Shule za Kata zifutwe, na Ujenzi zaidi usiendelee kwa shule mpya

BLACK MOVEMENT

JF-Expert Member
Mar 11, 2020
2,687
6,428
Katika moja ya makosa yaliofanyika ni uanzishwaji wa Shule za Kata, hizi Shule zimekuja kabisa kuua elimu nchini na mchango wa hizi shule kwenye kuzalisha wajinga ni mkubwa sana.

Kabla ya Shule za Kata tulikuwa na shule kubwa za Serikali, Shule kama Mkwawa, Tabora Boys and Girls, Karatu , Iliboru na kadhalika na kadhalika.

Hizi shule zilikuwa ni kubwa sana na hata majengo yake yalikuwa ni majengo yenye hadhi ya kuitwa shule kweli na kweli zilikuwa zinazalisha watalamu sana. Shule zilikuwa na Madarasa mengi sana, Labalatories Viwanja vya michezo na hata Magari ya Shule.

Shule kama Karatu Sec ilikuwa mchepuo wa Kilimo, Ile Shule ilijengwa kwa standard ya Chuo kabisa, ina kila kitu cha kuitwa Chuo, Nyumba za Walimu ni za Standard sana, pia na shule nyingine kwingineko huko.

Miaka ya 2000 na kuendelea huko ndio ikaja wazo la shule za kata na Walimu wa Clashing Program zikazalishwa shule balaa kila kata na shule yake. Na kwa sababu ya Siasa wanachozingatia pale na Mdarasa basi hata kama hayana sakafu chini ilimuladi ni Madarasa na walimu waingie wafundishe. Unakuta shule ya kata inawanafunzi 600 na kata ya jirani 500 na nyingine 700 na unaweza kuta Wilaya nzima ina wanafunzi 11, 000 kutoka kwenye shule zaidi ya 15 za kata.

Kwa utitili wa shule za kata kuja kuboreshwa kuendana na mazingira ya sasa ni kazi ngumu saba inahitajika fund ya kubwa sana, kwamba shule ziwekewe mifumo, ziwe na viwanja vya mazoezi, ziwe na Maabara za kisasa kabisa za kujifunzia, ziwe na miundombinu ya kila namna sio leo wala kesho.

Shule za zamani za Serikali mfano chukulia Ilboru au hata hiyo Karatu au Ihungo Sec. Shule kama Karatu Sec ingeboreshwa ingeweza ku accomodate wanafunzi 3000+.

Sasa wilaya kama Karatu zikawa na Shule ya ina ile 4 zinatosha kabisa ku accomodate wanafunzi, hizi shule zinakuwa na kila kitu kinachohitajika cha wanafunzi kujifunzia. Shule zikaaa na Computer Lab, Walimu wa Michezo wa aina zote za miche, Vifaa vya mazoezi kwa vitendo na kadhalika.

Au angalieni Majengo ya shule kama Ihungo, yale ndio mazingira ya shule inavyopaswa kuwa, Shule ikiongezewa nguvu inaweza accomodate wanafunzi 4000 ile.

Serikali badala ya kuendelea kuongeza shule za kata ni bora zikaunganishwa, kata 5 shule 1 au 2 na zikawa ni shule kweli za wakati tuliopo, hii ya kuwa na utitili wa shule sio kukuza elimu ni kuzalisha taifa la wajinga na mbumbumbu.

Dunia ya sasa na tunakoelekea tunahitaji shule ziwe na miundombinu na sio vyumba vya madarasa na Vyoo.

Kwa baadae Serikali ianze kuangalia namna ya kuziunganisha hizu shule za kata na kuja na shule moja au mbili standard kabisa. Shule zingine hizo zifungwe na majengo yabadilishwe kuwa Clinic za wakina mama.

Waasisi wa hili wazo la shule za kata waliangalia benefit za kisiasa zaidi kuliko za Maendeleo ya nchi. Ilipaswa nguvu ziwekwe kwenye ujenzi wa shule standard kwa wilaya na zenye kila kitu, hizi pesa zilizotawanywa kwenye shule za kata zingetosha kujenga shule za viwango kwa kila wilaya.

Tunakoelekea kwa sababu ya siasa zitakuja shule za Sekondari kila kijiji.

