferry au Daraja la Nyerere. Ukitaka the shortest distance basi lipa hapo Darajani. Madaraja mengine uliyoyataja kama Wami huwezi lipia kwa sababu kwanza ni mali ya serikali na pili hakuna other option.

Hata ingetokea flyover ya Ubungo wamejenga NSSF lazima tungelipia maana kama hutaki panga foleni chini.

Hata hostel za UDSM zile za Mabibo,kodi yake sio sawa na hostel za Main Campus maana NSSF anataka chake ASAP
Nakuelewa Mkuu, ila option ya 3 sio option, ni incovenience ambayo serikali ilitakiwa iishughulikie. Huwezi kuniambia tunajenga barabara ya kulipia toka Iringa kwenda Dodoma, na kama hutaki kulipia una option ya kupitia Morogoro kwenda Dodoma. Hapo hujanipa option, unaniadhibu kwa kukataa kulipia barabara yako ya Iringa - Dodoma.
 
Mkuu acha kuwa na roho ya kimasikini kiasi hicho(samahani lakini), so unataka wakazi wa kigamboni wote wawe kama wewe(maskini)? Kama wodi za wamama na zinginezo ni kipaumbele je tuna sababu gani ya kujenga daraja la pale salenda?
Huyu jamaa hajielewi kabisa, anaongea vitu havina msingi.
 
Nakuelewa Mkuu, ila option ya 3 sio option, ni incovenience ambayo serikali ilitakiwa iishughulikie. Huwezi kuniambia tunajenga barabara ya kulipia toka Iringa kwenda Dodoma, na kama hutaki kulipia una option ya kupitia Morogoro kwenda Dodoma. Hapo hujanipa option, unaniadhibu kwa kukataa kulipia barabara yako ya Iringa - Dodoma.
Kwani kabla ya daraja mlikuwa mnapita wapi kama mbadala wa Ferry?
 
Kwani kabla ya daraja mlikuwa mnapita wapi kama mbadala wa Ferry?
Tulitumia ferry, kwa hiyo huko kwingine hakukuwa mbadala kihalisi, ndio maana nikakupa concept ya Iringa Dodoma direct au kupitia Morogoro. Au unakumbuka wakati fulani tulisafiri Dar Mwanza kwa basi kupitia Kenya? Sasa huo sio mbadala halisi wa kwenda Mwanza.
 
Nimewasikia NSSF leo power breakfast wakijisifu kuwa wanakusanya bn1 kwa mwezi pale darajani. hawawezi acha aisee pesa tamu.
 
Back
Top Bottom