Shule taabani: Mwalimu Mmoja - Chekechea hadi Darasa la Saba... Lakini yafaulisha wanafunzi wote

Dr kawambwa ni mbunge wa Bagamoyo na waziri wa Elimu, kweli ccm ni mzigo
 
Tanzania wanafunzi wachache wanaofauru kihalali nina uhakika aslimia 100%
 
nyie mnashangaa machala? balaa lipo tuka misasa, chalinze mzee na malivundo ps. bagamoyo kuna kazi, mfano hyo chalnze mzee ipo km chache kutoka katka kasri la JK msoga lakini ofisi ya m/mkuu kilikuwa choo zaman.
 
Hivi hii nchi inaelekewa wapi jamani. Katika ulimwengu huu wa dot com bado kuna shule kama hii kweli alafu tunatembea kifua mbele tukisema tumethubutu na tumeweza. Nikiona vitu kama hivi najiuliza watu kama Chris Lukosi na wenzake ambao wanaishi au wamewahi kuishi nje ya nchi hii na bado wanaishabikia CCM kweli akili zao ziko sawa!
 
samahani,mi nauliza tu,hao wananchi wanaoishi eneo hilo (jimbo la uchaguzi) wana mwakilishi bungeni?

kama kumbukumbu zangu ziko sawa mbunge wa eneo hilo ni kawambwa, vinginevyo mwenye ufahamu mzuri anisaidie ktk hili!
 
Mwalimu huyo apewe zawadi kubwa kwa kazi nzuri
Ukitaka kupata taswira ya Tanzania ya kesho njoo JF, kwa hali ya shule ilivyo, idadi ya madarasa, idadi ya wanafunzi, idadi ya walimu hata kama tunatofautiana uwezo wa kufikiri sikutegemea mtu akakurupuka na pongezi kwa mwalimu, angalau hata ungeuliza hivi shule hii imesajiliwa kweli? Kwa uchangiaji huu tutafika kweli?
 
Hivi wizara husika imesajili kibanda hiki ambacho hakiko zaidi ya kilomita 60 toka ofisini kwa kama shule,najiuliza walikuwa wanaasomaje wakati wa masika,na wazazi wa watoto hao nyumba zao ziko hivi.
Kwa kutumia udongo huohuo walishindwa kutengeneza vyumba imara,wakati wanasubiri serikali yao sikivu inayoongozwa na mtoto wao kuwajengea majengo ya kudumu.
Lakini sishangai hata ukienda Lugoba kwenyewe alikosomea mweshimiwa huwezi amini.
Je kama shule yenyewe inaonekana hivyo choo chao kikoje au mambo yote yanaishia vichakani,ama kweli Tanzania ni moja ya maajabu ya dunia.
 
Nina imanI kati ya wanafunzi waoliofaulu 50% wamepitishwa tu, rejea matekeo ya mwanafunzi alifaulu wakati hakufanya mtihani.....haya matokeo yapo kisiasa zaidi kuliko utalaamu.!!

Yaani inaelekea haya matokeo yana walakini mkubwa. Tusubiri wiki ijayo tutaona mengi maana mikoa mbalimbali itaonesha miujiza ya shule kama hizo na wanafunzi waliofaulu wakati hawajafanya mtihani.
 
Hakuna cha kufaulu hapo, mwalimu alichofanya (kwa maelezo yake mwenyewe) ni kuhakikisha wanafunzi wanajua kusoma na kuandika. Unless mtihani wa darasa la saba ulikuwa ni kusoma na kuandika tu sioni namna mwanafunzi aliesoma katika mazingira hayo akifaulu kiingereza,hesabu au jiografia. Hao wamefaulishwa tu.
 
Kama ndani ya habari hii hakuna propaganda basi haraka sana naitaka serikali iifunge shule hii. Ilikuwaje shule yenye darasa moja la majani, wanafunzi hawajawahi ona kitabu cha kujisomea, mwal. Mmoja ambae anaishi kwenye gofu kwa miaka saba ikaruhusiwa kuitwa shule? Kwanini watendaji wa elimu wilaya wasifukuzwe wote? Waziri vipi?
 


Sasa mwashangaa nini! hivi ni vitu vya kawaida tu; shuhudieni na hapa;

shule-1.jpg


Madarasa mawili kwa wakati moja chini ya mti!
Ushishangae ukiambiwa hii shule imeshika nafasi ya kwanza kiwilaya/kimkoa!
Naam, ndiyo Tanzania ya CCM...majanga matupu!
 
Back
Top Bottom