Shule za wenye vipaji maalumu zimezama wapi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shule za wenye vipaji maalumu zimezama wapi?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kibongoto, Feb 16, 2010.

 1. K

  Kibongoto JF-Expert Member

  #1
  Feb 16, 2010
  Joined: Aug 5, 2009
  Messages: 227
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  "Nasema mtachonga sana! Eti wengine wakiwemo ambao hawajasoma hata nusu darasa wanazikashifu sekondari za kata. Kisa zaidi eti ni kwa kuongoza kwa divisheni ziro katika matokeo hayo. Kuchonga wanangu ni haki yenu ya msingi, hivyo endeleeni.

  Kwa hiyo mnashangalia matokeo ya sekondari za kata, mnayaacha mengine ya msingi katika sekta hiyohiyo ya elimu? Je hizo mlizoziita Shule za Wenye Vipaji Maalumu zimewafikisha wapi? Kuna cha vipaji maalumu hapa? Eti Ilboru, Mzumbe, Tabora, Kibaha hadi na Kilakala.
  Naapa na hawa wa Vipaji Maalumu walibeba viroba vya divisheni 0 hivyo msishangilie sekondari za kata.Mlitegemea bado hizo ni shule maalumu? Nyo! Wanafunzi huingizwa shuleni siyo kwa matokeo maalumu, bali ni kwa vijimemo toka kwa wazito.
  Mmebakia kwenye kuzitambua bado kama shule za wenye vipaji maalumu? Na St. Marian, St. Goreti, Uru Seminary zilizobeba viroba vya divisheni 1 ziwe nini? Acheni mzaha ukubwani. Kwanza mnawapotosha hao wanafunzi na kuwavimbisha vichwa buree"

  Wakuu hua mnasoma nakala za huyu bwana? Jamaa hua anaandika ukweli ktk style ya maongezi,basi hua napenda sana kumsoma. Ni ukweli tupu!
  http://www.mwananchi.co.tz/newsrids.asp?id=17971
   
 2. RayB

  RayB JF-Expert Member

  #2
  Feb 16, 2010
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 2,754
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Tatizo ni kuwa kinachotokea kama alivyonote hapo wanaokwenda kule sio maalumu kama zamani tena, umaalumu wa shule umebaki historia wazazi sasa wanafanya jitihada na juhudi kibao kumpeleka mtoto shule binafsi hasa hizi zinazofanay vizuri zaidi, na pia nahisi hata walw walimu bora wa kule maalumu hawapo tena either wamestaafu na wanaokuja kufundisha pale sio wanaostahili huko maalumu au walimu wa huko maalumu wameamua kwemda huku kwa kina Gorreti kwani maslahi ni mazuri. Mzazi siku hizi akiambiwa mtoto kafaulu kwenda Kibaha wala hashtuki hasa kwa O level kidogo bado High school wanajitahidi
   
 3. B

  Bao3 JF-Expert Member

  #3
  Feb 16, 2010
  Joined: Aug 7, 2009
  Messages: 318
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  nami nakubaliana na wewe mkuu
   
 4. D

  Domisianus Senior Member

  #4
  Feb 16, 2010
  Joined: Aug 1, 2008
  Messages: 154
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kweli hili la vipaji maalum linatakiwa liangaliwe kwa umakini wa hali ya juu sana.It doesn't kik in my head kwamba shule za vipaji maalum kama Ilboru kuna ziro 5 na division four 26, kweli tunaandaa makapi kama siyo vibogoyo, yaani hata hizi za vipaji zimetushinda kuziendesha tuzidi kupata wanafunzi bora wanaoandaliwa na serikali mpaka tunafikia division zero kabisa, that is non sense,sasa shule za kata ambazo hazina walimu wa kutosha na vitabu, maabara wala maktaba tukipata zero 50 kunaubaya wowote jamani?
  Turudi nyuma tujisahihishe na tuangalie kama bado tuko kwenye njia sahihi au tunaelekea magharibi wakati wengine wanaelekea mashariki!!!!!!
   
 5. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #5
  Feb 16, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,257
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Utaratibu wa kuwa na shule za wanafunzi wenye vipaji vya maalum kiakili ulishafutwa toka enzi za Mungai. Hoja ilikuwa ni kuwachanganya wanafunzi wenye uwezo kiakili na walio dhaifu kiakili ili kuongeza ufanisi wa jumla na sio kwa wachache wenye uwezo kiakili waliokuwa wakitengwa na kuwekwa kwenye shule maalum.

  Hivyo kwa sasa shule hizo zimebakiza tu historia, wanafunzi wanaochaguliwa kwenda shule hizo ni sawa na tu kwa vigezo vyote na wanafunzi wanaoenda kwenye shule zingine zozote za serikali nchini, katu usilinganishe kabisa matokeo ya shule hizi kwa sasa na enzi zile.
   
 6. M

  Magezi JF-Expert Member

  #6
  Feb 16, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,916
  Likes Received: 162
  Trophy Points: 160
  Tuliokuwa bora ni sisi ambao tulikwenda shule za wenye vipaji na kweli tulitokea vijijini lakini siku hizi ni wasio na vipaji ndo wananenda shule zile na kuondoka na zero.
   
