Shule ya Msingi Malungu wilayani Nyasa ina wanafunzi zaidi ya 440 waalimu 3

Phd Hewa

JF-Expert Member
Oct 3, 2016
572
466
Kama kichwa cha habari kinavyosema Shule ya msingi Malungu wilayani Nyasa Mkoani Ruvuma Songea Tanzania inakabiliwa na changa moto ya waalimu,

Ina wanafunzi 445 lakini waalimu wanaofundisha kwenye Shule hiyo ni watatu 3 tu tena wawili ni mke na mume wake,

Nilibahatika kufanya mazungumzo na mwalimu mmoja wapo anaefundisha shuleni hapo jina nalihifadhi kwa usalama wa Kazi yake nilipomuuliza kwa nini wanafunzi ni wengi halafu waalimu ni wachache?

Alinijibu kama ifuatavyo'ndugu tatizo hapa ni viongozi huko juu tumepeleka malalamiko hadi tumechoka sasa hivi tunaangalia macho tu mpaka wenyewe watakapo tuhurumia lakini kiukweli changa moto ni nyingi hasa kwenye upande wa kufundisha.

Unakuta mfano nanukuu Mimi ni mwalimu ambaye namudu kufundisha kiswahili lakini kingereza siwezi nafanyaje? hapo ndiyo inabidi nijilazimishe tu kufundisha mana kama sivyo watoto itakua hawasomi,

Zaidi akanieleza changa moto nyingine madarasa yote inabidi tupite lakini inashindikana muda mwingine inapita mpaka siku tatu mtoto yawezekana akasoma masomo mawili au matatu kwa week,

Changa moto ni nyingi siwezi elezea zote ila ombi kwa serikali wasaidieni waalimu wakutosha kama siyo hivyo huku vijijini elimu ya watoto wetu inashuka

Nasisi tunataka waje kuwa viongozi wa baadaye na wawe na maisha bora kama nyinyi.
 
walimu tupo mitaani,,shule hazina walimu,,
Inauma sana,,kama ipo shule ya namna ile mkoa wa mwanza nipo tayari kujitolea,,,ni chemistry ,biology &ict,,kwa o'level na advanced level,,
pia shule za msingi,,,
0652886184
 
walimu tupo mitaani,,shule hazina walimu,,
Inauma sana,,kama ipo shule ya namna ile mkoa wa mwanza nipo tayari kujitolea,,,ni chemistry ,biology &ict,,kwa o'level na advanced level,,
pia shule za msingi,,,
0652886184
hongera sana kwa moyo huu mzuri na wa kizalendo wa kujitolea. utasikika
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom