Shule Yafungwa Kwa Kukosa Chakula

Mgoyangi

Senior Member
Feb 6, 2008
184
9
Nimeangalia kwenye runinga habari ya kufungwa kwa shule ya Sekondari ya Pugu, kutokana na kukosa Msosi baada ya wazabuni, kususa kuendelea kutoa huduma bila malipo ama kwa LPO yaani Lipa Polepole Ofisa.

lakini pia naangalia kwenye habari makala kuu ya Rai naona jinsi wabunge wanavyolipwa mamilioni, hivi tunakwenda wapi? Siyo kwamba tunajenga jamii ya kifisadi, maana mtoto anayesoma katika mazingira ambayo anaona jamii hamjali, akikuwa lazima atakuwa mla rushwa!
 
ZAIDI ya wanafunzi 200 wa kidato cha tano na sita katika Shule ya Sekondari ya Ufundi Moshi, wamelazimika kusitisha masomo yao kwa muda usiojulikana kutokana na upungufu wa chakula unaoikabili shule hiyo.

Wanafunzi wanatakiwa kuondoka shuleni hapo kuanzia leo na kwamba watafahamishwa muda wa kurejea shuleni kupitia vyombo vya habari.

Kwa mujibu wa barua ya Mkuu wa Shule hiyo, Isack Malisa iliyosainiwa na Makamu Mkuu wa Shule, Sigfrid Saweru yenye kumbukumbu namba MTS/R.20/VOL.IV/59 ya Desemba 17, mwaka huu, kwenda kwa wazazi wa wanafunzi hao shule hiyo itafungwa rasmi leo.

Katika barua hiyo Mkuu wa shule alisema uongozi wa shule hiyo hautaruhusu mwanafunzi yeyote kubaki shuleni kwa muda wote ambao shule itakuwa imefungwa.

Source NIFAHAMISHE Tanzania news portal
 
Hivi kwa mambo kama haya ya kufunga shule kwasababu hakuna chakula tutafika kweli?
Inatia uchungu kuona mashangingi na magari ya kifahari yananuliwa kama kawaida wakati wanafunzi wanakosa masomo kwasababu serikali inashindwa kutoa chakula kwa shule
 
Shule za boarding zimekuwa zikufungwa kwa muda mrefu kabla ya kumaliza muhula wake kutokana na tatizo la vyakula....

Longido primary school katika miaka ya 80 ilikuwa ikifungwa mara kwa mara na ni Marehemu Sokoine aliyekuwa akisaidia wakati fulani kutofungwa kwa shule hiyo.

Miaka ya themanini shule kibao zilizoota kama uyoga wa masika zilijikuta zikikumbwa na dhahama hiyo hiyo...
 
Hivi Kumbe Malisa bado ni Headmaster wa Moshi Technical? Hata akiwa Lyamungo shule ilikua ikifungwa kabla ya muda.Wakati mwingine hata holiday ilikua inarefushwa kuliko shule nyingine.Kuna kipindi shule ilikua na holiday ya miezi miwili na wiki tatu

Angalao alipohama hapo Nicholaus Burreta akawa Headmaster Mpya wa Lyamungo,mambo yalikua shwari na academic performance ilikua juu kiasi cha kuichangamsha hata Ilboru.Sasa huyu Malisa kipindi hicho sijui alikua na sababu gani.Najua serikali imezembea kwa kiasi flani lakini hata huyu Malisa ana matatizo binafsi
 
Ukiona serikali inanunua magari ya fahari 700 wakati shule zinakosa vyakula, basi ujue kuwa kuna tatizo somewhere between serikali iliyoko madarakani na wapiga kura walioiweka serikali hiyo madarakani.

Na bado kuna mtu anatumia muda mwingi kutaka kujua ni kina nani wanaandika hapa JF badala ya kufanya bidii kulisha na kusomesha watoto walioko mashuleni.

Grrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr
 
Duh huyu mzee wangembadilisha
BTW-Hii shule ina wanafunzi wengi sana
 
Ukiona serikali inanunua magari ya fahari 700 wakati shule zinakosa vyakula, basi ujue kuwa kuna tatizo somewhere between serikali iliyoko madarakani na wapiga kura walioiweka serikali hiyo madarakani.

Na bado kuna mtu anatumia muda mwingi kutaka kujua ni kina nani wanaandika hapa JF badala ya kufanya bidii kulisha na kusomesha watoto walioko mashuleni.

Grrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr

Mwafrika upo sawa kabisa.Kuna mahali tatizo lipo.Shule ni nyingi zinazofungwa na hata same imefungwa juzi! Kuna ambao japo ni form 6 wanatakiwa kurudi almost 10 days before their national exams! Still our leaders shouts daily in public that we be patriot! There is good reason for strikes in this country untill some thing is done!
 
Hivi Kumbe Malisa bado ni Headmaster wa Moshi Technical? Hata akiwa Lyamungo shule ilikua ikifungwa kabla ya muda.Wakati mwingine hata holiday ilikua inarefushwa kuliko shule nyingine.Kuna kipindi shule ilikua na holiday ya miezi miwili na wiki tatu

Angalao alipohama hapo Nicholaus Burreta akawa Headmaster Mpya wa Lyamungo,mambo yalikua shwari na academic performance ilikua juu kiasi cha kuichangamsha hata Ilboru.Sasa huyu Malisa kipindi hicho sijui alikua na sababu gani.Najua serikali imezembea kwa kiasi flani lakini hata huyu Malisa ana matatizo binafsi

Mkuu Ben
Unaweza kuwa sawa ila kumbuka shule zilizofungwa ni nyingi. Tatizo ni hii shule moja imeripotiwa rasmi. Nyingine zimefungwa bila kuita waandishi wa habari. Ukiona hata waziri hajatoa tamko, na hakuna mwandishi aliyejitokeza kuhoji zaidi ya kuripoti jua ndo utaratibu wa Kitanzania ambao tumeuzoea
 
Heshima yako mkuu,
Moshi tech. ninayoifahamu mimi kuishiwa chakula na kufungwa, tatizo haliwezi kuwa serikali tu kushindwa kuwalipa wazabuni na mambo kama hayo, bali pia tatizo hilo litakuwa limechangiwa kwa kiasi kikubwa na huyo mkuu wa shule. Binafsi simfahamu huyo Malisa ila Saweru ninamfahamu vizuri sana maana alikuwa mwalimu wangu wa Basic mathematics na ama kwa hakika alikuwa mwalimu shupavu sana kwenye eneo lake la mathematics.Labda nitumie nafasi hii kumpongeza kwa kufikia nafasi ya kuwa makamu mkuu wa shule.
Shule ya sekondari Moshi ufundi ina eneo lkubwa sana la kilimo(kwa maana ya shamba).Miaka ile tunasoma pale tulikuwa tunalima shamba lile na liliweza kusaidia sana kupunguza utegemezi wa serikali kwa upande wa chakula.Mwanzoni mwa miaka ya tisini kulitokea pia tatizo la chakula karibia nchi nzima na shule nyingi zilifungwa lakini Moshi tech. haikufungwa kwa kuwa ilikuwa inajitosheleza kwa chakula(mahindi). Enzi za mzee Malale na baada ya kustaafu akaja marehemu Kimario ile shule ilikuwa na mipango mizuri sana na kuweza kuisaidia kupunguza makali ya uhaba wa chakula.Na zaidi ya hilo shamba, moshi tech, ilikuwa na karakana ambazo zilikuwa ni productive hususan ile ya "wood work", "Welding", "Motor vehicle", Arctectural drawings", n.k ambazo zilikuwa zinaiingizia shule pesa nyingi sana. Kwahiyo basi naweza kuungana na mwenzangu hapo juu kwamba bwana malisa anahusika kwa namna moja ama nyingine kusababisha shule kufungwa kwa ukosefu wa chakula.
Lakini mwisho wa yote ni kwamba serikali haitambui umuhimu wa elimu kabisaaa, ndio maana iko radhi kununua mashangingi 700 kuliko kununua chakula cha wanafunzi.
Ni wajibu wetu wananchi kuipima serikali yetu kama inatekeleza yale iliyotuahidi na yale inayopaswa kufanya ama inafanya usanii na elimu yetu, kisha ukifika mwaka 2010 kura zetu ziwahukumu kwa haki.
 
Mwita uko right,shule ina shamba kubwa sana la mahindi labda hali ya hewa haikuwa nzuri
Hizo karakana zilizokuwa zinazalisha sasa hivi hakuna kitu shule ina mradi wa mashine ya kusaga
Serikali pia ni ya kulaumiwa sababu hii shule ni moja ya shule yenye wanafunzi wengi mno nakumbuka kuna wakati olevel wakikuwa karibia 900 na a level walikuwa kama 50 kwa sasa naskia a level wameongezeka kuna combination 2 pcm na pcb
 
Well said Belo,
Lakini kama karakana zote zimekufa na wamebakiwa na mradi wa mashine ya kusaga, ndio kusema kuwa hata duka la shule nalo limekufa????
Na kama hali ndivyo ilivyo, basi tatizo haliwezi kuwa la serikali pekee, hata kama hali ya hewa ilikuwa mbaya kiasi hicho, wangeweza basi kuvuna hata kiasi fulani kingeweza kuwasogeza mbele.Na kama karakana ambazo zilikuwa zinaiingizia shule pesa nyingi nazo zimekufa hapo mkuu wa shule pamoja na bodi ya shule wanatakiwa kuwajibika, kwakuwa wanatakiwa kuwa na mipango endelevu, sio kusubiri vikao vya kufukuza wanafunzi shule.
Mbona shule nyingine kama umbwe,lyamungo, old moshi, n.k hazijafungwa??
Na hizo ni shule ambazo ziko jirani tu, kama ni hali ya hewa kuwa mbaya na wao hawana pa kuponea.
Uongozi wa malisa kuwa mbovu haiishii tu kwenye chakula, angalia hata academic performance ya moshi tech. sasa hivi iko chini sana ukilinganisha na miaka ile hajahamishiwa hapo.Kwa kweli ni aibu kwa shule kama moshi tech. kufungwa kwa ukosefu wa chakula.
 
Mwita nakuunga mkono Mzee Malale aliiweza sana hii shule hata Kimaro but tangu amekuja Malisa kazi yake ni kufukuza wanafunzi na mara nyingi hayupo shule so Mpande(Mwalimu wa michezo) anakuwa kama mkuu wa shule sijui kama bado yupo
Kuna wakati wanafunzi wakiwa darasani wapishi wanaiba chakula wanapeleka nyumbani kwao mkitoka darasani unaona punje za mchele zimemwagika kuelekea kwenye nyumba zao lakini hawafanywi lolote

Duka la shule wanauza suari,stationary na wanafunzi wengi wananunua vitu nje ya shule
 
Back
Top Bottom