mgt software
JF-Expert Member
- Nov 1, 2010
- 13,753
- 7,075
Wandugu,
Katika hali ya kustajabisha , kanisa la Roman Catholic limekumbwa na sintomfahamu kwa kujiweka sana karibu na kila dalili za ufisadi. Jambo hili nimekutana nalo baada ya kuangaika sana kumtafutia shule kijana wangu, hasa katika shule za kanisa katoliki ili angalau apate elimu ya dini yake pamoja na masomo yake, cha kushangaza nimekuta karo zinaanzia million 2 mpaka mil 3 kwa mwaka, cha kushangaza zaidi kuna shule za watu binafsi zinaanzia laki 7 hadi 9 na zainafaulisha vizuri tu. Nikawa najiuliza hivi hawa viongozi wa makanisa wanategemea kweli mtoto wa masikini kusoma pale au wanachukulia ule msemo wa aliyenacho ataongezewa, ajabu zaidi ni pale nilipoomba form naambiwa ni elfu 30 na baada ya hapo atafanya mitihani akishinda au kushindwa hizo hela hazirudishi, Maandalizi ya form hayazidi elfu tano lakini tunalipia 30 lakini kwingine ni elfu 10 tu.
Tunakuomba sana Cardinari Pengo kufuatilia shule hizi zenye mlengo wa kuwa karibu na matajiri tu na sisi masikini watufikie , kama ilivyokuwa zamani kwamba kazi ya kueneza injili ni pamoja na kupata elimu bora kwa watu wote.
Pia kuna baadhi ya shule zinazoanza na St. Zina matatizo sana hasa za mkoa wa Morogoro, Kama vile St. Joseph Soga, shule hii imeanza kuaribika kupita kiasi, watoto wanatoroka sana, wanamiliki simu, wanaomba sana pesa kwa ndugu na jamaa sijui wanazifanyia nini. Shule nyingi hazina uzio angalau hata wa michongoma, au sengengenge jambo ambalo ni hatari sana kwa mazingira ya wanaosoma boarding, wengi wanaokuwa karibu na vijiji wanaaribika kwa bangi na vitabia vingine.
Nakuomba Tafakari na chukua hatua ili kanisa letu liwe bora kwa elimu, upendo na thamani.