 7. Mama Mdogo

  Mama Mdogo JF-Expert Member

  #7
  Feb 16, 2010
  Joined: Nov 21, 2007
  Messages: 2,878
  Likes Received: 457
  Trophy Points: 180
  Magezi hapo umenena, ni sisi vijana wa zamani angalau tulionja shule za watoto wenye vipaji. Nakumbuka tulivyokuwa tunanyanyasana darasani kupokezana namba za juu, mambo moto moto mtindo mmoja. The old good days!!!!
   
 8. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #8
  Feb 17, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,824
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Ma mdogo wee, unanikumbusha mbali - Nikiwa Kibaha pale bwana tumetoka wani karibu darasa zima- tulikuwa hatuna mchezo na shule, tulikuwa tunataniana - " umetumwa na kijiji mzee" lakini end of the day perfomance juu.

  Shule zinazowika sasa ni za Private - wakati ule mtu ukisoma private unaonekana kilaza wa nguvu - tena kundi la wanaosoma shule za serikali hauwasogelei unatengwa ila kwa sasa ni opposite.

  Hizi shule zitazidi kuzama as days goes on sababu serikali imepunguza fungu sababu hakuna pesa na ukizingatika matatizo ya waalimu nayo inakuwa kikwazo kingine.
   
 9. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #9
  Feb 17, 2010
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,511
  Likes Received: 7,588
  Trophy Points: 280
  Sikubaliani na wewe wanaokwenda ni maalumu,naamini mazingira mabaya yanachangia kufeli kwao
   
 10. bht

  bht JF-Expert Member

  #10
  Feb 17, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  wat about it huh??
  mi ni alumni wa hapo na kwa taarifa yako tulikuwa real special students mkubwa!!
  Kama mabo hayaendi vizuri sasa hivi sijui wat happened to their selections!
   
 11. bht

  bht JF-Expert Member

  #11
  Feb 17, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  inawezekana kabisa
  unaenda pale na kipaji chako, huna mwalimu, hakuna vifaa vya kujifunzia unategemea hicho kipaji kitakua vipi kama si kudumazwa??
   
 12. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #12
  Feb 17, 2010
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,511
  Likes Received: 7,588
  Trophy Points: 280
  Tatizo sio selection,BTW wanaochaguliwa kwenda hizo the so called special siku hizi ndo hao wanaokwenda St marian,St francis et al.Pia shule hazina waalimu kuna matatizo mengi sana kwenye hizo shule siku hizi si kama zamani.
   
 13. Katoma

  Katoma Senior Member

  #13
  Feb 17, 2010
  Joined: Mar 11, 2008
  Messages: 135
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hamna selection maalum kwa shule za vipaji these days. waliamua ku'neutralize
   
 14. B

  Bao3 JF-Expert Member

  #14
  Feb 17, 2010
  Joined: Aug 7, 2009
  Messages: 318
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Hata ungekua wewe usingekubali mwanao aende akashangae madawati na kuliwa na mbu bure wakati zipo sehem ambazo anaweza kuishi maisha mazuri na taaluma iko tambalale. Tuwe wakweli tu!
   
 15. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #15
  Feb 17, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Shule za vipaji maalum zilifutwa kwa sababu kulikuwa hakuna vigezo sahihi cha kupima kipaji cha mwanafunzi kigezo walichotumia ni ufaulu wa mwanafunzi ikagundulika kuwa kupata Dv 1au 2 si kuwa wewe una kipaji maalum hata hao wa Dv 1 waliokuwa wanakwenda pale si wote walizipata kwa kutegea akili zao walikuwa wana prove failure kwa hiyo matokeo yake hizo shule zikawa zinadidimia kielimu mwaka hadi mwaka ikafikia wakati zikawa zinafanya vibaya zaidi ya shule zingine kwa hiyo serikali kupitia kwa Mungai ikasema hakuna haja ya serikali kuendelea kugharamia shule ambazo ni sawa na shule zingine tu
   
 16. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #16
  Feb 17, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,257
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Hapana, mazingira hayajawahi kuwa mazuri, suala ni kuwa wakati ule tofauti na sasa wanafunzi wenye uwezo mkubwa wa kiakili ndio walikuwa wanapelekwa kwenye hizi shule, na kutokana na hilo japo walimu wengi walikuwa hovyo lakini kwa uwezo wa wanafunzi na ushindani uliokuwepo kati yao na kati ya shule moja ya special na nyingine mwisho wa siku matokeo yalikuwa yanakuwa mazuri.
   
 17. B

  Bao3 JF-Expert Member

  #17
  Feb 18, 2010
  Joined: Aug 7, 2009
  Messages: 318
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Nasikia wakifika huko chuo kikuu wote wanakua wanaanza moja. Tena wengine hao wa vipaji utawaonea huruma marks walizoenda nazo hapo chuo na jinsi wanavyohaha kupata makarai. Kazi kwelikweli!
   
 18. Advocate J

  Advocate J JF-Expert Member

  #18
  Aug 14, 2013
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 3,879
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 160
  Hahaha wanachukua creamtupuuu na hamna vilaza
   
 19. s

  sawabho JF-Expert Member

  #19
  Aug 14, 2013
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,597
  Likes Received: 1,029
  Trophy Points: 280
  Ilifika wakati kutokana na shule hizi kutokuwa na walimu maalum, baada ya wale waliokuwepo kustaafu kwa mujibu wa sheria na kwenda kuajiriwa katika shule za St. Goreti, Mzazi akiona mtoto wake amechaguliwa shule maalum kama ana uwezo kipesa, anampeleka huko huko St. Goreti ambako anakutana na Mwalimu yule yule aliyefundisha shule maalum.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...