Shule taabani: Mwalimu Mmoja - Chekechea hadi Darasa la Saba... Lakini yafaulisha wanafunzi wote

Hii ni aibu kubwa sana wakati viongozi wakiendelea kuiba mabilioni ya wananchi hali imeendelea kuwa mbaya sana kwenye sekta ya elimu hivi wao hawaioni hii aibu kubwa kiasi hiki viongozi badilikeni kawambwa unasubiri nini kuwajibika! Huu ndio upuuzi wa serikali ya ccm.
 
Wanasiasa wanagombania kuongeza ruzuku tu bungeni, hawana haja na waliowachagua hadi wakati wa uchaguzi!
 
Wanaccm nijibuni,
Naibu waziri wa elimu na mafunzo alipokuwa anafunga shule zisizo na sifa hakuiona ile shule ya msingi ya serikali yenye mwalimu mmoja, chumba kimoja cha darasa cha nyasi wanamosomea kuanzia chekechea hadi drs la saba, ubao mmoja iliyoko mkoa wa Pwani halafu eti darasa la saba wote wamefaulu?
 
Hiyo shule iliachwa kwaajili ya makumbusho, huoni sasa tumefahamu jinsi gani elimu yetu ilivyonjia panda kupitia hiyo shule.
 
Kuna Lizaboni, Foxy ,na waturusha matusi wenzao bila ya kujali wanacho kisema sasa waje waseme.Wakiambiwa wanafanya siasa za kipuuzi mno .Yaani Bagamoyo na Dar kweli haya yako mwaka 2015.
 
maisha bora kwa kila mtz.
hiyo wilaya haina hata madiwani?
mkurugenzi+DC bado hawajajiuzuru hadi sasa?
Hela za mem na mesi zinafanya kazi wapi?
au wanasubiri kamati iundwe?
CHAMA cha walimu,mnaonaje mkimsimamia huyo mwalimu kupata tuzo ya NOBEL.
Hivi Kawambwa na Mulugo bado wapo ofisini?
 


Sasa mwashangaa nini! hivi ni vitu vya kawaida tu; shuhudieni na hapa;

shule-1.jpg


Madarasa mawili kwa wakati moja chini ya mti!
Ushishangae ukiambiwa hii shule imeshika nafasi ya kwanza kiwilaya/kimkoa!
Naam, ndiyo Tanzania ya CCM...majanga matupu!

FaizaFoxy! uko wapi njoo uelezee hii tafadhali!
 
Nadhani hii shule ipo karibu na Sekondari ya Kata,hivyo kwa kuwa shule hiyo ya sekondari ya kata ipo mbali na shule nyingine ndio maana wanafunzi hawa wakapata nafasi! Ni hayo tu BRN JUU,KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI! Mnaweza kukaa! ~Wapi FF?
 
Kama hii ni kweli...basi wizara ya elimu inapaswa kujitathmini vizuri kama kweli inaitakia nchi mema au la..huyo mwalimu ni shujaa...AMAZING STUFF!
 
So interesting. Mwalimu yuko smart for any way, amewaonesha majibu au wamefanya mtihani wenyewe kwa kufundishwa. Ni mwalimu mwenye uwezo ingawa hajawezeshwa, kama angetumika ipasavyo hakika elimu ingekuwa pengine. Pia inawezekana kuwadrill wanafunzi kwani nature ya mitihani yetu 'memorization' then 'reproducing'. Idadi ya 12 students ni rahisi kufanya jambo (no matter the nature of the classroom) na kwa mitihani yetu it is possible Congratulation, let them try their other chances in secondary education. Huu mchezo wa elimu yetu umeshatugarimu sana watanzania na hatujielewi kabisa, elimu yetu haitubadilishi, vyeti tunavyo lakini hakuna kinachofanana na pass mark tulizonazo, na huo ndio mtaji wa wanaotutawala. tumeshapoteza direction, tunatumika watakavyo. we need to take action now. tusome alama za nyakati. soma tu comment nyingi humu utagundua watu hawawazi kesho, fikiri unachojihusisha na future yako ya baadae na husiangalie ya muda mfupi. Acha Siasa kwenye mambo ya Msingi, Elimu ndio mtaji wa watanzania kujiendeleza.
 
Hakuna cha kufaulu maana sasa hivi hakuna drs la saba asiyeenda kidato cha kwanza ajue au asijue kusoma! Cha kumpongeza mwalimu ni kukubali kufanya kazi ktk shule hiyo ktk mkoa anaotoka waziri na rais wa nchi!!!
 
Ni mheshimiwa shukuru kawambwa, ndipo kwa kina young bilionear ritzmoja k na pia mkulu wa hano ndo anatokea wilaya hiyo hiyo ya Bwagamoyo
Samahani,mi nauliza tu,hao wananchi wanaoishi eneo hilo (jimbo la uchaguzi) wana mwakilishi bungeni?
 
Hakuna cha kufaulu maana sasa hivi hakuna drs la saba asiyeenda kidato cha kwanza ajue au asijue kusoma! Cha kumpongeza mwalimu ni kukubali kufanya kazi ktk shule hiyo ktk mkoa anaotoka waziri na rais wa nchi!!!

Umesema kweli.
 
Me namshangaa hata Rais huwa anajitoa sana kwenye misiba ya wasanii,mara amechanga 10 m,mara sijui shing ngapi sijui.
Hizo hizo 10m zisingetosha hata kumjengea madarasa mawili huyo mwalimu?
cha kushangaza zaidi ni sehemu ya kwao kabisa.
 
Back
Top Bottom