Shule za vipaji maalum kwa mfumo wa sasa hazina maana halisi ya vipaji. Zifanywe shule za ufundi

  • Kibaha
  • Mzumbe
  • Tabora Boys
  • Ilboru

  • Tabora Girls
  • Kilakala
  • Msalato

Hizi shule kila mwanafunzi anatamani kusoma hapo, nafurahi Advance level, nimesoma 1 kati shule hizo.

Kuhusu ufundi mbona shule zipo.

  • Musoma Tech
  • Moshi Tech
  • Tanga Tech
  • Iyunga Tech
  • Mtwara Tech

NB: Shule za vipaji zibaki km zilivyo na ziendelee na utaratibu huu.
 
Hujawahi kusoma shule za vipaji maalum ndio maana huwezi kujua uwezo wa wanafunzi wanaotoka shule hizo...
 
Hakuna shule za vipaji hapa, Kimsingi ni shule za watu wenye ufaulu wa juu zilizopachikwa jina la shule za vipaji. Mimi napendekeza kuwepo shule halisi za kuendeleza vipaji.
  • Kibaha
  • Mzumbe
  • Tabora Boys
  • Ilboru

  • Tabora Girls
  • Kilakala
  • Msalato

Hizi shule kila mwanafunzi anatamani kusoma hapo, nafurahi Advance level, nimesoma 1 kati shule hizo.

Kuhusu ufundi mbona shule zipo.

  • Musoma Tech
  • Moshi Tech
  • Tanga Tech
  • Iyunga Tech
  • Mtwara Tech

NB: Shule za vipaji zibaki km zilivyo na ziendelee na utaratibu huu.
 
Katika mfumo wetu wa elimu nchini kuna shule za sekondari ambazo zimekuwa zikijulikana kama shule za vipaji maalumu lakini kiuhalisia zisingepaswa kuitwa hivyo badala yake zingeitwa shule za waliopata ufaulu wa alama za juu katika mitihani.

Kuna tofauti kubwa sana kati ya kupata maksi za juu darasani na kuwa na kipaji fulani. Mtu anaweza kupata maksi za juu katika mitihani na akawa hana kipaji chochote. Mtu anaweza kupata maksi za chini darasani na akawa na kipaji.

Vipaji kwa wanafunzi ni kuweza kubuni na kuunda mashine kwa haraka, kuimba, utunzi na uandishi, uchoraji, uwezo wa juu kimichezo, debate, ujuzi wa lugha tofauti kwa haraka, uchoraji ramani, ubunifu katika kuchanganya kemikali na kuunda vitu vipya n.k

Watu wanaofaulu tu kwa kiwango cha juu mitihani ya darasa la saba na kidato cha nne hawapaswi kutambulika kama watu wenye vipaji bila kuonyesha vitu vya ziada walivyo navyo zaidi ya ufaulu wa mitihani.

Pia serikali iachane na mfumo wa sasa wa kuwatenga wanafunzi katika shule maalum zinazoitwa za vipaji na za bweni kulingana na ufaulu wa juu wa mitihani na badala yake shule hizo zote zifanywe za ufundi na vipaji halisi ile zilite tija katika taifa kwani kwa sasa hazina tija yoyote katika kuzalisha watu watakaochochea mabadiliko ya nchi.
Kipaji chao ni kuweza kufaulu kwa kiwango cha juu kuliko wengine. Is that too hard to understand ?
 
Kuwa na uwezo wa kumbukumbu kubwa hicho nacho ni kipaji mkuu, lakini mtu anaweza kuwa na uwezo mkubwa wa kukumbuka ila akawa na uwezo mdogo wa kuchakata taarifa.
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Shule za vipaji maalumu huo utaratibu uliishaisha zamani sana tu, hakunaga tena mambo ya vipaji maalum ni vile watu wanaziongelea kwa mazoea serikali ilishaondoa hiyo kitu kitambo.
 
Mtoa mada kama sikosei umechukua sehemu tuu ya maneno, wao huwa wanaita "Vipaji maalum kiakili" ..... sasa wewe sijui unafikiria vipaji vya kutengeneza ndege au vya kina Samatta....

Hiyo ndio niliyoikuta Kibaha Sec kwa miaka 6 niliyopitia pale.
 
Huku vyuo vikuu (e.g. UDSM) huna GPA ya 3.8 au zaidi, uhadhiri/uprofesa utausikia kwa wengine.

Naunga mkono hoja ya kuwa na shule za kuendeleza vipaji mbalimbali (michezo, ufundi, sanaa, etc.). But hii haina maana kuondoa shule za walifaulu vizuri (za vipanga aka joni kisomo), hizo ziendelee....zina faida zake na zinatoa motisha kwa watoto kupambana kufanya vizuri katika masomo yao.

Shule za ufundi (Ifunda, Tanga etc) pia ziendelee but ziboreshwe ili zitoe mafundi kweli na sio vyeti tu. Huko pia sio kila mtu anaenda....lazima uwe vizuri kwenye hisabati (labda kama miaka hii utaratibu umebadilika).
 
Watu wengi wakipata motisha na mazingira sahihi wanaweza kukariri kwa kiwango cha juu. Watu wengi wanaoenda shule zinazoitwa za vipaji maalumu hutumia muda mrefu tu zaidi ya wengine kusoma, huwa na vitabu vingi, na hufanya mitihani iliyopita mingi sana.
Ni watu wachache huwa na ule uwezo wa kukumbuka mambo mengi bila hayo yote(hao ndio tungesema ni kipaji)
Kuwa na uwezo wa kumbukumbu kubwa hicho nacho ni kipaji mkuu, lakini mtu anaweza kuwa na uwezo mkubwa wa kukumbuka ila akawa na uwezo mdogo wa kuchakata taarifa.
 
Dah kuna jamaa ana kipaji cha kuiba asee akija kukuibia mbona utajiona mjinga.
Vipi ni hiki ni kipaji maalum au?
 
Hukana shule ya kipaji maalum,wanafunzi wote wanavipaji vyao wakifundishwa vizuri na kuendelezwa.
 
Back
Top Bottom