Mgambilwa ni mntu
JF-Expert Member
- May 30, 2017
- 2,869
- 3,188
Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM, Yusuf Makamba amepingana na kauli iliyotolewa na aliyewahi kuwa Spika na Katibu Mkuu wa CCM, Pius Chipanda Msekwa juu ya shutuma alizoelekeza kwa Katibu Mkuu wa CCM, Dk. Bashiru Ally kwa kitendo cha kumuita kupitia majukwaani, kada wake, Bernard Membe.
Makamba akihojiwa na Mwananchi ameunga mkono utaratibu uliotumiwa na Mhadhiri huyo wa zamani wa UDSM na kudai Bashiru ni mtendaji mkuu wa Chama anayewakilisha Halmashauri Kuu na Mkutano Mkuu, hivyo ana mamlaka ya kumuita mwanachama yeyote hata ikiwa hadharani.
Makamba alisema kuwa, hata yeye alipokuwa Katibu Mkuu alikuwa akiwaita wabachama wake vivyo hivyo na kwamba aliwahi kuitwa na Viongozi wa TANU. "Mimi niliwahi kuitwa na (John) Mhavile, nilikuwa Mkuu wa Wilaya ya Tanga. Mhavile alikuwa Katibu Mtendaji wa TANU, yalitokea maneno pale Tanga nikaambiwa njoo, tena si kwa simu. Niliwahi kuitwa na (Balozi Daudi) Mwakawago. Kwa hiyo haya mambo si kwamba ni ya jana."
Mzee Makamba alisema kuwa hata yeye aliwahi kuitwa na Msekwa: "Niliwahi kuitwa na Msekwa kwamba njoo Dodoma na nikaenda. Kwa hiyo ni utaratibu haukuanza jana."
"Kwa hiyo kuitwa na wakubwa ni jambo la kawaida, msiwaonee kwa njia waliyotumia. Kubwa Katibu Mkuu yuko sahihi."