Shule ndiyo humpa Dr Slaa kura nyingi katika mitandao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shule ndiyo humpa Dr Slaa kura nyingi katika mitandao

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Zak Malang, Sep 23, 2010.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Sep 23, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Mimi nawashangaa wale wote wanaoziponda kura nyingi anazopata Dr Slaa katika kura za maoni kupitia mitandao – mfano Daily News, Mwanahalisi na hata humu JF. Jibu ni rahisi – shule.

  Wanaompa Dr Slaa kura hizo ni watu ambao angalau wamekwenda shule, wanaweza kuchambua mambo wao wenyewe bila kuburuzwa na wanaweza kutumia Internet. Hawa ni watu ambao tunaweza kusema linaanza kuliimarisha lile tabaka la jamii la Kati (middle Class) la wasomi, wenye kipato cha wastani, na ni tabaka ambalo hupiga kura kutokana na maamuzi ya vichwa vyao, na si miyoyo yao (voting from the head and not from the heart).

  Watanzania wengi bado ni mambumbumbu – watu wa kuburuzwa tu – na ukichanganya na umasikini wao, basi hufanywa kuwa vuno kubwa la CCM wakati wa uchaguzi.

  Wewe angalia tu maeneo ambayo tabaka hili linapatikana na uone nguvu ya Dr Slaa huko: Kilimanjaro, Arusha, Kagera Dsm, na maeneo ya ukanda wa ziwa.


  Kwingineko ni uburuzaji tu – fulana, T-Shirt, Sh elfu tano tano etc ndiyo hufanya kazi zaidi kuliko proper reasoning ya kutoka vichwani.


  CCM inaliogopa sana taabaka hili, kwani likizidi kukua litaitokomeza CCM na hivyo uburuzaji wa watu kama makondoo utakwisha.
   
 2. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #2
  Sep 23, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280


  Watanzania wengi bado ni mambumbumbu – watu wa kuburuzwa tu – na ukichanganya na umasikini wao, basi hufanywa kuwa vuno kubwa la CCM wakati wa uchaguzi.
   
 3. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #3
  Sep 23, 2010
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,079
  Likes Received: 4,022
  Trophy Points: 280
  umesahau Mbeya na Iringa kaka
   
 4. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #4
  Sep 23, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kunradhi -- Mbeya na Iringa pia.
   
 5. m

  muafaka Senior Member

  #5
  Sep 23, 2010
  Joined: Oct 30, 2009
  Messages: 102
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Bado ni tatizo la matabaka Mh. Wasomi, Matajiri, Born-towns how many of us belongs to non of the forementioned groups 80+%, angalia ni watu wangapi wana access ya internet na wapi!. You will be suprised to see that ni walewale wanaolipwa na vyama vyao kufanya contribution katika mitandao na sisi tulio vijijini hata kutuma SMS ni budget issue na wakati mwingine hatuna hata interest ya kushiriki katika opinion poll and remember that is just AN OPINION POLL just like KIPIMA JOTO CHA ITV hah! hah!
   
 6. m

  mwita ke mwita JF-Expert Member

  #6
  Sep 23, 2010
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 5,499
  Likes Received: 1,226
  Trophy Points: 280
  mkoa wa mara shule na msimamo
   
 7. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #7
  Sep 24, 2010
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Bado ni tatizo la matabaka Mh. Wasomi, Matajiri, Born-towns how many of us belongs to non of the forementioned groups 80+%, angalia ni watu wangapi wana access ya internet na wapi!. You will be suprised to see that ni walewale wanaolipwa na vyama vyao kufanya contribution katika mitandao na sisi tulio vijijini hata kutuma SMS ni budget issue na wakati mwingine hatuna hata interest ya kushiriki katika opinion poll and remember that is just AN OPINION POLL just like KIPIMA JOTO CHA ITV hah! hah!
  HAPO KAKA KWENYE RED UMEANDIKA KWA KUFUATA MOYO NA SIO BRAIN
   
 8. Hassani

  Hassani JF-Expert Member

  #8
  Sep 24, 2010
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 267
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 45
  Kinachoonekana kwenye mitandao ni reflection ya maoni ya watanzania wengi tu,wengi hatuna imani na serikali iliyoko madarakani,ila hatuna pa kusemea.Wengi wetu tunaoandika kwenye mitandao tunafanya hivyo sababu hatuonekani,hivyo kuponya ajira zetu(kwa wafanyakazi wa serikali na makampuni ambayo wamiliki wake ni wanaccm),so tuna sehem ya kumwaga machungu.Na hakika kama kila mtanzania angekuwa ana uwezo wa kuwa na access na jf kama sisi wachache ungeona "moto".Ndo tunarudi kwenye point ya muanzisha thread "Elimu".
   
Loading...