Shule ya Tusiime inaelekea kubaya/inachungulia kaburi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shule ya Tusiime inaelekea kubaya/inachungulia kaburi

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Kashaija, Jun 10, 2011.

 1. K

  Kashaija JF-Expert Member

  #1
  Jun 10, 2011
  Joined: Aug 7, 2008
  Messages: 255
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mpaka kufikia mwaka 2005, shule ya TUSIIME iliyoko Dar es salaam maeneo ya Tabata Segerea ilikuwa inavutia sana wazazi kupeleka watoto wao kutokana na mambo kadhaa kama; Ada ilikuwa ya kawaida, Idadi ya watoto kwa kila mkondo kati ya 25 hadi 30, walimu kujituma na kufuatilia wanafunzi kimasomo (diary ilijazwa kila siku na kukaguliwa kesho yake), chakula kizuri kinachozingatia diet, usafi wa mazingira ulikuwa wa kuridhisha, usafi wa vyoo ulikuwa wa kuridhisha na idadi ya matundu ya choo ilitosheleza idadi ya watoto, n.k

  Sasa hivi mambo ni tofauti sana, Ada haishikiki (mwanzoni mwa mwaka jana ilipandishwa kwa takribani asilimia 30 bila maelezo yoyote ya kina kwa wadau/Wazazi), chakula siku hizi ni ugali maharage j3 hadi Ijumaa (hata hivyo chakula chenyewe hakitoshi, ni scramble kwa kwenda mbele, wale watoto legelege mara nyingi hushinda njaa, Ufuatiliaji wa walimu kwa wanafunzi umepungua sana kiasi kwamba hata kwenye diary hawaandiki na hata kama mzazi utawaandikia hawakujibu, Vyoo vichafu pia watoto wanapanga foleni, hakuna tena eneo la watoto kuchezea japokuwa kila Ijumaa wanavaa nguo za michezo n.k

  Kwa kuwa mimi ni mdau katika shule hii (watoto wangu wawili wanasoma pale), juzi juzi nilijaribu kudadisi pale shuleni ili kujua ni nini hasa chanzo yote haya. Kati ya walimu watatu nilioongea nao kwa nyakati tofauti walikuwa na mtazamo unaofanana, kwamba ni UBINAFSI WA MWENYE SHULE. Kwamba pamoja na wazazi kulipa Ada kubwa, bado walimu wameendelea kupewa maslahi duni ikiwa ni pamoja na mishahara, na hivyo wengi wao wamekata tamaa na wengine wameanza kuikimbia shule.

  Vile vile nikaelezwa kwamba shule haina hata BODI YA WAKURUNGENZI, kila kitu kinaamuliwa na mwenye shule akisaidiana na mke wake, hivyo hawana hata mahali pa kulalamikia.

  Binafsi nafikiria kuwahamisha watoto wangu kuanzia mwakani, lakini kabla ya hapo nimeona ni vyema nilete hii kero hapa jamvini huenda mmiliki wa shule hii ni member hapa na anaweza kutupatia majibu. Vinginevyo naomba wadau tuijadili shule hii pamoja na zingine zinazofanana na hii.

  Nawakilsha.
   
 2. M

  Mshika Moja Member

  #2
  Jun 10, 2011
  Joined: Oct 31, 2008
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naafiki, hali si ya kutia moyo sana pale skuli na hasa chakula; swala la ada ni kweli ilipandishwa bila hata kushauriana na wazazi na ni
  kubwa sana lakini hailingani na huduma wapatayo watoto.

  Tena hata mikutano na wadau (wazazi) ni nadra.

  Sitegemei kupeleka mtoto wangu mwingine pale skuli, nina mmoja kwenye mwaka wa mwisho.
   
 3. C

  Cliffie Member

  #3
  Jun 12, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Nashukuru mdau uliyeibua hoja hii. Mimi pia nina mtoto pale yuko darasa la 3. Ni kweli kwamba darasani wako zaidi ya 30 (karibu mara 2 ya idadi hiyo); Chakula anaonesha kukifurahia; etc
  Kwa maoni yangu nafikiri suluhisho si kuhamisha watoto au kutopeleka watoto bali ni kumkabili mwenye shule au uongozi ili uweke utaratibu wa kamati / bodi ya shule ambapo wadau hasa wazazi waweze kuwakilishwa na hivyo kuboresha shule kwa manufaa ya watoto wetu. Changamoto ni jinsi gani ya kukabili uongozi kukubali wazo hilo la ushirikishwaji wa wazazi katika undeshaji shule...
   
 4. K

  Kashaija JF-Expert Member

  #4
  Jun 13, 2011
  Joined: Aug 7, 2008
  Messages: 255
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Tatizo kubwa liko hapo kwa mwenye shule kukubali changamoto ya kuanzisha bodi ya shule, maana anahisi bodi itaanza kuhoji namna ya matumizi ya hela nyingi anayoipata. Pili, wazazi takribani wote wanaonekana kuridhika, hakuna anayepiga kelele. Nadhani labda hawana hata muda wa kufuatilia maendeleo ya watoto wao na hivyo hawajui kinachoendelea pale.
   
 5. L

  Laura Mkaju Senior Member

  #5
  Jun 13, 2011
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 194
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nashukuru wadau kwa taarifa hii, mie ndio nilikuwa katika mchakato wa kumpeleka mwanangua akaanze chekechea. Simpeleki tena kama ndio kuko hivyo??
   
 6. Uliza_Bei

  Uliza_Bei JF-Expert Member

  #6
  Jun 13, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 3,109
  Likes Received: 428
  Trophy Points: 180
  Tafadhali wadau mtakapohamisha watoto wenu pale TUSIIME kwenda kwingineko, kumbukeni kumwambia ukweli huyo mmiliki huenda siku za usoni akakumbuka kujirekebisha atakapoona hana wanafunzi tena. tatizo kubwa la wamiliki wa shule za private ni tamaa za kuongeza wanafunzi---kuongeza pesa---lakini wanasahau kufikiria vitendea kazi na manpower, na shule nyingi za namna hii zimepungua na zimekosa ubora.
   
 7. e

  ebuji Member

  #7
  Jun 14, 2011
  Joined: Feb 28, 2007
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Mimi ni mdau wa muda mrefu wa shule hii, toka miaka ile jamaa alipoanzisha chekechea nyumbani kwake pale Tabata magenegeni akiwa ndiyo anaanza, hadi pale alipoweza kuijenga Tusiime yenyewe bado nina watoto pale, japokuwa yule wa mwanzo alishamaliza akaenda shule nyingine. Tatizo kama mnavyosema kweli ni utawala, huwezi kuwa mkurugenzi, mwalimu mkuu, na wa zamu wewe mwenyewe, utaharibu tu, jamaa kwa kweli alianza vizuri, lakini kwa sasa anaharibu kwa chakula, ada kupanda kila mara. Tatizo: Ni sisi wazazi kukubaliana kila kitu na huyu bwana , tunaweza kupanga mbinu ya kumpunguza speed, na halafu nadhani anayechangia ni yule mama wmenyekiti wa waziai, hajawahi kubalilka kila mwaka toka nijue shule hii miaka ya mwanzo ya 2000 hadi sasa na sijui kama ana watoto pale na anachaguliwaje? inawezekanaje mtu mmoja tu kuwa mwenyekiti miaka yote hii, wengine hawana akili ama vipi ? na kwa nini asi step down wengine wakaongoza kwa awamu specific? yeye ndiye amekuwa akiamua kila kitu on our behalf wazazi na kwa kuwa mikutano ile inatawaliwa kibabe, wengine tume loose interest hata ya kuhudhuria, kwa assumption kwamba as long as I can manage to pay school fees ya wanangu, haijalishi. Hii kwa kweli wadau inakera. Nakushuru mwanzilishi wa topic.
   
Loading...