Shule ya Sekondari ya Serikali Oldonyo Sambu, watoto wanalipa Tsh 440,000 kwa mwaka

sirluta

JF-Expert Member
Nov 28, 2012
6,194
2,000
Shule ya Sekondari ya Serikali OLDONYO SAMBU yenye usajili namba s0977 iliyopo Wilaya ya Arusha Vijijini (O-level) wanafunzi wake wanatozwa kiasi cha Tsh 440,000 kwa mwaka kwa ajili ya malipo ya mchango wa bweni na chakula. Mabweni yamejengwa ndani ya eneo la shule lakini watoto wanayalipia.

NAOMBA KUFAHAMU KAMA KUNA SHULE ZA SERIKALI ZA O-LEVEL AMBAZO HAZINUFAIKI NA ELIMU BURE.
 
Kibstec

JF-Expert Member
May 21, 2016
1,205
2,000
Mkuu ukiwa una leta habari kama hizi unatakiwa uweke ata vithibitisho KAMA RISITI ya unachokisema ili HABARI IWE NA UZITO WAKE vingnevyo hizi ni chuki tu unazotaka kuzipandikiza.......LAKI NA AROBAINI ARUSHA VIJIJINI?????? WAKATI MWINGNE TUWE SERIOUS
 
Ngushi

JF-Expert Member
Jul 8, 2016
9,085
2,000
Umeuliza hiyo serikali yako ya ccm imetoa shilingi ngapi kwaajili ya chakula?
Ukipata jibu njoo urekebishe uzi wako
 
muhomakilo jr

JF-Expert Member
Jul 28, 2013
11,165
2,000
Shule ya Sekondari ya Serikali OLDONYO SAMBU yenye usajili namba s0977 iliyopo Wilaya ya Arusha Vijijini (O-level) wanafunzi wake wanatozwa kiasi cha Tsh 440,000 kwa mwaka kwa ajili ya malipo ya mchango wa bweni na chakula. Mabweni yamejengwa ndani ya eneo la shule lakini watoto wanayalipia.

NAOMBA KUFAHAMU KAMA KUNA SHULE ZA SERIKALI ZA O-LEVEL AMBAZO HAZINUFAIKI NA ELIMU BURE.
Mabweni yamejengwa eneo la shule,Mali ya shule au mtu mwingine?,inawezekana Kuna mtu amejenga kwa makubaliano na shule wanafumzi walipie kwa muda Fulani mfano miaka 5,baada ya hapo majengo yanakuwa Mali ya shule...lakini Ada shule za bweni za serikali haijafika kiwango hicho.
 
CHARMILTON

JF-Expert Member
May 30, 2015
6,730
2,000
Hapa ndipo wanasiasa wanapopajipatia mwanya wa kudanganya umma.

Wakati Magufuli ana ahidi elimu bure tulitakiwa tumuulize kipi kitakuwa bure na kipi kitakacholipiwa.

Bweni, chakula n.k ni sehemu ya elimu.

Ni vema mijadala iwe lazima kwenye kipindi cha kampeni ili tuweze kuhoji ahadi za wagombea kwa kina zaidi.
 
kiwatengu

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
15,243

Mbona unalalamika sana? Kwani lazima mtoto wako asome hapo?
 
CHARMILTON

JF-Expert Member
May 30, 2015
6,730
2,000
Mbona unalalamika sana? Kwani lazima mtoto wako asome hapo?
Ndo tatizo kubwa la nchi hii, UBINAFSI! yaani kama tatizo halikuhusu unaona hakuna sababu ya kujisumbua nalo.
Tujifunze kuhangaikia majority interests..........BTW Magufuli na serikali yake hana uwezo wa kusomesha watoto wangu.
 
umla

JF-Expert Member
Oct 20, 2012
1,166
1,250
Acha wivu wa kike wewe...kazi yenu umbea tu...kashitaki kwa baba yako sasa!
 
Possibles

JF-Expert Member
Sep 22, 2011
1,523
2,000
Kwa ninavyofahamu;
1. Kuna shule za serikali za kutwa-hizi wanafunzi wanasoma bure(elimu bure).

