Jamani ifike mahali shule za binafsi zenye kawaida za kufelisha zifutwe kwani ni hasara kwa wazazi. Iweje kila mwaka bidhaa zao ziwe mbovu na bado TBS ya wizara ya elimu haiwamliki? Kaguzi zipi zinafanywa na wizara hii. Je, kuna fomu zozote ambazo ktk ukaguzi wao wanafunzi huzijaza? au wakishafika wakapewa bahasha huishia kuandika ripoti nzuri ili hali kila mwaka shule hizi hutoa divisheni zero kibao na kumwachia mzazi hasara huku wao wakiendelea kutamba kwa makusanyo.