Shule ya udereva wa magari kwa mda mfupi Dar es Salaam

Engineer E.

Member
Mar 1, 2015
34
2
Jamani wana JF nahitaji kujifunza udereva wa magari kwa mda mfupi kutoka Dar es salaam kwasababu mm mwenyewe nipo dar es salaam, nahitaji mnitajia mda wa kumaliza hayo mafunzo ndani ya kipind kifupi pamoja na ada yake na iwe wilaya ya kinondoni.
 
Mlimani School of driving, ofisi zipo mkabala na Kanisa la Kakobe njia Ya Sam Nujoma kuelekea mwenge. Shukia lufungila kituo cha daladala centre ya mafunzo ipo pale ilipo Yard ya Magari na Baiskeli nyingi inaitwa Top Car Junction Yard. Hapo ni siku 20 tu umekuwa dereva makini, mafunzo yao ni kwenye highway ya Sam Nujoma, MwaiKibaki, Sinza Mori na mwendo mrefu ni mpaka Ununio huko bunju, walimu wenye kujituma na wazoefu gari zao ni baloon mpya aina za Nissan, na kuna mitsubishi pajero mbili mpya, hawana magari machakavu kama centre zingine. Ada yao sasa ni 250,000/= mannual na 300,000/= Automatic. Kila jumamosi ni Test za kuandika darasani na Ukaguzi wa vifaa vya gari na makorokoro mengine.
 
Mimi ni dereva lakini nawish kujiunga na hao Mlimani Driving school. Je hawana sessions za jioni au weekend?
 
Pale ni wewe ndio unapanga muda wako wa mafunzo, iwe alfajiri, asubuhi, mchana, alasiri au jioni mafunzo mwisho saa kumi na mbili unusu jioni, ifahamike kwamba kila ukifika una dakika 30 barabarani na dakika 30 darasani ukisoma alama na michoro ya barabarani.
 
Mlimani School of driving, ofisi zipo mkabala na Kanisa la Kakobe njia Ya Sam Nujoma kuelekea mwenge. Shukia lufungila kituo cha daladala centre ya mafunzo ipo pale ilipo Yard ya Magari na Baiskeli nyingi inaitwa Top Car Junction Yard. Hapo ni siku 20 tu umekuwa dereva makini, mafunzo yao ni kwenye highway ya Sam Nujoma, MwaiKibaki, Sinza Mori na mwendo mrefu ni mpaka Ununio huko bunju, walimu wenye kujituma na wazoefu gari zao ni baloon mpya aina za Nissan, na kuna mitsubishi pajero mbili mpya, hawana magari machakavu kama centre zingine. Ada yao sasa ni 250,000/= mannual na 300,000/= Automatic. Kila jumamosi ni Test za kuandika darasani na Ukaguzi wa vifaa vya gari na makorokoro mengine.
Kaka mm nipo kitunda banana ukonga pls mm kijana wa miaka 23 nafanya tu kazi za garden kwa binamu yangu ila ndoto yangu ni kuwa dereva wa magari makubwa yaani maroly na busi nilimwbia kaka yangu uyo mbaeni mtoto wa mjba wangu akanibia sawa lakini utakuwaunakaa wapi na kazi unaacha na pesa ya kulipia utaitoa wapi nikajua tu uyu hataki mm nikajifunze magari ila kwa sasa nimesha jichanga changa naomba msaada naweza kupata wapi maala wanafundisha ayo magari makubwa na ni shingapi garama na nikwa mda gani ..natanguliza shukurani
 
Pale ni wewe ndio unapanga muda wako wa mafunzo, iwe alfajiri, asubuhi, mchana, alasiri au jioni mafunzo mwisho saa kumi na mbili unusu jioni, ifahamike kwamba kila ukifika una dakika 30 barabarani na dakika 30 darasani ukisoma alama na michoro ya barabarani.

Jombaa mbona hukumjibu hiyo dogo wa comment namba 6 hapo juu?

Halafu kina mtu kasema bora kwenda NIT sababu ada yao 100,000 tu. Wewe unasemaje. Nisaidie ushauri ndugu
 
Back
Top Bottom