Shule vs Gereza

Ndivyo?

  • Pana chembechembe za ukweli

    Votes: 2 100.0%
  • Urongo mtupu

    Votes: 0 0.0%

  • Total voters
    2
  • Poll closed .

Mlenge

R I P
Oct 31, 2006
2,125
2,291
ShulevsGereza.jpg
CHANZO
: mtandao wa intaneti

MAONI :

1. Sera ya taifa ya elimu inapendekeza mtoto mwenye umri wa miaka mitatu aandikishwe shule ya awali.

2. Sera zinataka elimu ya sekondari iwe ya lazima.

Kwa hiyo miaka ya ukuaji wa awali inalazimishwa kuwa kwenye mazingira ya shule.

3. Shule za binafsi za gharama kubwa sana (za kimataifa) zinapunguza makali ya mfanano kuliko shule za umma au za binafsi za gharama nafuu.

4. Kadiri shule inavyozidi kufanana na gereza, ndivyo wazazi wengi zaidi huisifia kwamba inadumisha "nidhamu".

5. Shule ikiwa ya bweni, tena ya wasichana, basi huwa na mfanano mkubwa zaidi na magereza.

Wadau, si/ni hivyo?
 
Mlenge, post: 25747107
Mkuu hiyo chart yako haipo vizuri hata hivyo nitajitahidi kuchangia maoni yako.
1. Sera ya taifa ya elimu inapendekeza mtoto mwenye umri wa miaka mitatu aandikishwe shule ya awali.
Sioni kama ni tatizo. Maana ya kuandikishwa shule mapema ni kuanza 'socialize' mtoto katika mazingira ya jamii. Watoto wadogo hujifunza vizuri kutoka kwa wenzao na si kwa kusikiliza
Mtoto aliyeanza na shule za awali anachangama vizuri na wenzake 'peers' kuliko aliyeibuka akiwa na umri
2. Sera zinataka elimu ya sekondari iwe ya lazima.
Hili tumelijadili katika mada ya VETA
Mabadiliko ya kidunia yanalazimisha weledi katika kiwango fulani. Sioni kama ni tatizo, ninchoweza kuona tatizo ni je, elimu inayotolewa inakidhi haja ya kiwango cha sekondari au ni wanafunzi kuingia katika vyumba vlivyoandikwa Form IV na kisha kurudi mitaani?
Kwa hiyo miaka ya ukuaji wa awali inalazimishwa kuwa kwenye mazingira ya shule.
Ndiyo! ni wakati ambapo uwezo wa mtoto kuwa 'innovative' au kufikiri kwa upana tu mambo ya kawaida unakuwa mkubwa

Kwa wenzetu nchi zilizoendelea mtoto anaandaliwa kuanzia utotoni si kumsubiri aibuke tu siku za mbeleni
Na hili haliishi katika shule za kitaaluma, ni pamoja na shule za sanaa na michezo
Kuwaacha watoto 'huru' katika miaka ya ukuaji ni kuwajengea mazingira mabovu mbeleni
Mtu haanzi matendo mabaya ukubwani, huanzia udogoni, akifika ukubwani ni experience tu inafanya kazi
3. Shule za binafsi za gharama kubwa sana (za kimataifa) zinapunguza makali ya mfanano kuliko shule za umma au za binafsi za gharama nafuu.
Kiuhalisia shule za binafsi hazina gharama.

Kinachopandisha gharama ni ubovu wa shule za umma na kusababisha 'imbalance kati ya demand and supply'
Inapotokea demand ni kubwa kuliko supply itakuwa reflected katika cost

Niliwahi kusoma mahali Rwanda shule binafsi zinafungwa kwasababu shule za umma zinafanya vema
Ili kukabiliana na tatizo la gharama, lazima quality ya shule za umma iwe nzuri
4. Kadiri shule inavyozidi kufanana na gereza, ndivyo wazazi wengi zaidi huisifia kwamba inadumisha "nidhamu".
Mafanikio iwe ya elimu, sanaa au michezo ni zao la nidhamu.
Huwezi kutenga mapacha hao kwa namna yoyote ukapata matokeo tarajiwa.

Shule kufanana na gereza si tatizo la mfumo au mitaala, ni mapungufu ya wasimamizi na walezi wa shule husika
Sheria zinaweza kuwepo na bado wanafunzi wakafurahia shule, inategemea sheria zinafuatwa kwa namna gani na nani anasimamia. Msimamizi akiwa mbovu shule ni mbaya kuliko gereza na kinyume chake
5. Shule ikiwa ya bweni, tena ya wasichana, basi huwa na mfanano mkubwa zaidi na magereza.
Nadhani hapa kuna kitu kinaitwa 'vulnerability' hasa kwa wasichana.

Tunarudi pale pale kuhusu usimamizi na ulezi na weledi wa wanaosimamia.
Kuna 'thin line between' uwepo wa nidhani (discipline) na protection kwa maana ya kuwalinda dhidi ya ''vulnerability''

Nakubaliana nawe kuwa ii shule iwe mahali pa kujifunza na siyo gereza lazima kuwe na freedom
Labda tujiulize, freedom gani tunayozungumzia, academic freedom au freedom ya kutenda mhusika anavyojisikia

Academic freedom ni jambo muhimu sana na kwa bahati mbaya mfumo wetu wa elimu haujazingatia hilo
Unaweza kuona kuanzia mashuleni, vyuoni hadi vyuo vikuu ambapo watu hawana fursa ya 'academic freedom'
Hili linachangia sana kudumuza wahitimu wetu kwasababu dunia ya sasa ni ya solution si ya kutema notisi

Dunia ya leo si kuhusu umefaulu kiwango gani, bali unawezaje kujieleza, kueleza, kutafuta suluhu na namna gani unatumia elimu katika mazingira unayohitajika. Ukiangalia wahitimu wetu hilo ni tatizo kubwa sana

Kachukue mwanafunzi kutoka South Africa, Uganda , Kenya, Tanzania au Egypt halafu wape changamoto ya jambo fulani na uwape uhuru wa kuzungumza kwa lugha wanayotaka, ninakuhakikisha Watanzania watakwama

Kukwama si kuwa hawajui, bali uwezo wao upo katika taaluma na hawawezi ku transfer knowledge wakaeleweka
Hili ni tatizo linaloanza kwa kukosa 'academic freedom'

Kuhusu uhuru tu wa kila mmoja, sikubaliani na hoja ya kuacha kila mmoja atende atakavyo

Hakuna institution yoyote ya jamii isiyokuwa na miongozo.
Yes miongozo inaweza kuwa mikali lakini ukali huchagizwa na mhusika.

Kutoa uhuru tu kwa kila mmoja ni kunyang'anya uhuru kwa wengine, uhuru lazima uwe na mipaka unapoanzia na unapoishia na hapo ndipo makali ya sheria yanapoonekana na huenda kutafsiriwa kama 'gereza'
 
Back
Top Bottom