Shule ya sekondari Central Dodoma yafungiwa!

Malolella

JF-Expert Member
Feb 3, 2012
366
111
Shule hii kongwe ipo Dodoma mjini imefungiwa rasmi baada ya kutotimiza vigezo. Akitoa ufafanuzi khsu uamuzi huo naibu waziri wa elimu bw Philipo Mulugo amesema shule haikidhi vigezo kwani inawalimu wawili2 na uongozi wa shule hiyo haueleweki.

Mkuu wa shule ndio manager, ndio mkurugenzi, ndio mwl wa taaluma, ndio mwl wa nidhamu, ndio mwl wa zamu,ndio mhasibu, na ndio mwl wa darasa. Ukipita shuleni hapo na kujitambulisha kuwa ww ni mwl unapewa kipindi ukimaliza unalipwa na mkataba umeisha.

Sababu hizo zimefanya naibu waziri kuifunga shule hiyo kwa muda usiojulikana.
 
ndiyo serikali yetu inavyopenda watoto si wataenda kusoma kwenye shule za vigogo, walalahoi mtajiju.
 
Acha uzushi si ya BAKWATA ni ya MBABAISHAJI MMOJA HIVI tena MKULIMA WA ZABIBU

Labda huyo "mkulima wa zabibu" awe ameinunua hivi karibuni. Kama mjumbe mmoja alivyosema mwanzoni hiyo shule ilikuwa chini ya Agha Khan (japo yeye hakusema Agha Khan ila wahindi) zamani kabla ya shule za binafsi kutaifishwa. Ila kabla ya utaifishwaji huo Agha Khan walishawapa BAKWATA.

Nina uhakika kuwa at least hadi katikati ya miaka ya 2000 hiyo shule ilikuwa chini ya BAKWATA, najua hivyo kwa kuwa nilishawahi kufundisha Mazengo Sekondari na nilikuwa na vipindi Central pia.
 
Waende na kwenye shule ya mbunge wa dodoma mjini inaitwa city sec nadhani nayo haina walimu maana ina div zero zaidi ya 170 huku ikiwa haina div 1 na div 2 zikiwa sita tu, div 3 ziko kumi na mbili
 
Waende na kwenye shule ya mbunge wa dodoma mjini inaitwa city sec nadhani nayo haina walimu maana ina div zero zaidi ya 170 huku ikiwa haina div 1 na div 2 zikiwa sita tu, div 3 ziko kumi na mbili

Wameionesha tbc wakipiga kampeni wanafunzi waliokuwa wakisoma central waende City aka shule ya mbunge wa Dodoma mjini.
 
Back
Top Bottom