Shule Zetu za Kata ziwe za Ufundi NA Kilimo Zaidi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shule Zetu za Kata ziwe za Ufundi NA Kilimo Zaidi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sabi Sanda, Sep 11, 2010.

 1. S

  Sabi Sanda JF-Expert Member

  #1
  Sep 11, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kama Taifa kuna haja ya kutafakari kwa kina na kufikia uamuzi wa kuzibadilisha nyingi ya shule zetu za kata ziwe za Ufundi na Kilimo zaidi kuliko ilivyo sasa. Lengo letu liwe angalau kuzibadili nusu ya shule hizo kuwa za Ufundi na Kilimo ndani ya miaka kumi ijayo. Hili linawezekana kama tukiamua na kuwekeza ipasavyo.

  FUNDI NA MKULIMA WENYE ELIMU BORA YA KILIMO HALALI NJAA NA HAWEZI KUSHINDWA KUENDESHA MAISHA YAKE NA YA FAMILIA YAKE.
   
 2. Njilembera

  Njilembera JF-Expert Member

  #2
  Sep 11, 2010
  Joined: May 10, 2008
  Messages: 1,398
  Likes Received: 127
  Trophy Points: 160
  Wazo jema kabisa. Wahitimu wa Shule za Ufundi na kilimo ni rahisi kujitengenezea ajira kuliko wa shule za aina nyingi nchini. Bahati mbaya mahitaji ya shule hizi hususani vifaa vya kufundishia na aina ya walimu ni adimu mno. Kwa ajili hii inakuwa rahisi kukimbilia kuanzisha shule za arts.

  hatari yake ni kuwa na wahiutimu wengi katika fani zisizochangiwa uchumi na ajira moja kwa moja, na hasa wale wa kuweza kubuni teknojia na ugunduzi mwingine wa kisayansi. matokeo yake maendeleo ya nchi yatakuwa ya pole pole mno na nchi kufanywa ya wachuuzi badala ya wazalishajii. Hii ni hatari kubwa!
   
 3. PatPending

  PatPending JF-Expert Member

  #3
  Sep 12, 2010
  Joined: Aug 17, 2007
  Messages: 490
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Cha kushangaza hakuna mgombea yeyote wa urahisi aliyegusia suala la elimu ya ufundi na kilimo haswa ukizingatia idadi ya wahitimu wa darasa la saba wanaoshindwa kuendelea na elimu ya sekondari kwa sababu mbalimbali na wale wa kidato cha nne na sita pia. Wao wamekalia kutoa ahadi za elimu bure na kujenga shule zaidi. Unajua ukweli ni kwamba sio mtoto anayeanza shule ana uwezo wa kufika chuo kikuu, wengine vipaji vyao vipo katika ubunifu na usanifu kuliko yale madaftari na hivyo wanapaswa wasaidiwe ipasavyo.

  Inachosha pale unapokuta asilimia kubwa ya wanaojiita mafundi Bongo viwango vyao ni duni jambo ambalo linaweza kuepukika kama ujumbe wa thread hii utatiliwa maanani.
   
 4. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #4
  Sep 12, 2010
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,042
  Likes Received: 1,204
  Trophy Points: 280
  Mie nafikiri tofauti kidogo. Yani ya kwamba kila wilaya kuwe na VETA ya uhakika. Wale ambao hawachaguliwa kuendelea na masomo wawe wanapelekwa moja kwa moja ktk VETA hizo, maana huko atajifunza huo ufundi/kilimo kwa malengo ya kujiajili na sio agriculture ama fundi wa secondari. Ni mawazo tu.
   
 5. PatPending

  PatPending JF-Expert Member

  #5
  Sep 12, 2010
  Joined: Aug 17, 2007
  Messages: 490
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Ndugu yangu hapo ndipo tunaporudi katika makosa yale yale wanayoyafanya watawala wetu. Kuwa na shule au vyuo vya mafunzo ni zaidi ya kuwa na majengo, unahitaji walimu na vitendea kazi. Shule za ufundi ni ghali na uwezo wa kuwa chuo katika kila wilaya au halmashauri si halisia. Suala hapa si idadi bali ubora, na kwa uwezo wa nchi kwa sasa hatuwezi kutoa vyote viwili kwa pamoja, we angalia tu matatizo ya elimu za msingi na sekondari.

  Pa kuanzia ni kuzifufua zile shule za zamani za ufundi na kujaribu kuwa na vyuo vichache ambavyo tutamudu kuviendesha kwa faida ya wengi.
   
 6. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #6
  Sep 12, 2010
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,042
  Likes Received: 1,204
  Trophy Points: 280
  Mkuu, yawezekana ukawa sahihi kabisa. Na bahati nzuri ama mbaya mie pia nimesoma shule ya ufundi sekondari. Ninachoweza kusema ni kua elimu ile haijitoshelezi kumuwezesha mwanafunzi kujiajili.

  Ninachokiamini mimi binafsi ni kuwa, VETA kila wilaya inawezekana, vyuo vikuu angalau viwili kila mkoa inawezekana na wataalamu watapatikana. Ila kinachokosekana ktk viongozi ni ile DHAMIRA ya kweli. Uwezo tunao na sababu tunazo.
   
 7. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #7
  Sep 12, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 0
  Haya ni makosa makubwa sana ambayo tutaendelea kuyafanya kwa muda mrefu, kwa nini usubiri mtoto afeli ndiyo umpeleke kwenye ufundi? Mfumo mzima wa Elimu Tanzania una matatizo makubwa, Elimu ya ufundi inatakiwa kupewa kipaumbele ili kuwapa vijana skills, na si kuwajaza knowledge mwanzo mwisho! Ndy maana graduates wetu wwengi wamezoea kufanya kazi za kukopi! Ni muhimu tuwaweke watoto katika misingi ya kuvumbua vipaji vyao. Niliwahi kutoa ushauri: Ni Lazima shule ZOTE za msingi na sekondari ziwe za ufundi, na kuwe na muunganiko mzuri wa madaraja ya kuvuka, kati ya mtu anayetoka O.Level na kwenda A.Level, na mtu anayetoka O.Level na kuendelea na ufundi kwa ngazi ya kati (VETA wangetoa Diploma, na hizo Certificate zingetolewa Sekondari) waweze kukutana chuo kikuu bila vikwazo! Kwa mpangilio uliopo sasa ni mparaganyiko usio na maana, VETA haina maana yoyote kwa jinsi ilivokaa!!!
   
Loading...