Shule ya Rashid Kawawa Liwale

Mzee wa Gumzo

Senior Member
Apr 21, 2008
197
5
Wana mtandao poleni kwa majukumu mengi ya ujenzi wa taifa letu.

Nimepotea kwa muda mrefu katika jukwaa kutokana na majukumu ya kazi mikoani.Nipo mtwara na nimetokea Lindi ambapo nimeshuhidia jambo lililoniacha na maswali mengi.

Ni jambo la kweli na ushahidi upo.

Kuna shule moja ya sekondari ya kata wilaya ya liwale tena mjini yu inaitwa Rashidi Mfaume kawawa Sekondary school.Ni moja kaati ya shule zilizoanzishwa wakati wa programu ya MMEM.shule hii ina jumla ya wanafunzi mia tano na thelathini (530) kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha nne.

Ina vyumba vitano vya madarasa,meza ndogo za kuandikia wanafunzi mia mbili na viti vya kukalia viivyozidi mia mbili.Viti na meza hizi ni vidogo hivyo haviwezi kukaliwa na mwanafunzi zaidi ya mmoja.
Kwa matiki hiyo nilishuhudia kuwa vidato vya tatu na nne wote wanakalia viti na kutumia meza na wanafunzi wachache wa vidato vya pili na kwanza.Nusu ya wanafunzi wanakaa chini.

Wastani wa wanafunzi kwenye darasa moja ni mia moja na kumi na tano ingawa kuna daraa lina wanafunzi mia na thelathini.

Katika wingi huu wa wanafunzi wanaofika mia moja kidato cha nne ambao wapo mia na thelathini wanatumia kopi mbili tu za kitabu cha Is it Possible ambazo ndizo zinazopatikana shuleni.Vitabu vingine ni tabu,hamna.

Waalimu kwa muda mrefu wamekuwa wakitumia mkorosho kama ofisi kwa kujibanza chini yake.

Baada ya kuzungumza na watu fulani pale shuleni kujua jitihada za serikali na wananchi kutatua hali ile nilijibiwa kuwa wananchi wamekuwa na mwamko mdogo sana kuchangia maendeleo ikiwemo elimu mahali hapo.Jmambo la pili ni kuwa serikali ya mahali pale (wilaya na halmashauri ) wamekuwa sehemu ya matatizo kwa kuendesha mambo kisiasa.Mfano hai niliopewa ni kuwa mkuu wa kisiasa wa eneo hilo aliwahi kuwatishia waalimu wa hapo kuwa endapo watatangaza kwenye vyombo vya habari kuwa shule yao ina matatizo na inahitaji kusaidiwa hatasita kuwawajibisha kwa kuwatimua au kuwahamishia maporini.Amekuwa akilalama mwana mama huyo ambaye aliwahi kuwa kigogo wa chama tawala katika wilaya moja huku kusini kuwa hayupo tayari kuona kibarua chake kikiota majani kwa kuchongewa kwa rais kupitia vyombo vya habari.

Kuna mwandishi mmoja wa habari alikwenda kufanya uchunguzi akakutana na mkwara wa mama huyo mwanasiasa machachari.

Pamoja na hayo yote wakuu wa shule na viongozi wengine wa karibu kama diwani walifanya jitihada za makusudi kimyakimya kumwona mzee kawawa Dar es Salaam na kumlilia shida.Kwa kutambua kuwa shule imebeba jina lake ,'simba wa yuda' hakuwaangusha, akawapigia pande TBLambako wamepata milioni kumi na tano.Wameamua kumalizia ujenzi wa nyumba ya mwalimu na wanaitumia kama ofisi kwa muda.

Binafsi nawapongeza sana waalimu, diwani na mzee kawawa na TBL.

