Shule ya sekondari St Amedeus kuna shida

MUGHOMBA

Senior Member
Oct 12, 2013
114
57
Ni habari ya kusikitisha ambayo nimekutana nayo, kuna mzazi nimekutana naye akiwa katika hali ya majozi na huzuni sana kuhusu shule ya St Amedeus kitu ambacho kimenifanya nijifunze kitu kikubwa kuhusu hizi shule za mission.

Mzazi alinieleza mwanae alijiunga na shule hiyo miaka mitatu iliyopita akiwa na uwezo mzuri ila baadaye hasa ilipofikia mwishoni mwa kidato cha kwanza maendeleo ya mtoto hayakuwa mazuri kulingana na wastani husika wa shule.

Hivyo wazazi wenye watoto wenye ufaulu huo dhaifu waliitwa shule wakiambiwa watoto wenu wana ufaulu ambao hauwaruhusu kuwa hapa, mzazi anasema waliomba wafanye kikao na walimu ili kupanga mikakati ya nini kifanyike ili kuinua ufaulu wa wanafunzi hao ila hawakupewa nafasi hiyo wakaambiwa chukueni hizo fomu msome mjaze kama mnakubaliana na yaliyomo na kama hamkubaliani chukueni watoto wenu, fomu hiyo ilimtaka mzazi kukubali kama mwanae hatafikia wastani husika wakati wa kufanya registration za kidato cha pili mtoto atatafutiwa shule nyingine ya kufanyia mtihani ila si pale,

Kwa hali iliyokuwepo ilikuwa ni ngumu kwa wazazi kukataa kusaini fomu hizo, hivyo walisaini. wakati wa kufanya usajili ulipofika watoto wote waliokuwa na uelewa mdogo walipelekwa shule ya sekondari iitwayo Lombeta kwenda kufanyia mitihani huko shule ikabaki na cream na kweli wote waliobaki pale walipata alama za juu na shule kuonekana kweli walimu wanafundisha kumbe wamechuja makapi,
baada ya matokeo ya kidato cha pili hao watoto wote waliokwenda huko Lombeta walifaulu. kutokana na maelezo ya mzazi si kwamba walihamishiwa Lombeta ila walipelekwa tu kufanya mtihani na kurudi shuleni st Amedeus, hivyo waliendelea na masomo yao hapo st Amedeus.

kama kawaida wakiwa kidato cha tatu na inavyoonekana kulingana na maelezo ya mzazi hawakuwa wanawafuatilia watoto hao tena ina maana ilibaki ni juhudi binafsi ya mtoto na hii ni kwa vile walikuwa wakipanga mikakati mingine ya kuijenga shule yao, mwanzoni mwa mwaka huu anasema waliitwa tena shuleni wakielekezwa kuwa watoto wenu hawajafanikiwa kufikisha wastani husika wa shule katika matokeo ya kumaliza kidato cha tatu hivyo kila mzazi achukue mtoto wake aondoke shule hiyo haina nafasi kwa watoto hao wenye uelewa mdogo, anasema mkutano ulikuwa mgumu kwani kama shule walishafanya maamuzi, tena sasa idadi si ile iliyokwenda Lombeta waliongezeka na wengine,

Baadhi ya wazazi walihoji ni kwanini msipange mikakati ya kuwasaidia hawa watoto kwani walikuwa wanafunzi wazuri walipofika shule hii, shule na wazazi tujadili nini cha kuwasaidia watoto, wazazi walilalamika wakihoji ni wapi shule itapatikana kuwachukua watoto wa kidato cha nne mbona ni jambo gumu. kumbe huo wote ulikuwa ni mtego wa kuwatega wazazi tayari shule ilishaandaa fomu za wazazi kusaini kwamba itakapofika wakati wa usajili kama mwanao hatafikisha wastani unaohitajika na shule atatafutiwa shule nyingine ya kufanyia mtihani na si hapa st. Amedeus tena, cha kushangaza huyu mzazi anasema wazazi walikubaliana wasaini ili watoto waendelee na masomo wasinyanyasike na hapa walikuwa na matumaini kwamba huenda wanafunzi wakafikisha alama zinazohitajika,

Hivyo aliendelea kueleza kwa uchungu mkubwa kwamba mwezi huu walikwenda shuleni hapo kuwatembelea wanafunzi ambapo wazazi walipigwa na butwaa baada ya wanafunzi kuwaeleza kuwa wamefanyiwa usajili shule ipo huko Rombo na wala si ile waliyofanyia hata huo mtihani wa kidato cha pili, tetesi ni kwamba kule Lombeta walisema kila abiria achunge mzigo wake. mzazi amekata tamaa na kweli inaumiza sana mzazi unalipa ada shule A mtoto anapelekwa kufanyia mtihani shule B.
Nilimuuliza huyu mzazi huko Rombo wanapelekwa kufanya mtihani kama Private candidate au wanakwendaje? kweli hii hainiiingii akilini na ndipo nilipojifunza kwamba matokeo ya hizi shule za mission tunayoyaona na kuona wanaongoza si sahihi tayari wameshachuja ili shule ziwe na majina kwamba zinafaulisha,

Wwito wangu mwenye uwezo wa kusaidia hili awaarifu wizara ya Elimu ili watoto hawa wapate haki yao ya msingi, kwani kisaikolojia hii hali inaumiza sana wanafunzi, saidieni watoto hawa wasio na hatia, kazi ya shule ni kumsaidia mwanafunzi ili aweze kufanya vizuri si kupokea ada za wazazi na kufanya mambo yasiyoeleweka, heri wangewakataa toka kidato cha kwanza, mama huyu aliwaomba shule wamwandikie mwanae barua ili arudie darasa wakakataa,

MWENYE MSAADA ILI WANAFUNZI HAWA WAPATE HAKI YAO.
 
Hapo rahisi sana.

Hao wazazi waende kwa afisa elimu wa wilaya au mkoa wakiwa na uthibitisho wakawatumbue hiyo shule.

Hiyo ni sekondary ya kawaida tu kama nyingine.
 
ndo mana me siwez kuwasifia walimu wa hzo shule kuwa wanajua kufundisha ndo mana watoto wanafaulu,sikatai kuwa wana effort academically lakini wapo too selective kwa watoto kusoma shule hzo,mwalimu amesomea kumfundisha mtoto wa aina yoyote fast learner na slow learner.so wazazi wasidhani kuwa mtoto wa aina yoyote anaweza kusoma shule hzo.
 
Back
Top Bottom