Shule za nipigetafu na walimu wa vodafasta | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shule za nipigetafu na walimu wa vodafasta

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by It is Sur_Plus, Dec 19, 2010.

 1. It is Sur_Plus

  It is Sur_Plus Senior Member

  #1
  Dec 19, 2010
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 169
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Aman ya Utanzania iwe nanyi wanaJF,
  Ndugu zangu juzi nilikua katika safari ndogondogo za mwisho wa mwaka huku mikoa ya nyanda za juu kusini katika mikoa ya Rukwa, Mbeya ,Ruvuma na Iringa. Kiukweli nilipita katika vijiji takribani 22 katika mikoa hiyo.
  Hali ya hizi shule zetu za nipige tafu zikiwa na walimu wa Vodafasta jamani inatisha, Shule unakuta ina mwalimu mmoja kidato cha kwanza hadi cha nne. Nilijiuliza ni aina gan ya elimu watoto wetu wanapata katika shule hizo au ndo wanaenda kukua tu katika shule hizo?
  Hivi haya magari wanayo tumia waheshimiwa ambayo hayatoi hata lifti kwa japo jirani zao. Na fedha zinazo tumika kuendesha semina zisizo na tija na zile zinazo tumika ktk misafara ya waheshimiwa. Zingeweza kubadirisha shule zetu hzi za NIPIGE TAFU na WALIMU WA VODAFASTA?


  PREASURE LIES NOT IN DISCOVERING TRUTH BUT IN SEEKING IT.
   
 2. It is Sur_Plus

  It is Sur_Plus Senior Member

  #2
  Dec 19, 2010
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 169
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nawasilisha
   
 3. Autorun

  Autorun JF-Expert Member

  #3
  Dec 19, 2010
  Joined: Mar 21, 2008
  Messages: 556
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Nadhan junahitaji kupiga kura ya kutokua na imani na raisi na jopo lake
   
 4. Autorun

  Autorun JF-Expert Member

  #4
  Dec 19, 2010
  Joined: Mar 21, 2008
  Messages: 556
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Nadhani tupige kura ya kutokua na imani na Raisi na jopo lake
   
 5. Autorun

  Autorun JF-Expert Member

  #5
  Dec 19, 2010
  Joined: Mar 21, 2008
  Messages: 556
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  ...
   
 6. It is Sur_Plus

  It is Sur_Plus Senior Member

  #6
  Dec 19, 2010
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 169
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sasa ndugu si ndo tutakua 2nakuza tatizo
   
 7. m

  markus New Member

  #7
  Dec 19, 2010
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wewe mwenye mawazo finyu, na usiyelitakia mema taifa ndo unatakiwa kupigiwa kura ya kutokuwa na imani.
  Raisi ameona mbele na kuweka maslahi ya taifa mbele ndo maana akaanzisha hizo shule. anahitaji kuungwa mkono kwa hali na mali.walimu wanaohitimu wakipangiwa mikoani waende.Na serikali nayo iboreshe maslahi ya walimu na mazingira ya kufanyia kazi pia, ili wavutiwe kwenda huko.Kwa kufanya hayo, lengo la Rais wetu litakuwa limetimia.
  Ila we unayechukia watanzania kupelekewa shule karibu ili wasome kwa urahisi nashindwa kukuelewa. Au kwa sababu wewe hukupata bahati hiyo? au kwa kwa sababu umesoma kwa shida na kuokoteza okoteza viqualifications vyako uchwara ndo maana ungependa na wengine wasisome? Huo ni wivu wa kijinga, na wala huwezi kuendelea kwa staili hiyo.
   
 8. shanature

  shanature JF-Expert Member

  #8
  Dec 20, 2010
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 718
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  unajua tatizo sio shule wala walimu...........shule ipo wapi mazingira gani,,,,hudmagani za jamiii zanazopatikana,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,inauchumi kiasi gani watu wa hapo ni waelewa kiasi gani shughuli zao ni zipi,wanamwako wa elimu kiasi gani ukipata jibu,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,litakuwa sawasawa na mwalimu mmoja/nipigetafu is equvalent to niongezee salio
   
 9. Deodat

  Deodat JF-Expert Member

  #9
  Dec 20, 2010
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 1,279
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145

  Hapo kwenye red: Inaonekana mkuu elimu ya uraia (civics) imekupita mbali, unamzungumzia Rais na serikali kana kwamba ni vitu viwili tofauti, Mtoa mada anasisitiza kuwa serikali (ambayo oinaongozwa na rais) iweke elimu kama top piority na fedhsa zinazotumika kwenye kununua magari ya kifahari yasiyo na umuhimu wowote zipelekwe kwenye kuboresha elimu. Rais wetu kashindwa kuhimiza hii hivyo naunga mkono hoja apigiwe kura ya kutokuwa na imani nae.
   
 10. m

  mamakunda JF-Expert Member

  #10
  Dec 20, 2010
  Joined: Jul 4, 2010
  Messages: 371
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hapo kwenye RED, we unadhani kwa nini vijijini walimu hakuna na mijini wamejaa tele? Wakubwa wetu wangeboresha miundombinu na huduma za jamii vijijini, hilo tatizo la walimu vijijini lisingekuwepo. Kuwepo kwa shule hizo kunazidi tu kuleta matabaka katika elimu, Hivi unafikiria sekondari yenye mwalimu mmoja wanafunzi wanasoma kweli? Wanachoambulia ni watoto wa kike kupata mimba kwa wingi kwa sababu hata hosteli hakuna na wala hakuna ulinzi wa kutosha. Serikali ingelifikilia hili kabla ya kufungua shule
  Maana kuwa na shule nyingi hakusaidii, kikubwa ni quality na si quantity.
   
 11. m

  mamakunda JF-Expert Member

  #11
  Dec 20, 2010
  Joined: Jul 4, 2010
  Messages: 371
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Viongozi wetu wengi ni wabinafsi, wako pale kwa maslahi binafsi.
   
 12. Good Guy

  Good Guy JF-Expert Member

  #12
  Dec 26, 2010
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 4,511
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  bazil mlamba,lowasa,JK hawa watu kufungiwa jiwe la kusagia ngano shingon na kutoswa baharini ni halali yao kwa wanavyoitesa na kuinyanyasa nchi na wananchi wake.
   
 13. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #13
  Dec 26, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,823
  Likes Received: 10,120
  Trophy Points: 280
  Kwa mtu anaetembea huko mikoani na kufuatilia issues za namna hio anaweza kuambulia kisukari au BP maana hutaweza kuelewa hayo mazingira yaliyofikiwa kuiita shule ya... ni ujinga mtupu ni zaid ya chekechea! last month nilikua wilaya mpya ya kilindi-tanga, vilio vitupu, au kilolo-iringa unaweza kuchanganyikiwa ukimuona mjin.. flani anasimama jukwaani na kujisifia upupu! Mungu atusaidie ila haya magenge ya majambazi tunayounda yatatugharimu sana!
   
Loading...