Hoja yangu ya msingi jamani ni kuhusu aina ya viongozi tulionao katika wilaya na halmashauri zetu.Hivi ni haki tuendelee kuwaonea haya viongozi wanaoiweka rehani elimu na mustakabai wa maisha ya watoto na wadogo zetu kwa kutaka kulinda himaya zao binafsi?.Hebu tulitizame hili na kuziangalia shule nyingine nyingi kama hizi kila kona ya nchi.Hatuhitaji kuwa na viongozi wanaowatisha wale wanaotaka kuanika uovu wao.
 
Kuna sehemu zimesahauliwa na serikali, na Liwale ni mojawapo. Elimu ya kuwa na watoto 115 katika darasa moja, na watoto kukaa chini sio Elimu. Ni mzaha tu!

Wananchi kama hawa wanatakiwa kuwaasi viongozi wao. Wanaogopa nini? They have nothing to loose. Wamfukuze huyo Mama anayewakalia! Apigwe marufuku kuonekana Wilayani humo.

Mashirika ya Kidini yanaweza kuwa msaada mkubwa katika kuleta Elimu sehemu ambazo zimesahauliwa na serikali. Wananchi husika wawaalike Masista waje kuwasaidia kielimu. Hata kama ni Waislamu wasijali. Bila Elimu hawatakaa waendelee.
 
Mfano hai niliopewa ni kuwa mkuu wa kisiasa wa eneo hilo aliwahi kuwatishia waalimu wa hapo kuwa endapo watatangaza kwenye vyombo vya habari kuwa shule yao ina matatizo na inahitaji kusaidiwa hatasita kuwawajibisha kwa kuwatimua au kuwahamishia maporini.

Amekuwa akilalama mwana mama huyo ambaye aliwahi kuwa kigogo wa chama tawala katika wilaya moja huku kusini kuwa hayupo tayari kuona kibarua chake kikiota majani kwa kuchongewa kwa rais kupitia vyombo vya habari.

Hoja yangu ya msingi jamani ni kuhusu aina ya viongozi tulionao katika wilaya na halmashauri zetu.Hivi ni haki tuendelee kuwaonea haya viongozi wanaoiweka rehani elimu na mustakabai wa maisha ya watoto na wadogo zetu kwa kutaka kulinda himaya zao binafsi?.Hebu tulitizame hili na kuziangalia shule nyingine nyingi kama hizi kila kona ya nchi.Hatuhitaji kuwa na viongozi wanaowatisha wale wanaotaka kuanika uovu wao.

Hapo ni baado tu unawaonea haya kwa kushindwa kuweka jina lake bayana
 
Nashangaa kwa nini wanafunzi wakose madawati ili hali Liwale kuna msitu mkubwa wa kuvuna mbao,viongozi wa halmashauri wako wapi??
 
Kocha,

Kutoka msitu wa miti hadi madawati kuna kamwendo! Mbona Tanzania kuna dhahabu nyingi lakini wananchi hawana fedha?

Tatizo la msingi ni uongozi mbovu na kusahauliwa na serikali. Wakishapigiwa kura viongozi wanaishia, wanasubiri uchaguzi mwingine. Kwa vile wananchi hawana elimu, inakuwa rahisi kuwarubuni na kuchaguliwa tena.

Wananchi wachache wa Liwale amabao wamefunguka macho na wako Dar waunde Kamati ya Maendeleo ya Liwale. Hiyo kamati ijue wazi kwamba maendeleo = elimu. Wafanye mazungumzo na wadau mbali mbali wa elimu, ikiwa ni pamoja na serikali na makundi ya kidini.

Mimi nawashukuru sana Masista waliojenga shule ya sekondari kwetu Bagamoyo (nimehamia huko). Masista hao hao mkiwaomba wanaweza kuja Liwale wakafanya kweli pale. Kwa sasa mnacheza tu.
 
Kwa ujumla huku kusini kazi ipo ndugu zangu,kuna watu huku kila kitu ni siasa.Hata hivyo huyu mzee jina lake litatumika ktk shule ngapi? Shule ya sekondari pale Mafinga JKT inaitwa kwa jina lake.
 
Back
Top Bottom