Shule moja tumerudishiwa, tunaendelea kudai shule zilizobaki, viwanja vya michezo, na majumba yetu

REAGAN C.MABOGO

JF-Expert Member
Jan 3, 2014
1,266
2,000
Sifa na utukufu vidumu daima kwa rais wetu mwema. Najua kila mtu anajua kwamba tangu vyama vingi vianze, CCM imeendelea kujimilikisha shule za umma maarufu kama shule za wazazi.!

CCM pia ikajimilikisha viwanja vya michezo kama kirumba, al hassan mwinyi, amri abeid, majimaji, nk. Si hivyo tu, CCM pia ikang'ang'ania na inaendelea kukalia majengo mbalimbali ya umma kama chimwaga na lile la pale kati Dodoma, la umoja wa vijana pale barabara ya Morogoro Dar es salaam, lumumba pia Dar es salaam, Mwanza, nk. Wakati wote tangu kuanza vyama vingi, sisi wananchi wazalendo tumekuwa tukidai mali hizo za umma turudishiwe.

Lakini CCM (chama dola) na serikali wamejifanya hawasikii. Napenda kuutumia uhai wangu kumkumbusha mwenyekiti wa CCM, mtukufu rais wetu mwema, kuwa, tunataka aturudishie shule zetu hizo zote, viwanja vyetu hivyo vyote, na majumba yetu hayo yote yanayokaliwa na CCM. Natanguliza ahsante. Sifa na utukufu zidumu daima kwa rais wetu mwema.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom