SHULE YA SEKONDARI YA KATA YA TURA (TABORA yapotez dira. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

SHULE YA SEKONDARI YA KATA YA TURA (TABORA yapotez dira.

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by MCH, Jul 22, 2012.

 1. MCH

  MCH Member

  #1
  Jul 22, 2012
  Joined: Jul 21, 2012
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwakutokana na uhaba wa waalimu katika shule nyingi za kata hapa nchini sasa tura sekondari yakaribia kupotea katika ulimwengu wa shule za sekondari kwa kukosekana kwa waalimu wa kuiwezesha shule hiyo sasa shule hiyo ina waalimu wawili tu.je kwa elimu hii tutafika?
   
 2. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #2
  Jul 22, 2012
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Mbona afadhali hiyo mkuu, kuna shule nyingi zina mwalimu mmoja, naye ni mlezi tu tena wa shule ya msingi. wanaofundisha pale ni form six leavers ambao hata uvoda fasta hawakupitia. Taratibu tutarekebisha labda huko mbeleni, mhimu ni nyinyi wananchi ni kutengeneza mazingira mazuri ya kupata walimu. Jitoleeni kuwajengea walimu nyumba, somesheni watoto wenu ili baadae waje wafundishe hapo. Vinginevyo, matatizo kama hayo hayataisha.
   
 3. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #3
  Jul 22, 2012
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Sielewi kwa nini serikali za vijiji au kata hazina mipango madhubuti za kutatua tatizo kama hilo!! Nilitegemea wakati zinaanzishwa hizi shule, serikali za kata zingekuwa zimeshajipanga kuhakikisha zinatoa ufadhili kwa wanafunzi wanaotoka maeneo yao kwenda hata private schools, au kwenda kufanya hata uchuuzi kwenye vyuo vya walimu kwa kuwavutia!!
  Elimu ni kama uwekezaji siku hizi kutokana na tatizo kubwa la walimu, inabidi kuwavutia walimu!! hata hawa wanaohitaji fields au mazoezi basi kungekuwa na nyumba nzuri za wao kuweza kukaa bila malipo, wangekuwa wanapunguza tatizo.
  Yote hayo yanahitaji viongozi wenye vision, wenye kujitolea siyo kuvizia watu wanaotaka kupiga watu faini ili wajenge nyumba zao.Wewe kwa vile umeweza kufika hapa jamvini, fanya kitu cha maana!! don't just sit there and do nothing, its for your ward, village and your neighbours!!
  Itisha mkutano waeleze A - Z, nini kinatakiwa kufanya ili kuokoa watoto wenu katika kata ile.Naimani utafanikiwa na utakuwa shujaa wa hiyo kata, wilaya, mkoa pamoja na taifa. Kamwe usikatishwe tamaa na vikwazo utakavyokumbana navyo!! Undeni hata kamati ndogo huru ya watu wenye moyo safi kushughulikia hiyo inshu.
  Unaweza hata kumwalika mkuu wa mkoa ukiona mambo yanaenda vizuri/vibaya hata waziri wa elimu. Kifupi mustakabli wa shule hiyo uko mikononi mwako kwani unaonekana una uchungu na hiyo shule. Kila la kheri.
   
 4. MCH

  MCH Member

  #4
  Apr 1, 2013
  Joined: Jul 21, 2012
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sasa ebu angalia matokeo ya kidato cha pili ni mabaya mno pia kidato cha 4 ndo usiseme yaani shule haina 1,2,wala 3 yaan kuna 4 tena kuanzia 30 nao ni wanafunzi 7 tu walio baki ni 0.jumla walikua wanafunzi 13 tu.je shule hii itafika kweli?
   
Loading...