Shule yajengwa ndani ya saa nane baada ya Rais Magufuli kuunguruma

Pain killer

JF-Expert Member
Aug 15, 2017
4,559
2,000
Habari wakuu

Nashindwa kuelewa hivi hawa viongozi wetu akili zimedumaa namna hii, ubunifu hakuna kabisa, nahisi mh rais kuna wakati anajuta kuwateua, wanamwangusha sana, sijui ni woga.

ile shule ya ubungo, baada ya Rais kusisitiza, huwezi amini, sijui pesa imetoka wapi, budget sijui nan katenga, malori ya mchanga, cement, kokoto, zimemwagika ndani ya sekunde moja, shule imejengwa hadi miti imepakwa rangi ya kijani, shule ilikuwa na bonde halipitiki daraja safi limejengwa ndani ya nusu saa.

Hapa ndio nimeamini kuwa sisi watanzania ni kama punda, sio kwamba kufanya kazi hatuwezi ila anahitajika mtu nyuma na mjeredi na mkong'oto mkali wa kama jpm wa kucharaza bakora hawa watendaji wavivu ambao hawana ubunifu wapo wapo tu kama maji ya kandolo ubungo.

Saizi kila mwanchi anatamani arecord kero zinazosumbua mtaani na kumpelekea moja kwa moja mh rais, kwa sababu
Mwenyekiti hovyo:
  • Diwani hoi
  • Mkurugenzi hana maamuzi
  • Mkuu wa wilaya ujanjajanja mwingi
  • Mkuu wa mkoa hajui la kufanya
  • Mbunge haelewi

Wote hao kama vile kuna kitu kimekamata uwezo wao wa kutatua changamoto za wananchi.

Mungu ibariki Tanzania.
 

ZALEMDA

JF-Expert Member
Aug 15, 2017
873
1,000
Kuna sehemu Rais kaahidi barabara ya lami kuelekea hospitali fulani huu ni mwaka wa pili sasa hakuna kilichofanyika cha maana. Sijui tatizo ni nini? Walikuja kipindi cha uchaguzi wakajifanya wanatengeneza baadaye wakaishia mitini. Labda kipindi cha mvua barabara hazijengwi maana mie siyo mtalaamu wa ujenzi wa barabara.

But in short, sisi watanzania ni wavivu kufikiri au kuwa wabunifu. Tofauti kabisa na Mkenya. Ukimwajiri mkenya unainjoyi sana. Kumuongoza mtanzania inaitajika kutumia nguvu kubwa kama siyo bakora. Hivi kama mtu anakosea hata kujaza form ya uteuzi unategemea nini kwa mtanzania wa aina hii?
 

paul sylvester

JF-Expert Member
Mar 18, 2020
3,480
2,000
Dar! Bado haijapata viongozi

Yule mkuu wa mkoa wa Simiyu anapaswa awe Dar!

Sisi Tanzania, Dar ndilo jiji kubwa na linalopokea wageni wengi kuliko jiji lingine hapa, na ndilo jiji la mfano, shida ni halijapata viongozi wabunifu
 

mzamifu

JF-Expert Member
Mar 10, 2010
5,224
2,000
Tatizo ni pesa hakuna halmashauri isiyotaka kufanya hayo. Hapo ni kuwa kumefanyika misallocation of fund.. ndio kusema hatuwezi maliza matatizo kwa mtindo wa zimamoto.
Umesema sawa. Ziko shule nyingi mbovu but hazijafikiwa na media na hatimaye rais. Ni vigumu kufanya sawa kwa njia maagizo.
 

mama D

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
8,976
2,000
Ok fine . Kwahiyo hakuna Tena ndani ya halmashauri ya ubungobau dar nzima sehemu yenye changamoto? Yani mnapelekshwaa na sinema za ccm

Kwani mbona kama hujapenda hiyo shule inavyojengwa? Huwezi appreciate hata hili zuri kati ya hayo unayoona ni mabaya!? Na bado likiwa baya utashangilia kwamba serikali imeshindwa kufanya kazi yake🤔

Haya ngoja nikujibu swali lako, ubungo changamoto bado zipo na zitaendelea kuwepo ila shule ni moja ya priorities sababu watoto wanatakiwa kuwa darasani

Nina uhakika hata hapo kwako changamoto zipo na haziwezi kwisha, tena changamoto zinazosababishwa na wewe mwenyewe... kikubwa zipe priority kama ubungo
 

Inside10

JF-Expert Member
May 20, 2011
21,946
2,000
Umesema sawa. Ziko shule nyingi mbovu but hazijafikiwa na media na hatimaye rais. Ni vigumu kufanya sawa kwa njia maagizo.
Kwahiyo ufumbuzi Hadi ufanyike Hadi media hakuna bodi za shule, maafisa elimu n.k
 

mama D

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
8,976
2,000
Mama D, ukumbuke matofali kusubiriwa yakauke kwenye maungio haijalishi nani katoa amri..!!! Hata zege kusubiri likauke haijalishi nani kasema, lazima lisubiriwe..!! Madhara yake tutakuja yaona
Mbona ubungo suppliers wa tofali ni wengi sana!?

Hata kama wanatengeneza zao wenyewe bado wanaweza kuwa wanachimba msingi huku idadi ya to tofali ikiongezeka

Wananchi tuondoe vikwazo vya fikra kila kitu kinawezekana
 

mrangi

JF-Expert Member
Feb 19, 2014
52,792
2,000
Huo sio mkurupuko ni kuwajibishana
Haina kungoja wala kusubiri
Tatizo siku hizi halmashauri hazina fedha.

Na fedha yote inakwenda hazina,ukisema uombe fedha hazina kuna process na inaleta delay.

Utakuta hata wakitaka pesa ya kuweka vitasa waombe hazina ....inawezekana pia hiyo ni tatizo.

Ova
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom