Shule ya Sekondari ya Wavulana Geita (GESECO) imefungwa kwa muda wa wiki mbili baada ya kuungua mara 3 ndani ya siku 7

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Rosemary Senyamule ameifunga Shule ya Sekondari ya Wavulana Geita (GESECO) kwa muda wa wiki mbili baada ya moto kuwaka katika bweni la wavulana usiku wa kuamkia leo Julai 14, 2021.

Kutokana na uamuzi huo, wanafunzi wote wametakiwa kurudi majumbani, na wanafunzi wanaosoma kidato cha tano watahamishiwa katika shule zingine za sekondari zilizopo katika mkoa huo.

Kufuatia tukio hilo, wanafunzi watatu wanapatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita baada na kupata matatizo ya kiafya, ambapo vifaa vyao yakiwemo magodoro, masanduku na nguo na mali nyingine za shule vimeteketea.

Hii ni mara ya tatu kwa shule hiyo kuungua moto ndani ya kipindi kifupi cha wiki mbili ambapo awali darasa lililokuwa likitumiwa kuhifadhi magodoro na masanduku ya wanafunzi liliungua, kisha ikifuatiwa na kuungua kwa maabara ya kemia na baiolojia na kupelekea kuharibika kwa mali mbalimbali.

Mwananchi
 
wachunguze hao wanafunzi vizuri,
siku hizi kuna wanafunzi watukutu na wavuta bangi na wahuni.
baadhi ya shule siku hizi hazina mkazo na umakini wa kusimamia nidhamu ya wanafunzi.
 
Tiss wapo kazini kuna kitu wanakitengeneza kuwaaminisha watz wengi bado hawajajua ni wachache tu ndio wataweza kuunganisha dots

Mama awe makini sn ikiwezekana aifumue Tiss na diwani apangiwe kazi nyingine
 
Hao waalimu na wanafunzi walienda msibani kweli kipindi kile cha mwendazake?
Au walijifanya wako bize?
 
Baadhi ya wanafunzi huwa bange zinawakolea.
Wakikua wataacha na kujutia elimu waliyoichezea
Uzuri ulimwengu huwa unafunza kiundani zaidi
 
Hyo shule toka miaka ya early 2000 ilikuwa na wanafunz mabangi bangi
 
Tiss wapo kazini kuna kitu wanakitengeneza kuwaaminisha watz wengi bado hawajajua ni wachache tu ndio wataweza kuunganisha dots

Mama awe makini sn ikiwezekana aifumue Tiss na diwani apangiwe kazi nyingine
Inawezekana aisee!
Halafu wako karibu sana na Geseco
 
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Rosemary Senyamule ameifunga Shule ya Sekondari ya Wavulana Geita (GESECO) kwa muda wa wiki mbili baada ya moto kuwaka katika bweni la wavulana usiku wa kuamkia leo Julai 14, 2021.

Kutokana na uamuzi huo, wanafunzi wote wametakiwa kurudi majumbani, na wanafunzi wanaosoma kidato cha tano watahamishiwa katika shule zingine za sekondari zilizopo katika mkoa huo.

Kufuatia tukio hilo, wanafunzi watatu wanapatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita baada na kupata matatizo ya kiafya, ambapo vifaa vyao yakiwemo magodoro, masanduku na nguo na mali nyingine za shule vimeteketea.

Hii ni mara ya tatu kwa shule hiyo kuungua moto ndani ya kipindi kifupi cha wiki mbili ambapo awali darasa lililokuwa likitumiwa kuhifadhi magodoro na masanduku ya wanafunzi liliungua, kisha ikifuatiwa na kuungua kwa maabara ya kemia na baiolojia na kupelekea kuharibika kwa mali mbalimbali.

Mwananchi
Wahusika tunaomba mjithathimini sana kutokana na haya majanga ya moto sahivi kunakazi kubwa ya kufanya maana athari za moto zimegeuka kuwa janga sahvi.
 
Tiss wapo kazini kuna kitu wanakitengeneza kuwaaminisha watz wengi bado hawajajua ni wachache tu ndio wataweza kuunganisha dots

Mama awe makini sn ikiwezekana aifumue Tiss na diwani apangiwe kazi nyingine
Diwani ameshindwaje kutengeneza machawa mashuleni??
 
Back
Top Bottom