Tuishauri Serikali kama kweli inataka kukuboresha elimu lazima iangalie miundombinu na kwa shule za kata zilivyo nyingi Serikali haitaweza.

Mfano mzuri ni shule za Msingi za Serikali sawa zinasaidia sana ila wakati sio rafiki.

Picha : Shule ya Sekondari Ihungo baada ya ukarabati: Picha mtandaoni

FB_IMG_1657977615492.jpg
FB_IMG_1657977587680.jpg
 
Shule hizi ni muhimu kwa mustakabali wa elimu na vijana tatizo ni wazazi kuyakimbia majukumu yao kwasababu binafsi,umaskini,siasa na uzembe.shule hizi zimezalisha wasomi wengi tokea zinaanzishwa mpaka hivi sasa.
Wasomi? Kwenye njanya zipi? enzi za elimu za aina hii zimeisha, zinahitajika shule ambazo vijana watajifunza na kudadisi, usiangakie sijui wamefaulu angalia mfumo mzima na nyakati tulizopo.
 
Kinachoua elimu yetu inchini ni private schools na wala sio shule za kata.

Ningekuwa na mamlaka inchi hii ningefuta shule zote za private.

Wote tukutane kata.

Sent using Jamii Forums mobile app
Swala sio shule za Privatw swala ni kwamba kuna shift ya Dunia kwa sasa na kwa mtindo wa mifumo ya elimu tutalia sana. Usha fika International School hata kutembelea tu? Zile shule kwanza vuwanja vyao vya Mpira huo Pitch ni balaa tupu, njoo kwenye walimu wa Michezo ni wale walio qualify na kazi yao ni hio tu, wana kila aina ya vifaa vya kujifunzia, Sasa Serikali kwa wungi wa shule haitaweza kamwe ni lazima ziunganiswe.

Lazima tuwe na shule ambazo zina muandaa mtoto kwa mambo mengi na sio swala la kufaulu tu.

Kenya unazani ni wajinga kufuta mitihani ya Taifa?
 
Hizo shule zote kubwa kubwa nyingi tulikwiba na nyinginezo zilijengwa kama msaada kwa taifa ili. Sijui kwa nini serikali siku hizi wanapojenga miradi yao mingi wanashindwa kuweka na nyumba za watumishi. Nafikiri shirika la nyumba walitazame ili vizuri.

Hujio wa shule za kata si mbaya ni mzuri. Changamoto ni uwekezaji hafifu unaofanya na serikali kuanzia walimu na nyenzo zinginezo. Inapelekea mapokeo yake kutokutoa majibu.

Sema kiasi fulani zilimkomboa kikwete na ajira za waalimu kwa kila mwaka
 
Napinga hii hija kwa nguvu zangu zote.
Kwanza ujue shule ni wanafunzi na walimu, madarasa hata kama yakiwa ya nyasi sawa tu. .
Kikubwa wadau waendelee kuboresha elimu na kuandaa walimu wanaokidhi mahitaji. Madarasa sio madrasa tutajenga kwa misaada ya wadau wa elimu. .
 
Aisee we jamaa huna akili ivi hujui kwmba population ya watu inaongezeka na shule lazima ziwe nyingi.....mm product ya shule za kata advance Pugu nimekutana na watoto wa iliboru na kibaha advance na chuo hawana maajabu yoyote so sio kweli unachokisema.....
 
Siku Moja zitakuja kuwa magofu.. na pia hakukuwa na haja ya kuharibu walimu wazuri wamekimbia ualimu kwa sababu ya maslahi za kisiasa wamejaza walimu hawana uelewa..wajuzi wamehama kwenye mashirika na taasisi zinazolipa vzr, marehem magufuli ni mfano tosha

Nakumbuka mwl aliyeenda ualimu jamaa wa kwanza mimkoa au kiwilaya alipelekwa teaching.... Zamani hiyo

Majuzi nikasikia kuna mwl wa vida faster Sasa hiv ni afisa taaluma wilaya flan ujinga kabisa. Siasa mbaya sana.

