Shule Usukumani, mtaala Cambridge!

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
“SHULE zetu za msingi na sekondari ni lazima ziwatayarishe vijana wetu kukabiliana na hali halisi na mahitaji ya Tanzania. Kufanya hivyo kunahitaji mabadiliko ya kimapinduzi, siyo tu katika mfumo wa elimu lakini pia katika tabia zilizojengeka katika jumuiya”.

Wapendwa, leo nimeshawishika kuanza na nukuu hiyo ya Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere iliyomo katika mada aliyoitoa mwaka 1967 kuhusu Elimu ya Kujitegemea. Nimeamua nianze nayo kwa sababu ndilo suala ninalotaka tulijadili wiki hii.

Kilichonichochea kuzungumzia suala la elimu wiki hii ni tukio moja lililotokea, takriban wiki mbili zilizopita, huko Shinyanga la uzinduzi wa shule moja ya sekondari inayoitwa Savannah Plains International School.

Shule hiyo, inayomilikiwa na mjumbe wa NEC ya CCM anayewakilisha mkoa wa Shinyanga, Hilal Hamad, ilizinduliwa na Rais Jakaya Kikwete katika sherehe kamambe zilizotangazwa moja kwa moja na kituo cha televisheni cha Star TV. Shule hiyo imegharimu shilingi bilioni 21 na ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 97.

Mpendwa msomaji, nina hakika utakubaliana nami kwamba kwa mkoa kama Shinyanga ambao uko nyuma karibu kwa kila kitu, uzinduzi wa shule

kubwa iliyogharimu mapesa mengi kiasi hicho, zinapaswa kuwa habari njema si tu kwa wakazi masikini wa mkoa huo; bali pia kwa Watanzania wote wanaopenda maendeleo ya nchi yao.

Utafiti uliofanywa unaonyesha kwamba mkoa wa Shinyanga si tu kwamba ni miongoni mwa mikoa ya Kanda ya Ziwa inayoongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya watu, lakini pia unaongoza kwa mauaji ya vikongwe na watu wenye ulemavu wa ngozi (albino). Na hiyo ni kutokana na imani potofu za kishirikina zilizokita mizizi katika mkoa huo.

Aidha, inasadikiwa katika mkoa huo kwamba mtu hafi isipokuwa kwa “mkono wa mtu”; kwa maana ya kulogwa, jambo linalosababisha kutafuta sababu za magonjwa na kifo kwa wapiga ramli, badala ya kutafuta kisayansi vyanzo vya vifo na magonjwa hayo. Kwa ufupi, kama kuna mikoa mitatu iliyobobea nchini kwa imani za kishirikina, Shinyanga ni mmojawao.

Na kwa upande wa elimu, mambo ni hovyo zaidi. Taarifa zinaonyesha kwamba Mkoa wa Shinyanga umekuwa wa mwisho katika matokeo ya mitihani ya shule za msingi na sekondari nchini kwa miaka mingi mfululizo.

Hiyo ndiyo picha ya Shinyanga. Na sitaki kuzungumzia hapa kwamba pamoja na hali hiyo duni ya maisha ya wakazi wa Shinyanga (maisha ya kuwaabudu Sangoma katika karne ya sayansi na teknolojia), mkoa huo umezungukwa na utajiri mkubwa wa madini; hususan dhahabu.

Sitaki kulizungumzia hilo leo; kwani lenyewe linastahili makala ya peke yake. Itoshe tu kusema hapa kwamba kama mikoa mingine katika Tanzania inatembea, mkoa wa Shinyanga bado unatambaa!

Kwa hiyo, katika mazingira kama hayo ya Shinyanga, unaposikia kwamba kuna shule kamambe imejengwa na kuzinduliwa mkoani humo, unapaswa kufurahi na kufarijika. Unapaswa kufurahi na kufarijika kwa sababu, kimsingi, tatizo kuu la mkoa wa Shinyanga ni kuwa na wakazi wengi vijijini wajinga – yaani wakazi ambao hawajaona vya kutosha mwanga wa elimu.

Lakini je, tunapaswa kufurahi na kufarijika kwa sababu shule inayoitwa Savannah Plains International School imezinduliwa mkoani Shinyanga? Je, ni kwa kiasi gani shule hii mpya itachangia kuuondoa ujinga wa wakazi wa Shinyanga ili wakazi wake waachane na imani za kishirikina ili hatimaye waondokane na umasikini na kujipatia maendeleo?

Sijui jibu la wadau wa elimu nchini; hususan wajuzi na wachambuzi wa sekta ya elimu nchini, ni lipi; lakini kwa mtazamo wangu, mchango wa shule hiyo mpya katika kutatua matatizo hayo ya mkoa wa Shinyanga niliyoyaeleza mwanzoni, utakuwa mdogo mno.

Utakuwa mdogo mno kwa sababu, kimsingi, shule hiyo mpya haikujengwa kwa ajili ya Wasukuma wa Shinyanga; bali imejengwa kwa ajili ya watoto wa wafanyakazi wa kigeni walioko katika migodi ya madini ya Kanda ya Ziwa, na hasa wa Afrika Kusini.

Nasema hivyo; kwani si siri kwamba migodi hiyo imejaa wafanyakazi wengi wa kigeni kutoka Afrika Kusini, Canada na kwingineko ambao hawakuwa na shule ya hadhi ya Savannah kwa ajili ya watoto wao.

Na uthibitisho huo naupata kutoka katika maelezo yaliyotolewa wakati wa uzinduzi wake. Ilielezwa kwamba shule hiyo inaendeshwa kwa kuzingatia mtaala (curriculum) wa kitaifa wa nchini Uingereza kwa wanafunzi hadi kidato cha pili, na mitaala ya mitihani ya Cambridge kwa vidato kuanzia cha tatu hadi cha sita.

Ilielezwa pia kwamba kwa sasa walimu wote wa shule hiyo ni wa kigeni (wazungu?) na kwamba wanafunzi ni kutoka nje ya nchi na ndani ya nchi.

Kwa maana hiyo, mpendwa msomaji, mimi nitakuwa mtu wa mwisho kuamini kwamba shule iliyojengwa Shinyanga inayofuata curriculum ya Uingereza ikiwemo ya Cambridge, itawanufaisha watoto wa Wasukuma masikini wa Shinyanga!

Kwa maneno mengine, naamini shule hiyo ni kwa ajili ya watoto wa wageni wanaofanya kazi katika migodi ya Kanda ya Ziwa na wengine kutoka nje ya nchi, na of course watoto wachache wa Watanzania wenye uwezo, na hasa wale wanaopapatikia shule zenye curriculum za Cambridge.

Nirudie tena kusisitiza hoja yangu:

Uwekezaji katika elimu wa shule yenye mitaala ya kigeni (Uingereza) kama hiyo, hautausaidia mkoa huo wa Shinyanga wala Taifa, kwa sababu mengi yatakayofundishwa ni kuhusu Ulaya, na kidogo zaidi kuhusu jamii ya Kitanzania; kiasi kwamba hayaendani na hali halisia ya maisha ya jamii yetu.

Ni kweli kwamba mkoa wa Shinyanga ni mmoja wa mikoa masikini Tanzania; licha ya kuzungukwa na migodi ya dhahabu. Ni kweli pia kwamba ki-elimu, mkoa wa Shinyanga ni miongoni mwa mikoa ya mwisho nchini, na hata matokeo ya mitihani ya taifa yanaonyesha hivyo. Ni kweli pia kwamba, kwa sababu ya kuwa nyuma ki-elimu, Shinyanga ni miongoni mwa mikoa nchini inayoongoza kwa imani za kishirikina.

Kama ukweli wa mazingira ya Shinyanga ndiyo huo, nisisitize kwamba ufumbuzi wa matatizo yote hayo haupo katika mkoa huo kuwa na shule hizi zinazoitwa international zenye mitaala ya Ungereza! Na hapo ndipo ninapotaka tuirejee nukuu ile niliyoanza nayo ya Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere.

Najua kwamba kuna shule nyingi tu nchini za binafsi zinazojiita international (hata kama hazina wanafunzi wa kigeni) zinazofuata mitaala ya Uingereza kama hiyo ya Savannah, na kwa hiyo kuna wanaoweza kuuliza ni kwa nini niisakame shule hiyo moja tu kwa kufuata mitaala ya Cambridge; ilhali zipo nyingi tu nchini.

Jibu langu kwao ni moja – makosa mawili hayafanyi jambo kuwa sahihi (two wrongs do not make a right), na isitoshe; shule hizo nyingine zipo kwenye mikoa yenye wakazi wenye afadhali kidogo kielimu kama vile Moshi, Arusha na Dar es salaam, na si mkoa kama Shinyanga ambako bado katika zama hizi watu wanaua albino wakiamini watakuwa matajiri!

Ninaamini kabisa toka moyoni kwamba kama Bw. Hilal Hamad, ambaye ni mjumbe wa NEC ya CCM, angekuwa na dhamira ya kweli ya kuwainua kielimu na kimaisha wakazi masikini wa Shinyanga, angalitumia Sh. bilioni hizo 21 kujenga shule angalau mbili tatu hivi katika vijiji vya mkoa huo na kuzipa waalimu wa kutosha, vitabu na maabara; shule ambazo wanavijiji wangemudu gharama, na ambazo watoto wangefundishwa kwa kufuata mtaala wa hapa hapa nchini.

Kwa kufanya hivyo, angekuwa amesaidia kuwaandaa vijana wetu wa mkoa huo kuzikabili changamoto za Shinyanga. Kwa maneno mengine, angewapa elimu ambayo ingewawezesha kukabiliana na mazingira yanayowazunguka; na hivyo ndivyo Nyerere alivyomaanisha katika nukuu yake ile.

Sielewi ni vipi Bw. Hamad, ambaye ni kiongozi wa CCM, ameamua kutumia mabilioni ya mapesa yake kutoa elimu kwa watoto wa wageni; ilhali wazazi wa ‘watoto wa nyumbani’, kwenye mkoa wake mwenyewe, bado wamekita kwenye imani za kishirikina zinazoshamirishwa na ujinga!

Ni vyema kwamba katika hotuba yake ya kuzindua shule hiyo; Rais Kikwete alikazia umuhimu wa elimu kwa mkoa wa Shinyanga katika kuondokana na tunguri na nguvu za giza; ingawa shule yenyewe ambako alitoa hotuba hiyo ni kwa ajili ya watoto wa wageni na wa Watanzania wachache wenyenacho, na si shule ya watoto wa masikini ambao ndiyo hasa wana tatizo hilo la kuabudu tunguri.

Rais Kikwete alisema hivi wakati akifungua shule hiyo: “Ni jambo la kusikitisha kwamba wakati wenzetu wa nchi zilizoendelea wanapiga hatua ya maendeleo kwa kuongozwa na sayansi na teknolojia, sisi bado tunayatafuta maendeleo hayo kwa kupiga ramli”.

Kwa nini aliamua kuzungumzia suala hilo la elimu vs kupiga ramli katika shule ambayo, kwa kiasi kikubwa, ni kwa ajili ya wageni, na ambayo mitaala inayofuatwa ni ya Uingereza (Cambridge)?

Je, Rais Kikwete huyo huyo ambaye aliiagiza Wizara ya Elimu, hivi karibuni, kuhakikisha shule zote nchini zinatumia vitabu vya kiada vinavyofanana, anajua kwamba kuna shule nyingi za sekondari za binafsi nchini, kama hiyo ya Shinyanga, zinazofuata mtaala wa Cambridge?

Kama anajua, ni kwa kiasi gani anaamini kuwa shule hiyo, kwa ajili ya wageni na Watanzania wachache wenye uwezo, na yenye kufuata mitaala ya Uingereza, inaweza kuwasaidia Wasukuma kuachana na tabia hiyo ya kupiga ramli?

Sitaki kuizungumzia zaidi hotuba hiyo ya Kikwete; maana kuna wasomaji kadhaa, wiki iliyopita, walinitumia sms wakilalamika kwamba namwandama bure Rais Kikwete; nami sitaki nionekane hivyo; japo ni wajibu wetu sote kumkumbusha kwamba yeye ni rais, na rais ni kiongozi si mtawala!

Nikirejea kwenye hoja ya msingi ambayo ni suala la elimu, nashawishika kuwauliza Watanzania wenzangu kama kweli kuna mantiki ya kujenga shule Usukumani, kwenye umasikini mkubwa na imani kedekede za kishirikina, na kisha shule hiyo ikawa ni kwa matajiri wachache; hususan wageni.

Nahoji vilevile kama kuna mantiki kujenga shule Usukumani, na kisha ikafuata mtaala wa Cambridge! Sote tunajua kwamba shule za namna hiyo zinawaandaa wanafunzi wake kuishi na kufanya kazi Ulaya, na si kuishi na kufanya kazi Dar es Salaam; achilia mbali Usukumani.

Nihitimishe kwa kusema kwamba tuna tatizo Tanzania na aina ya elimu tunayowapa vijana wetu. Elimu hii ya kutumia mitaala ya Cambridge inayowaandaa vijana wetu kufanya kazi London, haitatufikisha popote - haitatusaidia kukabiliana na mazingira yetu yenye changamoto kibao zinazotokana na kudumaa kwetu kwa miaka mingi kimaendeleo.

Na inapotokea kiongozi wa CCM (kama Bw. Hamad) ndiye anakuwa mstari wa mbele kujenga shule kwa ajili ya wageni; tena yenye kufuata mtaala wa Uingereza, tena katika mkoa ambao kielimu ni wa mwisho, ujue tatizo ni kubwa kuliko tunavyofikiria.

Nimalizie kwa kurejea tena nukuu nyingine ya Mwalimu Nyerere: “Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.”

Ndugu zangu, hatuwezi kuamka kama taifa na wala hatuwezi kubadili mawazo na matumaini ya taifa kama tutaendelea kuwapa vijana wetu elimu inayofuata mitaala ya Cambridge; labda kama tunawaandaa kufanya kazi nje ya nchi (London)!

Tafakari.
 
Sasa unapagawa nin na calculation za mfanyabiashara kuwekeza kwenye investment anayoona itamlipa..?

Huelewi dunia imekuwa kijiji na vijana wanandaliwa kupambana na changamoto za dunia nzima sio Tanzania pekee... unaweka siasa kwenye biashara za mtu mkuu?
Mbona hiyo shule haitakuwa ya kwanza wala ya mwisho kutoa elimu ya kimataifa nchini au tatizo ni shinyanga
 
SHULE zetu za msingi na sekondari ni lazima ziwatayarishe vijana wetu kukabiliana na hali halisi na mahitaji ya Tanzania. Kufanya hivyo kunahitaji mabadiliko ya kimapinduzi, siyo tu katika mfumo wa elimu lakini pia katika tabia zilizojengeka katika jumuiya.

Wapendwa, leo nimeshawishika kuanza na nukuu hiyo ya Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere iliyomo katika mada aliyoitoa mwaka 1967 kuhusu Elimu ya Kujitegemea. Nimeamua nianze nayo kwa sababu ndilo suala ninalotaka tulijadili wiki hii.

Kilichonichochea kuzungumzia suala la elimu wiki hii ni tukio moja lililotokea, takriban wiki mbili zilizopita, huko Shinyanga la uzinduzi wa shule moja ya sekondari inayoitwa Savannah Plains International School.

Shule hiyo, inayomilikiwa na mjumbe wa NEC ya CCM anayewakilisha mkoa wa Shinyanga, Hilal Hamad, ilizinduliwa na Rais Jakaya Kikwete katika sherehe kamambe zilizotangazwa moja kwa moja na kituo cha televisheni cha Star TV. Shule hiyo imegharimu shilingi bilioni 21 na ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 97.

Mpendwa msomaji, nina hakika utakubaliana nami kwamba kwa mkoa kama Shinyanga ambao uko nyuma karibu kwa kila kitu, uzinduzi wa shule

kubwa iliyogharimu mapesa mengi kiasi hicho, zinapaswa kuwa habari njema si tu kwa wakazi masikini wa mkoa huo; bali pia kwa Watanzania wote wanaopenda maendeleo ya nchi yao.

Utafiti uliofanywa unaonyesha kwamba mkoa wa Shinyanga si tu kwamba ni miongoni mwa mikoa ya Kanda ya Ziwa inayoongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya watu, lakini pia unaongoza kwa mauaji ya vikongwe na watu wenye ulemavu wa ngozi (albino). Na hiyo ni kutokana na imani potofu za kishirikina zilizokita mizizi katika mkoa huo.

Aidha, inasadikiwa katika mkoa huo kwamba mtu hafi isipokuwa kwa mkono wa mtu; kwa maana ya kulogwa, jambo linalosababisha kutafuta sababu za magonjwa na kifo kwa wapiga ramli, badala ya kutafuta kisayansi vyanzo vya vifo na magonjwa hayo. Kwa ufupi, kama kuna mikoa mitatu iliyobobea nchini kwa imani za kishirikina, Shinyanga ni mmojawao.

Na kwa upande wa elimu, mambo ni hovyo zaidi. Taarifa zinaonyesha kwamba Mkoa wa Shinyanga umekuwa wa mwisho katika matokeo ya mitihani ya shule za msingi na sekondari nchini kwa miaka mingi mfululizo.

Hiyo ndiyo picha ya Shinyanga. Na sitaki kuzungumzia hapa kwamba pamoja na hali hiyo duni ya maisha ya wakazi wa Shinyanga (maisha ya kuwaabudu Sangoma katika karne ya sayansi na teknolojia), mkoa huo umezungukwa na utajiri mkubwa wa madini; hususan dhahabu.

Sitaki kulizungumzia hilo leo; kwani lenyewe linastahili makala ya peke yake. Itoshe tu kusema hapa kwamba kama mikoa mingine katika Tanzania inatembea, mkoa wa Shinyanga bado unatambaa!

Kwa hiyo, katika mazingira kama hayo ya Shinyanga, unaposikia kwamba kuna shule kamambe imejengwa na kuzinduliwa mkoani humo, unapaswa kufurahi na kufarijika. Unapaswa kufurahi na kufarijika kwa sababu, kimsingi, tatizo kuu la mkoa wa Shinyanga ni kuwa na wakazi wengi vijijini wajinga yaani wakazi ambao hawajaona vya kutosha mwanga wa elimu.

Lakini je, tunapaswa kufurahi na kufarijika kwa sababu shule inayoitwa Savannah Plains International School imezinduliwa mkoani Shinyanga? Je, ni kwa kiasi gani shule hii mpya itachangia kuuondoa ujinga wa wakazi wa Shinyanga ili wakazi wake waachane na imani za kishirikina ili hatimaye waondokane na umasikini na kujipatia maendeleo?

Sijui jibu la wadau wa elimu nchini; hususan wajuzi na wachambuzi wa sekta ya elimu nchini, ni lipi; lakini kwa mtazamo wangu, mchango wa shule hiyo mpya katika kutatua matatizo hayo ya mkoa wa Shinyanga niliyoyaeleza mwanzoni, utakuwa mdogo mno.

Utakuwa mdogo mno kwa sababu, kimsingi, shule hiyo mpya haikujengwa kwa ajili ya Wasukuma wa Shinyanga; bali imejengwa kwa ajili ya watoto wa wafanyakazi wa kigeni walioko katika migodi ya madini ya Kanda ya Ziwa, na hasa wa Afrika Kusini.

Nasema hivyo; kwani si siri kwamba migodi hiyo imejaa wafanyakazi wengi wa kigeni kutoka Afrika Kusini, Canada na kwingineko ambao hawakuwa na shule ya hadhi ya Savannah kwa ajili ya watoto wao.

Na uthibitisho huo naupata kutoka katika maelezo yaliyotolewa wakati wa uzinduzi wake. Ilielezwa kwamba shule hiyo inaendeshwa kwa kuzingatia mtaala (curriculum) wa kitaifa wa nchini Uingereza kwa wanafunzi hadi kidato cha pili, na mitaala ya mitihani ya Cambridge kwa vidato kuanzia cha tatu hadi cha sita.

Ilielezwa pia kwamba kwa sasa walimu wote wa shule hiyo ni wa kigeni (wazungu?) na kwamba wanafunzi ni kutoka nje ya nchi na ndani ya nchi.

Kwa maana hiyo, mpendwa msomaji, mimi nitakuwa mtu wa mwisho kuamini kwamba shule iliyojengwa Shinyanga inayofuata curriculum ya Uingereza ikiwemo ya Cambridge, itawanufaisha watoto wa Wasukuma masikini wa Shinyanga!

Kwa maneno mengine, naamini shule hiyo ni kwa ajili ya watoto wa wageni wanaofanya kazi katika migodi ya Kanda ya Ziwa na wengine kutoka nje ya nchi, na of course watoto wachache wa Watanzania wenye uwezo, na hasa wale wanaopapatikia shule zenye curriculum za Cambridge.

Nirudie tena kusisitiza hoja yangu:

Uwekezaji katika elimu wa shule yenye mitaala ya kigeni (Uingereza) kama hiyo, hautausaidia mkoa huo wa Shinyanga wala Taifa, kwa sababu mengi yatakayofundishwa ni kuhusu Ulaya, na kidogo zaidi kuhusu jamii ya Kitanzania; kiasi kwamba hayaendani na hali halisia ya maisha ya jamii yetu.

Ni kweli kwamba mkoa wa Shinyanga ni mmoja wa mikoa masikini Tanzania; licha ya kuzungukwa na migodi ya dhahabu. Ni kweli pia kwamba ki-elimu, mkoa wa Shinyanga ni miongoni mwa mikoa ya mwisho nchini, na hata matokeo ya mitihani ya taifa yanaonyesha hivyo. Ni kweli pia kwamba, kwa sababu ya kuwa nyuma ki-elimu, Shinyanga ni miongoni mwa mikoa nchini inayoongoza kwa imani za kishirikina.

Kama ukweli wa mazingira ya Shinyanga ndiyo huo, nisisitize kwamba ufumbuzi wa matatizo yote hayo haupo katika mkoa huo kuwa na shule hizi zinazoitwa international zenye mitaala ya Ungereza! Na hapo ndipo ninapotaka tuirejee nukuu ile niliyoanza nayo ya Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere.

Najua kwamba kuna shule nyingi tu nchini za binafsi zinazojiita international (hata kama hazina wanafunzi wa kigeni) zinazofuata mitaala ya Uingereza kama hiyo ya Savannah, na kwa hiyo kuna wanaoweza kuuliza ni kwa nini niisakame shule hiyo moja tu kwa kufuata mitaala ya Cambridge; ilhali zipo nyingi tu nchini.

Jibu langu kwao ni moja makosa mawili hayafanyi jambo kuwa sahihi (two wrongs do not make a right), na isitoshe; shule hizo nyingine zipo kwenye mikoa yenye wakazi wenye afadhali kidogo kielimu kama vile Moshi, Arusha na Dar es salaam, na si mkoa kama Shinyanga ambako bado katika zama hizi watu wanaua albino wakiamini watakuwa matajiri!

Ninaamini kabisa toka moyoni kwamba kama Bw. Hilal Hamad, ambaye ni mjumbe wa NEC ya CCM, angekuwa na dhamira ya kweli ya kuwainua kielimu na kimaisha wakazi masikini wa Shinyanga, angalitumia Sh. bilioni hizo 21 kujenga shule angalau mbili tatu hivi katika vijiji vya mkoa huo na kuzipa waalimu wa kutosha, vitabu na maabara; shule ambazo wanavijiji wangemudu gharama, na ambazo watoto wangefundishwa kwa kufuata mtaala wa hapa hapa nchini.

Kwa kufanya hivyo, angekuwa amesaidia kuwaandaa vijana wetu wa mkoa huo kuzikabili changamoto za Shinyanga. Kwa maneno mengine, angewapa elimu ambayo ingewawezesha kukabiliana na mazingira yanayowazunguka; na hivyo ndivyo Nyerere alivyomaanisha katika nukuu yake ile.

Sielewi ni vipi Bw. Hamad, ambaye ni kiongozi wa CCM, ameamua kutumia mabilioni ya mapesa yake kutoa elimu kwa watoto wa wageni; ilhali wazazi wa watoto wa nyumbani, kwenye mkoa wake mwenyewe, bado wamekita kwenye imani za kishirikina zinazoshamirishwa na ujinga!

Ni vyema kwamba katika hotuba yake ya kuzindua shule hiyo; Rais Kikwete alikazia umuhimu wa elimu kwa mkoa wa Shinyanga katika kuondokana na tunguri na nguvu za giza; ingawa shule yenyewe ambako alitoa hotuba hiyo ni kwa ajili ya watoto wa wageni na wa Watanzania wachache wenyenacho, na si shule ya watoto wa masikini ambao ndiyo hasa wana tatizo hilo la kuabudu tunguri.

Rais Kikwete alisema hivi wakati akifungua shule hiyo: Ni jambo la kusikitisha kwamba wakati wenzetu wa nchi zilizoendelea wanapiga hatua ya maendeleo kwa kuongozwa na sayansi na teknolojia, sisi bado tunayatafuta maendeleo hayo kwa kupiga ramli.

Kwa nini aliamua kuzungumzia suala hilo la elimu vs kupiga ramli katika shule ambayo, kwa kiasi kikubwa, ni kwa ajili ya wageni, na ambayo mitaala inayofuatwa ni ya Uingereza (Cambridge)?

Je, Rais Kikwete huyo huyo ambaye aliiagiza Wizara ya Elimu, hivi karibuni, kuhakikisha shule zote nchini zinatumia vitabu vya kiada vinavyofanana, anajua kwamba kuna shule nyingi za sekondari za binafsi nchini, kama hiyo ya Shinyanga, zinazofuata mtaala wa Cambridge?

Kama anajua, ni kwa kiasi gani anaamini kuwa shule hiyo, kwa ajili ya wageni na Watanzania wachache wenye uwezo, na yenye kufuata mitaala ya Uingereza, inaweza kuwasaidia Wasukuma kuachana na tabia hiyo ya kupiga ramli?

Sitaki kuizungumzia zaidi hotuba hiyo ya Kikwete; maana kuna wasomaji kadhaa, wiki iliyopita, walinitumia sms wakilalamika kwamba namwandama bure Rais Kikwete; nami sitaki nionekane hivyo; japo ni wajibu wetu sote kumkumbusha kwamba yeye ni rais, na rais ni kiongozi si mtawala!

Nikirejea kwenye hoja ya msingi ambayo ni suala la elimu, nashawishika kuwauliza Watanzania wenzangu kama kweli kuna mantiki ya kujenga shule Usukumani, kwenye umasikini mkubwa na imani kedekede za kishirikina, na kisha shule hiyo ikawa ni kwa matajiri wachache; hususan wageni.

Nahoji vilevile kama kuna mantiki kujenga shule Usukumani, na kisha ikafuata mtaala wa Cambridge! Sote tunajua kwamba shule za namna hiyo zinawaandaa wanafunzi wake kuishi na kufanya kazi Ulaya, na si kuishi na kufanya kazi Dar es Salaam; achilia mbali Usukumani.

Nihitimishe kwa kusema kwamba tuna tatizo Tanzania na aina ya elimu tunayowapa vijana wetu. Elimu hii ya kutumia mitaala ya Cambridge inayowaandaa vijana wetu kufanya kazi London, haitatufikisha popote - haitatusaidia kukabiliana na mazingira yetu yenye changamoto kibao zinazotokana na kudumaa kwetu kwa miaka mingi kimaendeleo.

Na inapotokea kiongozi wa CCM (kama Bw. Hamad) ndiye anakuwa mstari wa mbele kujenga shule kwa ajili ya wageni; tena yenye kufuata mtaala wa Uingereza, tena katika mkoa ambao kielimu ni wa mwisho, ujue tatizo ni kubwa kuliko tunavyofikiria.

Nimalizie kwa kurejea tena nukuu nyingine ya Mwalimu Nyerere: Taifa letu taifa lolote ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.

Ndugu zangu, hatuwezi kuamka kama taifa na wala hatuwezi kubadili mawazo na matumaini ya taifa kama tutaendelea kuwapa vijana wetu elimu inayofuata mitaala ya Cambridge; labda kama tunawaandaa kufanya kazi nje ya nchi (London)!

Tafakari.
Umeandika uharo mtupu ! Eti Arusha kuna utajiri na wasomi ! Pole sana hao wamasai tunaowarushia maji huko Monduli, Ngorongoro na Longido ndio wasomi. Kwa ufupi wewe ni mjinga fulani usiyelewa kitu.
 
Back
Top Bottom