Shule ya awali na msingi inayomilikiwa na Taasisi ya Kiislam ya Istiqaama iliyopo mkoani Tabora yaungua moto

Unawajua istiqaama au unawasikia!!.. hizi ni hujuma
Ni kina nani hao? kwenye lugha adhimu ya kiswahili hatuna matumizi ya herufi Q.

Na unaweza kuthibitisha kuwa hizi ni hujuma? na zinafanyika ili iweje? Ni kipi ambacho ni cha maana kipo kwenye hizo shule?

Ni maswali ya kawaida ila yanaweza kutusaidia kupata majawabu
 
Huu ni mwendelezo wenye kutia mashaka sana.
Yaani kuanzia mwezi April mpaka September kuna zaidi ya shule tano za kiislamu zimeteketea kwa moto. Binafsi ninaamini haya sio matukio ya bahati mbaya (Accident) huenda ni matukio ya kupangwa!
Unavyohisi nani kayapanga?

Embu waza tu.
1. Ni matukio ya mfululizo.
Ni jambo la kawaida kabisa kwa sababu yanatokea maeneo tofauti tofauti.

Shule ya Kikristo ya Mwanza ilivyoungua mwaka huu ulipata taarifa zake?

2. Ni shule za kiislamu tu.
Wataka za Kikristo na Serikali nazo ziungue ili uwepo usawa?

3. Hakuna uchunguzi wowote wa kina.
Una hakika mkuu?

4. Hakuna ripoti yoyote kuhusu chanzo.
Sasa ripoti itatoka wapi na umeshaandika hakuna uchunguzi wa kina?

5. Hakuna wahusika waliochukuliwa hatua.
Watatoka wapi kiongozi na uchunguzi umeandika haupo?

Acha masikhara bwana
 
Moto naujua vizuri sana hapa Kuna hadi nyumba za nyasi zina umeme hatusikii hayo mambo...
Sasa huku umeingia kwenye field yangu usitake nikuingize darasani tafadhali jikite tu kwenye kuhisihisi chanzo cha hiyo mioto.
 
Unaleta udini usimezwe kiasi hicho kwahyo na hizo shule mbili za kikristo zilizoungua nazenyewe Chanzo chake utasema ni nini
Sileti udini, kinachonishangaza ni ujinga wa hali ya juu ambao watu wengi wako nao.

Mtu na madevu yake mwingine na maziwa yake kilo tatu anashupaza kichwa kabisa akiuliza swali "Kwanini za kiislamu tu?" WTF ulitaka na za Kikristo ziungue ama za Serikali? kwanini usiulize kwanini hili tatizo la moto limekuwa likijitokeza mara kwa mara?

Yani unprofessional and foolish questions ndio zimejaa kwenye mada za hivi litanzania sijui alililaani nani 😡😡
 
Sasa huku umeingia kwenye field yangu usitake nikuingize darasani tafadhali jikite tu kwenye kuhisihisi chanzo cha hiyo mioto.
Sema unikumbushe Mkuu Ila nimefanya kazi ya Moto kwa miaka mingi na maeneo tofauti nimeizunguka dunia kwa sababu ya Moto...
 
Nina mashaka pamoja na mapungufu katika ujenzi, yanayoweza kuleta, hitilafu za umeme n.k.
Nahisi huku nikifikiria nyuma ya keyboard, huenda kuna ubadhirifu mkubwa wa ujenzi, na wahusika, wameamua kuchomoa betri kupoteza ushahidi, au ni mbinu njama, ya kutafuta misaada at the expense of innocent childrens' lives..

Something is fishy! Too fishy!

Everyday is Saturday............................. :cool:
Kwa kuwa ni fikira sawa, hebu fikiria ikiwa ni issue ya mapungufu katika ujenzi ni kwa nini haya matukio yatokee shule za kiislamu tu? Tulianza Dar, Kagere na leo Tabora. Mimi nadhani kuna jambo liko nyuma haya matukio na linaweza kuwa katika namna mbili, Moja kuna watu wajaribu kuhujumu hizi shule kwa malengo yao binafsi. Au taasisi yenyewe kwa kushirikiana na vikundu mbalimbali kuwamua kufanya hivi ili kupata huruma ya watu fulani na hatimaye kuungwa mkono ikionekana wanaonewa. Ni mtazamo tu pia
 
Isije ikawa kuna Boko Haram ya Bongo isiyoamini mfumo wa kupata Elimu Dunia kwa watoto wa Kiislam! Ni vyema mamlaka husika zikaacha kufanya kazi kwa mazoea.

Waingie kazini kufanya uchunguzi wa kina na matokeo ya huo uchunguzi yawekwe hadharani ili Wananchi wote tujue chanzo cha hayo yote. Kuendelea kushuhudia vifo vya watoto wetu na uharibifu mkubwa wa mali, ni jambo lisilo vumilika hata kidogo.
Wazi lako limenifikirisha sana. Na kama kweli ni hao jamaa, basi kazi ipo kuweza kuwabaini kwani wamejizatiti haswa.
 
Binafsi naamini ni hila za mabeberu na si kwa shule za kiislam tu wanaweza pia kufanya hivyo mahospitalini makanisani au popote

Mfano huko uarabuni wanalipua misikiti

Ila naamin serikali yetu sikivu ipo kazini
Wasiwasi wangu ni kwamba tukianza kusingizia mabeberu hatutaweza kutatua tatizo linalotusibu. Neno mabeberu linatumiwa sasa katika kipindi hiki na aghalabu katika masuala ya kisiasa. Mkishindana kisiasa kila mmoja anaishia kumuita mwenzake kwamba ni beberu. Hebu tujiulize kwanza, hivi beberu, kuacha yule mbuzi dume, ni nani hasa?
 
Isije ikawa kuna Boko Haram ya Bongo isiyoamini mfumo wa kupata Elimu Dunia kwa watoto wa Kiislam! Ni vyema mamlaka husika zikaacha kufanya kazi kwa mazoea.

Waingie kazini kufanya uchunguzi wa kina na matokeo ya huo uchunguzi yawekwe hadharani ili Wananchi wote tujue chanzo cha hayo yote. Kuendelea kushuhudia vifo vya watoto wetu na uharibifu mkubwa wa mali, ni jambo lisilo vumilika hata kidogo.
Wanakuambia Boko Haram Ni Kikundi Cha Marekani kilichoundwa kwa ajili ya kupora mafuta Nigeria
 
Back
Top Bottom