Shule za akademia na kudumaza kwa vipaji vya watoto wetu

namraroh

Senior Member
Sep 9, 2010
112
122
Habari za mchana wanabodi, hongera kwa waliofanikiwa kufunga mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhan mpaka siku ya leo, hakika mola yupo nanyi! Baada ya salamu hiyo napenda kutoa maoni yangu machache kuhusu hizi shule zetu zinazoibuka kila siku kwa jina english medium, kwa kweli napenda kukiri kwamba uwepo wake umechangia sana kupanua wigo wa upatikanaji wa elimu kwa umma wa Tanzania, kwani zimesaidia sana kuziba pengo ambalo serikali kwa namna moja imeshindwa kutimiza wajibu wake kwa jamii.

Shule hizi zimeongeza idadi ya vijana wanaopata elimu ya msingi na sekondari na pia kuleta msisimko katika tasnia nzima ya elimu katika taifa letu, pamoja na ukubwa wa gharama zake lakini wazazi wengi wamejitahidi kuhakikisha watoto wao wanapata fursa hii adhimu ya kuwapeleka watoto wao katika shule hizo kutokana na ukweli kwamba mazingira yake yanavutia na yanasadikisha upatikanaji wa elimu bora na ya uhakika.

Pamoja na ubora wa vifaa, majengo na miundombinu mizuri iliyopo katika shule hizi, baaadhi ya shule hizi zinaendeshwa kwa mtindo wa mashindano ya kuoneshana nani bora zaidi ya mwingine ili kuvutia wateja wengi, na hili wazazi ndio tunachangia sana kwani tunavutiwa na shule inayoongoza bila kudadisi kuhusu ubora wa elimu wa wanaopita hapo!

Kumekuwa na mtindo kufundisha ili kufaulu katika mitihani ya kitaifa pasipo kuonyesha jinsi gani wanafunzi wao wameendelezwa katika vipaji vyao! wanafunzi wanafundishwa kukariri mitihani ili washinde na kuongoza katika ngazi za kiwilaya, kimkoa na kitaifa, ili hali kwenye ujuzi na maarifa ya kujietegemea katika masomo na kupata maarifa kutokana na walichojifunza hakipo, hapa nina imanisha kwamba wanafunzi wengi wanapoteza vipaji vyao wa minajili ya kufaulu mitihani ili kuendelea ngazi ya elimu inayofuata pasina maarifa na ujuzi wa kukabiliana na mazingira ya darasa linalofuata.

Mfano mzuri ni wanafunzi wanaotoka katika shule za akademia na hawa wanaotoka shule za kawaida wanapojiunga na vyuo vikuu, tumeshuhudia wanafunzi wengi wanaotoka katika shule za kawaida wakifanya vizuri katika masomo yao cha vyuo vikuu kadri siku zinavyokwenda tofauti na hawa wa akademia ambao wanapoanza vyuo vikuu wanakuwa wazuri lakini kadri siku zinavyokwenda wanaanza kupoteza mwelekeo.

Hapa tatizo kubwa inaonekana kwamba watoto hawa wa akademia hawana ujuzi wala maarifa ya kujifunza wenyewe kwani wamezoeshwa kulishwa/kumezeswa past papers na kufanya marudio na sio kutafuta vitabu na kujisomea kama hao wenzao wanaotoka shule za kawaida(kanumba).

Inafahamika kabisa kwamba kwenye shule zetu za kata waalimu hawana muda wa kutafuta past papers bali wanafunzi wanahangaika wenyewe na kutafuta vitabu na hizo papers na kufanya marudio wao kwa wao, na hivyo kuwajengea uwezo wa kupambana na hali yoyote ya kimasomo inayojitokeza.

Ni muhimu sana kwa wazazi tujitahidi kuahakikisha wakati watoto wetu wanapokuwa likizo tunajitahidi kuwatafutia vitabu wasome na tuhakikishe kwamba wanavisoma kweli, ilibidi inabidi uwe umekipitia ili uweze kumuuliza baadhi ya maswali vinginevyo tutakuwa tunatwanga maji kwenye kinu, najua wapo watakaosema kwamba tunatafuta pesa ili walimu wafanye kazi zao lakini nawakumbusha watoto sio wa walimu bali ni watoto wetu!

Nawatakia Idd Mubarak in advance!
 
Naisi kuna tofauti kati ya English medium na academy.

Ila ulichokisema kina weza kuwa na ukwel kwa kiasi flan.
 
Naisi kuna tofauti kati ya English medium na academy.

Ila ulichokisema kina weza kuwa na ukwel kwa kiasi flan.

Kwamba waliotoka kwenye shule za kawaida wanafanya vizuri zaidi kuliko waliosoma shule za English Medium?
 
Hiyo ilikuwa zamani. Kwa sasa mambo yamebadilika.

Mwanafunzi wa medium anaingia chuo kikuu akiwa anafahamu mambo mengi kutokana na kutoka katika mazingira mazuri ya kujifunzia.
 
Hiyo ilikuwa zamani. Kwa sasa mambo yamebadilika. Mwanafunzi wa medium anaingia chuo kikuu akiwa anafahamu mambo mengi kutokana na kutoka katika mazingira mazuri ya kujifunzia
Ni kweli wanaingia chuo kikuu wakijua mambo mengi ya walipotoka lakini sio kwa level ya chuo kikuu! Pili wanapoanza chuo wanaanza vizuri lakini kadri siku zinavyokwenda wanapoteza mwelekeo kwani hawana orientation ya kujifunza kupitia vitabu vya rejea
 
Back
Top Bottom