Mkumbwa Jr
JF-Expert Member
- Mar 23, 2016
- 2,370
- 3,148
Mara zote shule binafsi wanakua vinara katika matokeo ya mitihani aidha darasa la saba au kidato cha nne.
Sababu za matokeo yakiwa mazuri au mabaya zipo kama vile uwezo binafsi wa mwanafunzi, bidii, mazingira, rasilimali vitabu,walimu bora, maabara za kisasa, maslahi bora ya watumishi, mbinu mbalimbali za ufikishaji mada, msukumo wa familia na jamii inayomzunguka mwanafunzi.
Nikijikita zaidi kwenye hoja nikwamba waandishi wa habari walio wengi wamejikita zaidi kuwahoji waliofaulu na kufaulisha.
Wanawahoji wanafunzi walioingia kumi bora. Mfano jana Tanzania One amehojiwa akifuatiwa na mzazi wake na leo asubuhi Channel Ten wamewahoji washindi wawili walioingia kumi bora ambapo wamemhoji mshindi wa tano na mshindi wa kumi.
Ingekua bora zaidi kama wangehojiwa wasimamizi wa zile shule kumi za mwisho pia, baadhi ya waliofeli (kama wakitaka kutoa ushirikiano). Wazazi wa wanafunzi ili changamoto zijulikane, maafisa elimu na hata waziri wa elimu. Waieleze jamii hasa changamoto nizipi na kama taifa tunapunguzaje hii aibu ya kufeli, kupoteza fedha na hasara ya muda kwa miaka minne kisha mtu apate zero
Waandishi wa habari msiishi na kufanya kazi kwa ushabiki. Kueni wachokonozi na watafiti. Mtagundua changamoto nyingi sana ambazo baadhi zingeweza kutatuliwa.
Msikae na kuwaita tu watu studioni, wafuateni huko majumbani kwao mkawahoji juu ya hii aibu ya kufeli. Wapo watakaotoa ushirikiano na MTASIKIA MLIYOKUA HAMYAJUI WALA KUYATARAJIA.
Waandishi wa habari bado hamjaamua kubalance hii story ya kufaulu na kufeli. Mnataka kujua waliofaulu wamefanyaje lakini hamtaki kujua waliofeli wameshukiwa na vitu vyenye uzito kiasi gani vichwani mwao.
Ukiachia sababu kama michujo mikali shule binafsi ikilinganishwa na shule za umma kwamba kuna walioenda kwa ana ana dooo, ninaamini kuna vitu vingine vizito na vyenye ncha kali vinavyowapiga wanafunzi kwenye shule za umma. Vitu hivyo vinaweza kua vyakwao binafsi, mazingira yanayo wazunguka au historia zao na watu wengine kama wazazi, jamii, walimu na hata serikali.
Waandishi wa habari jaribuni kufanya mizania kwenye habari msizame upande mmoja.
Mkiongozwa na hisia kama sababu za kufeli mnazijua basi hata za kufaulu hamuwezi kushindwa kujua maana hizo za kufaulu zipo wazi zaidi na zinazungumzika kila uchao na uchwa
Natoa hoja jukwaani