Shule ya awali na msingi inayomilikiwa na Taasisi ya Kiislam ya Istiqaama iliyopo mkoani Tabora yaungua moto

Cannabis

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
8,937
25,279
Shule ya awali na msingi inayomilikiwa na Taasisi ya Kiislam ya Istiqaama iliyopo mkoani Tabora imeungua kwa moto usiku wa kuamkia leo Septemba 27. Hakuna madhara yoyote kwa binadamu yaliyotokea kwa tukio hilo.

=====

Shule ya Awali na Msingi ya Taasisi ya Kiislamu ya Istiqaama iliyopo mkoani Tabora imeungua moto usiku wa kuamkia leo na kuteketeza baadhi ya vitu vya wanafunzi katika bweni moja.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Tabora, Barnabas Mwakalukwa amethibitisha kutokea kwa tukio la kuungua kwa moto kwa shule ya msingi.

Akizungumza na EATV / Radio Digital hii leo Septemba 27, 2020 Kamanda Mwakalukwa amesema kuwa moto huo ambao chanzo chake hakijajulikana haukusababisha madhara yoyote kwa binadamu.

''Ni kweli shule imeungua moto, hakuna madhara yoyote kwa binadamu lakini kuna bweni moja ambalo walikuwa wanakaa wasichana 45 vitu vyao vimeungua moto,” amesema RPC Mwakalukwa

Aidha Kamanda Mwakalukwa amesema kuwa uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea ili kubaini chanzo cha moto huo.

Ei6LzBEXkAozXsS.jpeg
Ei6LxwuXYAAvEHM.jpeg
Ei6Lwh5WAAAphne.jpeg

Shule ya awali na msingi inayomilikiwa na Taasisi ya Kiislam ya Istiqaama iliyopo mkoani Tabora imeungua kwa moto usiku wa
kuamkia leo Septemba 27. Hakuna madhara yoyote kwa binadamu yaliyotokea kwa tukio hilo.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Tabora, Barnabas Mwakalukwa amethibitisha kutokea kwa tukio la kuungua kwa moto kwa shule ya msingi.
Akizungumza na EATV / Radio Digital hii leo Septemba 27, 2020 Kamanda Mwakalukwa amesema kuwa moto huo ambao chanzo chake hakijajulikana haukusababisha madhara yoyote kwa binadamu.

''Ni kweli shule imeungua moto, hakuna madhara yoyote kwa binadamu lakini kuna bweni moja ambalo walikuwa wanakaa wasichana 45 vitu vyao vimeungua moto,” amesema RPC Mwakalukwa

Aidha Kamanda Mwakalukwa amesema kuwa uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea ili kubaini chanzo cha moto huo.
 
Nina mashaka pamoja na mapungufu katika ujenzi, yanayoweza kuleta, hitilafu za umeme n.k.
Nahisi huku nikifikiria nyuma ya keyboard, huenda kuna ubadhirifu mkubwa wa ujenzi, na wahusika, wameamua kuchomoa betri kupoteza ushahidi, au ni mbinu njama, ya kutafuta misaada at the expense of innocent childrens' lives..

Something is fishy! Too fishy!

Everyday is Saturday............................. :cool:
 
hili jambo lisifumbiwe macho.....kwa nini linaendelea?! kuna nini?! kwa nini?!
jeshi la polisi tafadhali sana toeni majibu haraka na kwa wakati. kwa mtiririko huu wa haya matukio ya kuungua moto si ishara nzuri kabisa .....uchunguzi ufanywe kwa haraka na taarifa itolewe, lkn pia kuna haja ya viongozi wa shule kuchukua tahadhari, wekeni ulinzi wa kutosha kwenye shule zenu

kama ni uchakavu wa miundobinu ya umeme tufahamishwe. au kama kuna uhalifu pia itolewe taarifa
 
Tena ni kuweka hiden camera tu, huu mchezo umezidi kipimo.
 
Wala siyo kawaida hii ata mtoto wa la saba ataona kuna jambo linaendelea na hii itakuwa n mbaya sana mana inaweza zua chuki za ajabu, mamlaka nina imani zipo kazini, tumuombe mungu tu atukinge na hizi balaa
 
Back
Top Bottom