Hata wale wataalamu kabisa wamehamia private school. Namjua mmja kwenye fizikia ni mtamu. Lkn alikinbia miaka ya 90 huko. Kwa Sasa private Moja wanamtumia. Na ndio maana madaktari kwenye upande wa PCB ukicheki utaona wanatokea private school
 
Unachoongea kina maana kwa mbali

Kwa sababu izo shule kama unaweza kuzijataja ni kwamba kuna sehemu zilijengwa na kwingine kujengwa shule za kata ila kufanya elimu za sehemu fulani kuwa duni hii ilikuwa ni agenda tangu enzi za nyerere
 
Wazo la kufuta shule za kata siyo zuri.

Nilisoma Karatu Sec School miaka ile shule inaanza, ilikuwa shule ya kilimo. Namkumbuka Mwalimu Mbise (ambaye alikuja kupata ajali, ni kama alilazwa KCMC kwa miaka mingi sana till he died, Rest well Mwalimu Mbise)

Huyu bwana alikuwa mwalimu wa kilimo, eneo lile lilikuwa kubwa, tulilima ngano sana kulikuwa na kila aina ya trekta ya kulimia, kupanda, kupalilia, hadi kuvuna, Mbise alimudu hii kazi.

Sikujua ni nini kilichokuja kuharibu huu mfumo ila kwa ushauri tu ni vizuri urudishwe.

Shule za kata, ni shule nzuri sema mtoto awe smart na ajue alichofuata shuleni.

Nina mfano mzuri wa binti yangu, alisoma mshikamano primary, then kiluvya secondary alipokutana na mwalimu aliyemtanfika fimbo zaidi ya 20 baada ya kuwakuta wamechelewa shule wakajificha mtaroni.

Kiluvya alipata division three, akapangiwa Mungai mafinga huko high school, hizi zote ni za kata.

JJ Mungai alipata division one ya point saba,

Then to jkt mlale,

Sijui ubaya wa shule za kata, cha kusema ni serikali iweke waalimu wazuri pia mazingira yaboreshwe.

All in all, this is challenge and I should vote to you.

Hongera mwaya.
 
Chukulia mfano Karatu Sec yes Je unazani Kuna shule ya Kata inaweza fikia ile levo leo hii hata wakisema warudishe kilimo? Jibu ni hapana kwa sababu kwanza ziko nyingi sana.

Na kumbuka kwa wakati huu wa sasa mambo yamebadilika sana, hadi 2030 zaidi ya kazi Million 800 zitakuwa zimechukuliwa na mashine au roboti, most of kazi za Offisi zinaenda kuisha na tusha anza kuona.

Bila kuwa na shule ambzo zilo equiped unazani tutaweza toboa?

Shule zetu zinaandaa watoto wafaulu mtihani waende Chuo kikuu basi hakuna kitu kingine wanaandaliwa
 
Wazo la kufuta shule za kata siyo zuri.

Nilisoma Karatu Sec School miaka ile shule inaanza, ilikuwa shule ya kilimo. Namkumbuka Mwalimu Mbise (ambaye alikuja kupata ajali, ni kama alilazwa KCMC kwa miaka mingi sana till he died, Rest well Mwalimu Mbise)

Huyu bwana alikuwa mwalimu wa kilimo, eneo lile lilikuwa kubwa, tulilima ngano sana kulikuwa na kila aina ya trekta ya kulimia, kupanda, kupalilia, hadi kuvuna, Mbise alimudu hii kazi.

Sikujua ni nini kilichokuja kuharibu huu mfumo ila kwa ushauri tu ni vizuri urudishwe.

Shule za kata, ni shule nzuri sema mtoto awe smart na ajue alichofuata shuleni.

Nina mfano mzuri wa binti yangu, alisoma mshikamano primary, then kiluvya secondary alipokutana na mwalimu aliyemtanfika fimbo zaidi ya 20 baada ya kuwakuta wamechelewa shule wakajificha mtaroni.

Kiluvya alipata division three, akapangiwa Mungai mafinga huko high school, hizi zote ni za kata.

JJ Mungai alipata division one ya point saba,

Then to jkt mlale,

Sijui ubaya wa shule za kata, cha kusema ni serikali iweke waalimu wazuri pia mazingira yaboreshwe.

All in all, this is challenge and I should vote to you.

Hongera mwaya.
Zaidi ya shule zetu kuandaaa watoto wafaulu mtihani ambao na wenyewe unatungwa chini ya mitala mibovu je kuna cha zaidi wanatoka nacho shuleni? Au ni lazima tena waende VETA?
 
Back
Top Bottom