Shule za Dar kushika mkia matokeo ya kidato cha Nne, Makonda jitafakari na ikiwezekana jiuzulu

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
pic+matokeo+dar+es+salam.jpg

Hakika jiji la Dar es Salaam linatia huruma katika sekta ya Elimu, miundombinu mingi imewekezwa Dar lakini bado sekta ya Elimu bado iko hoi bin taaban...

Kuna mikoa hutoa sababu ya kuwa waalimu wanawakimbia na kukimbilia mjini lakini hapa Dar watoto wanachemka kwa sababu gani?

Mkuu wa mkoa jitafakari upya ikiwezekana jiuzulu kwa aibu hii.....

Pia nasubiri tamko la PM kwakuwa matokeo ya kidato cha pili baada ya Mtwara kuchemka vibaya sana aliagiza uchunguzi ufanyike.......
 
Mbona hizo shule zenyewe hazijulikani

Zitakuwa za mikoani tu Dar wamesingiziwa
 
Hata ukichukua wanafunzi wote ambao wana akili sana ukawapa paper lazima apatikane wa kwanza mpaka wa mwisho hiyo ndio utaratibu wa evaluation

Vinginevyo hakuna maana ya mtihani tena

Examination is for evaluation and ranking haiwezekani wote muongoze lazima wa mwisho apatikane tu
Sasa inakuwaje matokeo ya kidato cha nne ufaulu mbovu utoke katika shule za mkoa wako tena katika shule kumi mkoa wako unakuwa nazo 6
 
Back
Top Bottom