Swet-R
JF-Expert Member
- Jul 20, 2018
- 5,613
- 8,042
Watoto siku hizi wanabebeshwa madaftari mengi yenye uzito kuzidi umri wao. Unakutana na mtoto wa darasa la kwanza kabeba mkoba una madaftari 8 mpaka 10, yote yale yenye kurasa nyingi.
Nimekutana na kisa kimoja mtoto wa darasa la pili analalamikia mgongo. Wazazi wake wakawa hawajui ni kwa nini. Baadae nikawaambia wamwangalie anapoenda shule tembea yake akibeba daftari. Ndipo ikagundulika anasumbiliwa na mgongo sababu ya uzito wa madaftari.
Watoto siku hizi wanabebeshwa daftari nyingi lakini bado elimu yetu ndio inazidi kudidimia. Watu wa elimu hawana ubunifu kabisa siku hizi, tofuati na kipindi chetu cha JACKSON MAKWETA. Enzi zetu darasa la kwanza la pili daftari 2 tu la HISABATI NA KISWAHILI. Hili la kiswahili linahusika pia kwenye mwandiko. Na Elimu enzi hizo ilikuwa bora sana.
Hili bunge linafanya nini kuvisemea vitu kama hivi. Wenzetu Kenya mtoto wa darasa la kwanza wanabeba daftari 2,3 na elimu yao iko vizuri kuliko sisi.
Kibaya zaidi watoto siku hizi hawafurahii kabisa utoto wao. Hawapewi hata muda wa kuutumia utoto wao, hawapewi muda wa michezo. Kutwa ni darasani. Mtoto anaanza kwenda shule kama mzaha hivi anapelekwa akashinde na wenzie kuanzia miaka mitatu anapelekwa chekechea, wengine miwili. Hapo akianza tu, ndio ujue imetoka hiyo mpaka chuo kikuu. Mtoto anaamushwa saa 11 anaandaliwa. Basi la shule linamchukua anasinzia humo kwenye gari mpaka kufika shule na kuingia darasani saa 2 anakuwa amechoka kabla hajaanza masomo. Ukitoka darasani anaenda tuition mpaka saa 1 usiku tena anaingia nyumbani akiwa amebeba daftari nyingi, anakuwa amechoka mno.
Wabunge waingilie kati hili. Kizazi kijacho kinapotea mapema kabisa. Ni kama hawaoni hivi
Kuna watu watakuja hapa kusema ndio mtoto akomae. Anakomaa huku elimu ikishuka kwa kasi. Fikiria wewe uliesoma miaka ya 90,mazingira yale na sasa. Na elimu ilivyokuwa bora enzi hizo.