mzee wa mkeka
Senior Member
- Mar 12, 2017
- 142
- 236
Habari wanajf;Tangu mgombea ubunge wa bunge la jumuia ya afrika mashariki (EALA) Shy-Rose Bhanji aenguliwa na vikao rasmi vya CCM kumekuwa na maneno yenye lengo la upotoshaji toka kwake mwenyewe. Nayaita ni maneno ya upotoshaji kwa sababu yeye binafsi anajua sababu hasa iliyofanya jina lake liondelewe licha ya kupata kura nyingi kwenye mchakato wa awali.
Kwa mwanasiasa wa kiwango chake anatakiwa atoke aseme sababu za yeye kukatwa na aweke wazi msimamo wake kuhusu hizo sababu halafu aache wananchi wachambue na waamue kati yake na CCM nani hakutendewa haki.
Shy-Rose unajua msimamo wa Tanzania kuhusu mkataba wa EPA (mkataba wa ushirikiano wa kibiashara kati ya EAC na umoja wa ulaya, EU), pia unajua msimamo mkali wa rais Maghufuli dhidi ya EPA. Pia tunajua wewe ni muumini mzuri wa EPA na namna ulivyopigana ndani na nje ya bunge la afrika mashariki kutetea mkataba huu. Tunajua hata kiasi ulichopokea kutetea EPA (hili tuliacha kwa sasa) na ulivyoshirikiana na sakretariati ya jumuia kuwayumbisha wakuu wa nchi za EAC kuhusu EPA. Pia tunajua ushirikiano wako na nchi waumini wa EPA ili kuyumbisha msimamo wa Tanzania.
Turudi kwenye common sense, Tanzania kama nchi na rais Magufuli kama mwenyekiti wa chama chako wanapinga kwa nguvu zote EPA (huu mkataba unajadiliwa toka enzi za rais mkapa) na wewe unaomba uwakilishi wa Tanzania kwenye EALA.
Ni chama na nchi gani itapeleka muwakilishi anayepingana kwa nguvu zote na msimamo wa nchi au chama? Huko EALA unataka uwakilishe chama/nchi gani?