2. Kuna shule za serikali za bweni mf. Mzumbe, Ilboru, Minaki, Pugu,Ruvu girls n.k hizi wanafunzi hulipia 75,000/- kama sikosei kwa ajili ya kuchangia chakula. Serikali pia hutoa ruzuku ya chakula kwa shule hizi.

3. Kuna shule za serikali zenye hosteli-hizi wanafunzi hujilipia wenyewe chakula yaani serikali haipeleki huko ruzuku ya chakula. Shule hizi wazazi hupangiwa kiasi cha kuchangia ili watoto wao waweze kula shuleni.
 
labda hii shule ipo katika hiyo aina ya 3 ila mbona kiwango ni kikubwa sana? Vigezo gani hutumika kupanga haya maana shule ipo vijijini halafu watoto wanalipa hela zote utadhani private?
 
Possibles

JF-Expert Member
Sep 22, 2011
1,523
2,000
labda hii shule ipo katika hiyo aina ya 3 ila mbona kiwango ni kikubwa sana? Vigezo gani hutumika kupanga haya maana shule ipo vijijini halafu watoto wanalipa hela zote utadhani private?
Ni kweli yaonekana ni kubwa. Hata mimi sijui hesabu zake vizuri. Labda inaonekana kubwa kwa kuwa tunailinganisha na ile elfu 70 wanayolipa walioko shule za bweni.

Pia nijuavyo hii ni pesa ya kula na malazi kwa mwanafunzi kwa milo miwili + uji wa asubuhi + chai kwa siku zisizopungua 197 ambazo mwanafunzi anapaswa kuwepo shuleni kwa mwaka.

Nadhani kuna umuhimu wa serikali kuzipatia ruzuku hizi shule ili kuwapunguzia makali wananchi.
 
Kkimondoa

JF-Expert Member
May 31, 2014
4,464
2,000
Shule ya Sekondari ya Serikali OLDONYO SAMBU yenye usajili namba s0977 iliyopo Wilaya ya Arusha Vijijini (O-level) wanafunzi wake wanatozwa kiasi cha Tsh 440,000 kwa mwaka kwa ajili ya malipo ya mchango wa bweni na chakula. Mabweni yamejengwa ndani ya eneo la shule lakini watoto wanayalipia.

NAOMBA KUFAHAMU KAMA KUNA SHULE ZA SERIKALI ZA O-LEVEL AMBAZO HAZINUFAIKI NA ELIMU BURE.
Isije ikawa Taarifa kutoka mtu wa tatu.
 
suranne

Senior Member
Aug 12, 2010
120
250
Jamani hiyo pesa ukiiangalia kwa macho ya kwaida ni kubwa sana ila kimatumizi kwa mwanafunzi wa bweni ambaye serikali haichangii ni ndogo sana!!! Chukulia uji asub, chakula mchana na jioni na bado malazi afu kokotoa ndo ujue kiasi gani wanapunjwa au wanapunja shule
!!!
 
mwanaapolo

JF-Expert Member
Mar 14, 2014
256
195
Nimesoma Oldonyo Sambu Seminary/ Arusha Seminary/Immaculate Heart of Mary Seminary , naifahamu vizuri tu hiyo Sekondary ya Oldonyo Sambu almaarufu Mavumbini. kwa kipindi nilipokuwa shule 'Donyo" Hapakuwa na hospitali, umeme. maji yalikuwa yana upungufu wa madini yakawa yanapindisha mifupa ya viungo vya watoto waliozaliwa pale. Nadhani kipindi kile hali ya hiyo sekondari ilikuwa mbaya sana.

Tatizo la huduma mbovu za kijamii Oldonyo Sambu ni kutokana na udogo wa utashi wa kisiasa. Mfano ni hiyo wanafunzi kulipia mabweni, lipo miaka nenda; rudi ila hakuna mtu anayethubutu kulisema kwa mamlaka husika.
Sijajua kama hospitali, umeme na maji vimefika mpaka sasa, hao wanafunzi kupata sifuri, sio mapenzi yao ni mazingira sio rafiki kwani eneo hilo hilo, ipo Seminary inayofanya vizuri sana Mkoa na taifa.

Ora et Labora, Deus adest son has! Ora! Ora! Ora! et Labora!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom