Shule za Roman Catholic si rafiki tena na masikini, Ada yao ni Zaidi ya Shule binafsi

Kama unataka kuwekeza kwa mtoto wako na ukadhani gharama ni tatizo kwa kulinganisha kiasi cha ada kati ya shule za kikatoliki na binafsi bila kuangalia kiwango cha elimu aipatayo mtoto wako utakua unatengeneza bomu litakalokulipukia mwenyewe.Nenda kafanye utafiti kisha uje hapa na hii dhana ya gharama na kiwango bila kusahau mandhari na malezi mema

Kweli dini zimewaziba watu, zimewafanya vipofu... wajanja kwa kulijua hili wanazitumia dini kufanya biashara... UMENIAMINISHA KUWA DINI ZIMEFANYWA BIASHARA,
 
Basi inabidi ufanye Haya

1..Nenda kiwandani uwaambie Watengeneze Vitabu kwa ajili ya Masikini

2. Nenda Vyuoni waambie Watoe Walimu kwa Ajili ya Masikini wa Bei nafuu

3. Nenda Tanesco waambie watoe umeme kwa Ajili ya Masikini.. Umeme wa Bei nafuu

4. Nenda kwa Wakulima Waambie walime kwa Ajili ya Masikini.. Vyakula vya Bei nafuu


Halafu ndo Uje Ulalamikie Kanisa Katoliki.....


Pili Kama Unaona Kanisa Linatoza Bei Nenda tu kwenye Shule za Milioni 1 mpka 1.5 kuna Tatizo kwani

Mkuu,,,,ukisema namna hiyo unakosea unaweza kuniambia nini Faida ya miradi inayochangiwa na waumuni wote Kanisani.....!!
 
Kanisa katoliki la Roma lipo jirani kabisa na masikini, mie nimesomeshwa hadi chuo na kanisa langu! Gharama kupanda ni kawaida maisha ya sasa sio sawa na ya zamani ati

Wewe unaweza usione wanacholalamikia wenzio kwavile umesomeshwa bure
 
Serikali ilitakiwa kuboresha shule zake ili kuepushia wananchi gharama. Si jambo la kufurahia kuona watu wanakaa kjadiri shule za privates kama vile jambo la kawaida
Nakubaliana na busara zako mkuu. Kusema kweli haya yote chanzo chake ni serikali yetu kuziacha shule zake kukosa viwango na hadhi. Matokeo yake wananchi tunalazimika kuhangaika shule za binafsi kwenye gharama ili watoto wasome vizuri
 
Kweli dini zimewaziba watu, zimewafanya vipofu... wajanja kwa kulijua hili wanazitumia dini kufanya biashara... UMENIAMINISHA KUWA DINI ZIMEFANYWA BIASHARA,

Mkuu mimi sioni tatizo kwa sababu mtu huvuna kutokana na akipandacho ukipanda mbegu bora na ukasimamia vizuri shamba lako ukaweka mbolea pia ukafanya palizi vizuri na ukiwa mwerevu ukajihadhari na mabadiliko ya tabia nchi kwa kujiandaa kuyakabili mabadiliko ni lazima utavuna mavuno mema.
 
Tatizo wenye serikali (decision makers) wamezitelekeza shule za serikali na hata wao hawasomeshi shule hizo

Kwa hiyo kama serikali imetelekeza shule zake ndio ulazimishe shule binafsi zishushe Karo zake kwa kigezo ni shule za kanisa.?

Kama serikali itaboresha shule zake hakuna atakaehangaika na shule binafsi na pia watalazimika kushusha Karo zao maana viwango vyao wanapima toka serikalini.

Usisahau hata kwenye afya ni hivyo hivyo.
 
Kweli dini zimewaziba watu, zimewafanya vipofu... wajanja kwa kulijua hili wanazitumia dini kufanya biashara... UMENIAMINISHA KUWA DINI ZIMEFANYWA BIASHARA,


Tatizo litakuwa huwezi kumudu gharama zao kutokana na ukata ndo maana povu linakutoka mwanzo mwisho.

Watu wanatoa 7 m pale Feza boys wewe unalialia kisa 2m inayotolewa kwa awamu nne.

Mpeleke shule ya kata au hizo za maustadhi akazungushe maana hushikiwi fimbo kumpeleka RC.

.
 

Tatizo litakuwa huwezi kumudu gharama zao kutokana na ukata ndo maana povu linakutoka mwanzo mwisho.

Watu wanatoa 7 m pale Feza boys wewe unalialia kisa 2m inayotolewa kwa awamu nne.

Mpeleke shule ya kata au hizo za maustadhi akazungushe maana hushikiwi fimbo kumpeleka RC.

.

Tatizo si Ada Tu bali Ana Chuki na Mpaka Kanisa Lenyewe....

