Si ACACIA tu, wachimbaji wote wa madini, gesi na mafuta lazima watusikilize. Mikataba si msahafu!

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,175
25,446
Tunafahamu fika kuwa wachimbaji wa madini, gesi asilia na mafuta hapa Tanzania ni wawekezaji. Tunafahamu pia kuwa wawekezaji, katika dunia ya sasa ya ubepari, wana haki zao na wanalindwa kisheria na kimikataba. Iko wazi, madini, gesi asilia na mafuta yaliyopo Tanzania ni mali ya watanzania wote iliyowekwa chini ya Serikali kwa uangalizi wake.

Madini, gesi aslia na mafuta yaliyopo Tanzania ni kwa ajili yetu na kwa faida yetu. Kama zilivyo mbuga za wanyama na rasilimali nyingine, madini, gesi na mafuta zinahitaji usimamizi makini na wa kizalendo ili kuweza kutunufaiusha wote kama nchi. Usimamizi mzuri na bora ni pamoja na kuhakikisha kuwa Sheria na Mikataba inakuwa ya kisheria na ya haki.

Sheria na Mikataba si msahafu katika maana ya kutobadilishwa au kupokea mabadiliko. Sheria na Mikataba, ikiwemo ya madini, gesi asilia na mafuta, inabadilika kulingana na hali ya uchumi wa kidunia, mahitaji ya kinchi na haki katika manufaa yatokanayo na uchimbaji au utafutaji huo. Jambo kubwa ni kufuata taratibu za kufanya marekebisho hayo.

Ndiyo maana nasema, si tu ACACIA, wachimbaji na watafutaji wote wa madini, gesi asilia na mafuta hapa Tanzania lazima watusikilize. Sheria na Mikataba inayohusu uwekezaji katika mambo hayo si msahafu na Tanzania, kwakuwa ndiye mwenye mali asili hizo, ana haki ya kurekebisha chochote kwa maslahi yake. Atakayegomea marekebisho, atatupisha na kutuachia nchi yetu.

Kama wenye mali, hatupaswi kujinyenyekeza na kuwa 'wadogo' katika majadiliano. Tunapaswa kusimama imara katika kutetea rasilimali zetu hizo katika namna ya kufaidika nazo. Hata kama kulifanyika makosa ya kisheria na kimikataba huko nyuma, hilo halituzuii wenye mali kutaka 'bei' mpya na maslahi mapya.

LAZIMA wenye mali tusikilizwe. Waliokosa WASIBAKI salama kisheria!
 
HAKIKA MKUU,MWISHO WA SIKU MALI ASILI ZETU LAZIMA ZIWE KWA AJILI YA MANUFAA YA WATANZANI
 
Wakuu, mwenye fursa ingia kwenye website ya TRA nenda sehemu iliyoandikwa Library then chagua decided tax cases ....pale fungua TRA V African Barrick Gold mine PLC ( Appeal No. 128 of 2013 dated 9th July 2015) ....ni very interesting case hasa kwa hili linaloendelea ....tumuunge mkono Rais wetu kwa nguvu zote ....inatosha kuibiwa ....
 
Nitafanya hivyo Mkuu. Asante
 
tumuunge mkono kwa lipi naona usanii tu
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom