Shule nzuri ya primary hapa Dar na hasa Kinondoni kwa vigezo hivi.

mzeemzima

Senior Member
Apr 14, 2010
122
78
Wadau ,

Naomba kujuzwa shule nzuri ya primary kwa hapa Dar na hasa wilaya ya Kinondoni. Na ninaposema nzuri kwangu namaanisha vitu hivi hapa,

1. Mahali ambapo elimu inayotolewa inampa mtoto practical hands on experience ya vitu anavyosoma

2. creativity and thinking is praised over cramming and passing exams. Sio kwamba kuwaza kufaulu mitihani ni vibaya lakini wengi wetu ni mashahidi elimu yetu kwa sehemu kubwa ni kuwaza tu kufaulu mitihani, elimu ambayo dunia sehemu nyingine wameshaachana nayo na wengine wanaiacha kwa kasi.

3. Mazingira ya elimu yanayojenga msingi wa neno la Mungu na maadili mapema toka darasa la kwanza kupitia mafunzo ya Biblia katika masomo.


Nashukuru kwa msaada wenu
 
Back
Top Bottom