Lingekuwa ni Ada Angejua Kuna Shule Hiyo ya Feza Boys na Angeacha Kelele zake
 
haya majamaa majanja sana yakitaka kukupiga hela zako wanakamsemo chao. Utawasikia wananukuu biblia. ,mshikeni sana elimu usimwa........,
 
Wewe mleta.mada shule ya Feza Sec Dar es Salaam inatoza o na A level hela ya mwaka mmoja ni hela ya kusomesha.miaka mitatu i.e form one mpaka three st joseph o level Goba. Shule ya Fisadi mama Tibaijuka ini almost five million kwa mwaka. Je hizo ni za kanisa katoliki??!! Hiyo ni mifano michache tu. Peleka mwanao hizo za laki sita mpaka milion!!! Hata za laki tatu zipo. Miziki yake ni matokeo ya o and a level zikishika mkia mnaanza kusema shule za kanisa or mara wakristu upendeleo. Mwal competent gharama yake unaijua?? If you think education is expensive try ignorance.
 
Serious...?


Oui,il a bonne réponse.

Jibu la Pengo ndo lakuamika zaidi.

Sababu mimi wala siyo mkatoliki lakini kwenye ukweli na uhalisia wa mambo huwa sina unafiki.

Kwangu koleo siyo kijiko kikubwa.
 
Wandugu,

Katika hali ya kustajabisha , kanisa la Roman Catholic limekumbwa na sintomfahamu kwa kujiweka sana karibu na kila dalili za ufisadi. Jambo hili nimekutana nalo baada ya kuangaika sana kumtafutia shule kijana wangu, hasa katika shule za kanisa katoliki ili angalau apate elimu ya dini yake pamoja na masomo yake, cha kushangaza nimekuta karo zinaanzia million 2 mpaka mil 3 kwa mwaka, cha kushangaza zaidi kuna shule za watu binafsi zinaanzia laki 7 hadi 9 na zainafaulisha vizuri tu. Nikawa najiuliza hivi hawa viongozi wa makanisa wanategemea kweli mtoto wa masikini kusoma pale au wanachukulia ule msemo wa aliyenacho ataongezewa, ajabu zaidi ni pale nilipoomba form naambiwa ni elfu 30 na baada ya hapo atafanya mitihani akishinda au kushindwa hizo hela hazirudishi, Maandalizi ya form hayazidi elfu tano lakini tunalipia 30 lakini kwingine ni elfu 10 tu.

Tunakuomba sana Cardinari Pengo kufuatilia shule hizi zenye mlengo wa kuwa karibu na matajiri tu na sisi masikini watufikie , kama ilivyokuwa zamani kwamba kazi ya kueneza injili ni pamoja na kupata elimu bora kwa watu wote.

Pia kuna baadhi ya shule zinazoanza na St. Zina matatizo sana hasa za mkoa wa Morogoro, Kama vile St. Joseph Soga, shule hii imeanza kuaribika kupita kiasi, watoto wanatoroka sana, wanamiliki simu, wanaomba sana pesa kwa ndugu na jamaa sijui wanazifanyia nini. Shule nyingi hazina uzio angalau hata wa michongoma, au sengengenge jambo ambalo ni hatari sana kwa mazingira ya wanaosoma boarding, wengi wanaokuwa karibu na vijiji wanaaribika kwa bangi na vitabia vingine.

Nakuomba Tafakari na chukua hatua ili kanisa letu liwe bora kwa elimu, upendo na thamani.
Mkuu unajua mimi nimekushangaa sana?!!

Maana sijaona mtu yeyote aliyekulazimisha kumpeleka huko huyo mtoto wako! Kama hapo jirani yako kuna shule inalipisha laki saba ya nini umpeleke kwenye shule za milioni 2? Shule mkuu ni gharama ulshauliza kuhusu menu ya hao watoto wa hizo shule za laki 7 na hao wa shule za 2m? Asikwambie mtu shule ni gharama, shule ninayoifahamu ambako hata wa kwangu anasoma huko (ya Katoliki) menu yake ni kama nyumbani. Hebu peleleza hizo za laki 7 utakuja utusimulie hapa!!

Unataka shule zetu ziendeshwe kwa matakwa yako wewe? Ulishatusikia sisi wenyewe tunalalamika? Acha hizo mkuu!
 
Dhambi ni dhambi tu, uwe unaimba kwaya na mapambio au Uimbe Haleluya- Ukweli ni kuwa kanisa katoliki tokea kuanzishwa kwake halijawahi kuwa upande wa maskini

Kama Kanisa Katoliki halijawahi kuwa karibu na maskini sijui ni kanisa gani unaloweza kulitaja duniani au hapa nchini ambalo linawasaidia maskini wengi hata kukaribia tu Kanisa Katoliki.

Asilmia zaidi ya 80% ya watoto yatima wote tanzania waliopo kwenye vituo vya malezi wanalelewa na Kanisa Katoliki

Kuna nyumba ngapi za kutunza walemavu na wakoma hapa tz zinazoendeshwa na Kanisa Katoliki, zaidi ya mia....

Kuna vituo vingapi vya afya na hospitali za Kanisa Katoliki

Au unataka kutaja ni yatima, wakoma au maskini wangapi ambao kanisa la Kakobe, mzee wa upako, mama Lwakatare, Gwajima, nk wanawasidia. Je haya "makanisa" ya watu binafsi yamejenga hospitali ngapi na shule ngapi za bei nafuu?
 
Mkuu mbona mimi kijana wangu amepata shule ya katoliki nyegezi sec school mwanza na ada nalipa 900,000/=tu au wewe ni shule ipi unazungumzia?
 
Back
Top Bottom