Shule ya J.M. Kikwete yashusha hadhi ya jila la Rais wetu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shule ya J.M. Kikwete yashusha hadhi ya jila la Rais wetu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Andindile, Feb 9, 2010.

 1. Andindile

  Andindile JF-Expert Member

  #1
  Feb 9, 2010
  Joined: Mar 18, 2009
  Messages: 305
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Jina la Rais wa Jamhuri wa muungano wa Tanzania Dr., mheshimiwa rais Jakaya Mrisho Kikwete limeshushwa hadhi na matokeo ya kidato cha nne ya shule ya Sekondari ya J.M. Kikwete iliyopo wilayani Mbozi nje kidogo ya mji mdogo wa Tunduma . Shule hiyo ambayo imepewa heshima ya pekee ya kutumia jina la Kikwete imefanya vibaya kwenye matokeo ya kidato cha nne yaliyotangazwa hivi karibuni hata kufanya jina la J.M. Kikwete likose heshima inayostahili. Nimeambatanisha matokeo ya shule husika. Kwa nini jambo kama hili liruhusiwe kutokea? Hivi rais anataarifa kuwa kuna shule inatumia jina lake? Kama taarifa anazo, amefanya jitihada gani kuhakikisha kuwa wanafunzi na walimu wa shule hiyo wanalitangaza jina lake vizuri kwa kufanya vyema kwenye matokeo ya kitaifa?
   

  Attached Files:

 2. saitama_kein

  saitama_kein JF-Expert Member

  #2
  Feb 9, 2010
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 982
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Mkuu hizo ndo shule za tigo fasta (kata)....bora limemvumbulikia mwenyewe!
   
 3. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #3
  Feb 9, 2010
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,158
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  ........daah yaani mbali na kufeli kote huko, yet hii shule bado siyo ya mwisho? hizo za huko mwishoni, watoto wote wamepata sifuri nini?
   
 4. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #4
  Feb 9, 2010
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,765
  Likes Received: 1,028
  Trophy Points: 280
  Hii shule haijashusha hadhi yoyote kama mwandishi anavyotaka kutueleza inaonyesha jinsi ambavyo uwezo wa mweneyekiti wa Chama Cha Majambazi ulipofikia, Zero. Si mnaona jinsi anavyoendesha shughuli za urais ni sawa kabisa na matokeo hayo.
   
 5. Mkaa Mweupe

  Mkaa Mweupe JF-Expert Member

  #5
  Feb 9, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 655
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Hawa viongozi wetu wa sasa wananishangaza sana, wanataka kila mahali waache majina. Wawe wanaangalia wenzetu huko nje nishule chache sana zinapewa majina ya watu. Labda kama alijenga kwa nguvu zake, lakini si kwa kodi ya walala hoi afu unajipachika jina lako.

  Shame on them!
   
 6. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #6
  Feb 9, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,534
  Likes Received: 1,542
  Trophy Points: 280
  kwani toka lini JK ana hadhi unayoizungumzia wewe?
   
 7. akashube

  akashube JF-Expert Member

  #7
  Feb 9, 2010
  Joined: Dec 24, 2009
  Messages: 411
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Nani kamponza mwenziwe Shule au Jina la shule? Unaamini juu ya bahati na nuksi, kama huamini mpe mtoto wako jina la Kazi bure au Hayawani halafu uone.

  Chunguza maana ya majina ya shule zinazoongoza kwa kufaulu. Halafu angalia shule zinazofelisha.

  Hebu angalieni ka-centre kanajiita London Secondary School, yaani ni Zero mpaka waalimu na wao mtihani huu wana zero. Zero tu. ZEEEEEROOOOOOOO!!!!!!!!!
   
 8. L

  Lubaluka JF-Expert Member

  #8
  Feb 9, 2010
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 496
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hivi ni nani alie ipa Jina hilo la kiongozi wa juu wa nchi hii !!! Ndio yale yale jasho la walala litumike, then yeye aje na Msafara wa mashangingi unaotuma gharama za haohao walala hoi aje kuifungua shule na kukubali shule ibatizwe jina lake. Hapo alipo wala hajui kinachoendele mweeee !!!! na ajue ili nini wakati hata senti ajachangia !!!!
   
 9. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #9
  Feb 9, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,468
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Hahahahaah! Aisee umenichekesha sana!
   
 10. D

  Domisianus Senior Member

  #10
  Feb 9, 2010
  Joined: Aug 1, 2008
  Messages: 154
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Haina maana kabisa, hiyo shule ibadilishwe jina, vinginevyo ni kudhalilishana tena kwa kiwango cha juu sana.Sijafurahishwa kabisa na hayo matokeo hata kidogo.
   
 11. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #11
  Feb 9, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 12,076
  Likes Received: 4,450
  Trophy Points: 280
  jibu lako hili hapa chini


  Kigogo; You made my day!
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...