Shule kumi ghali Tanzania

Ni Sawa nakubaliana na wewe hazikuwa lakini maisha yana Siri kubwa sana mkuu!!! Mungu niwaajabu sana sometimes.... Matajiri hata izi shule hawajasoma lakini ndo wanawapeleka watoto huko kusom nikuondoa ujinga tu kichwani lakini kama unataka mtoto awe na Mali mfundishe kutafuta pesa tangu mdogo asikae kae om kama una biashara nenda nae ajifunze huko!!!! Na ako kaelimu kake atakakopata maisha hayawezi kumshinda
Hao watoto wanasomeshwa waendeshe international companies. Au wanaendesha local companies with international exposure and connection.

Bakhresa amewapeleka watoto wake huko sahivi ndo wasimamizi wakuu wa makampuni yake. Yeye amekaa pembeni, unadhani hizo kampuni zitayumba?

Hata huyo mtoto ataanzisha kampuni leo, ndani ya miaka mitano yupo mbali kuliko huyo wako atakaekuwa anasimamia duka kkoo.

Wahindi, wazungu, waarabu wanatuzidi kwenye exposure and connection. Anzisha biashara leo na yeye aanzishe yake, 5 years atakuwa na revenue 10 times yako. Unadhani kwanini?
 
Hebu tupasheni ni Faida wanazoleta kwa Taifa hili baada ya Kupita huko internationally
 
Unaweza kukuta kuna watoto wa watumishi wa umma wa nchi hii wanasoma hizi shule!
 
International school - English ya puani = Kayumba

Nimefanya kazi na ninafanya kazi na baadhi ya waliosoma hizo shule. Thinking process yao bado ile ile tu kama ya watoto wengine wa kayumba

Kikubwa hizi shule zimewafundisha wawe na culture ya wazungu tu basi. Nothing more nothing less.
 
Anayemaliza hapo anatakiwa akasome vyuo vya huko mbali; akisoma vyuo vya hapa nchini ni matumizi mabaya ya fedha. Na wengi wao huwa hawaajiriwi zaidi ya kuendeleza makampuni walioachiwa na familia au kuanzisha kampuni mpya.
 
Milioni 70 ada tu kwa mwaka kwa miaka Sita hadi form Six na matumizi mengine ni wastani wa kalibu Tsh. milioni Mia Tano.
Ukichukua na ghalama za Shule ya Chekechea miaka 2 na Msingi miaka 7 inakaribia Tsh Billioni moja
 
Wenyewe wa aina tatu: (a) wapigaji kwenye eneo lolote lile, (b) wanaosomeshewa watoto wao na waajiri wao, (c) wafanyabiashara wakubwa wasiokwepa kodi na walianzisha biashara zao kihalali, kinyume na haya ni wapigaji!
Usiwasahau wenye salary zao kuna raia anakunja 30 million Tzs kila mwezi ada milioni 10 kitu gani
 
Wacha vijana wasome tupate ma pilot na ma Air hostesses wanaobonga ungenge kupitia puani kuna rubani mmoja ni masai akiwa kwenye cruising au anakaribia kushusha pipa utasikia “Flight attendants prepare for landing please.” ila sasa unatambua tu hii ni spishi ya IST maana neno utalosikia ni landing tu...shule duni haitamsaidia mwanao...hushangai kwanini amehushuria saili 40 hajawa hata shortlisted!? Tatizo ni quality!

Tusomeshe watoto shule nzuri tuache kuponda waje wafanye noble jobs.

Sio toto linamaliza University hata past participle tense halijui hafu linakuja jf kuponda au mzazi sababu ya ukata ufuta anakuja kuponda wenzie wenye hela. UMASKINI SAWA NA UCHAWI. TUTAFUTE HELA.
 
Mimi nasema hivi kama una maono makubwa na vijana wako ya kimaisha wasome kayumba wasome Harvard wasome IST haijalishi vijana lazima wapate spirit ya kupambana na kujifunza maisha yao yote.Wapo watu tangu wamalize degree zao wanachosomaga ni magazeti tu labda na JF au Instagram hukuti hata ana kitabu hizo exposure atazipata vipi.Binafsi nimeona watu wengi wakipata exposure tena ile positive kwa ku explore tu vitabu na pages mbalimbali ambazo ni constructive.Tena wengi wameishia form 4 au 6 so kama vijana wako wapo private au kayumba don't worry even YouTube is best to all those universities and those international school.Refer Elon musk yeye hata ku recruit staffs wake haangaliii degree anachoangalia ni creativity and growth spirit.Refer pia marehemu Ruge wa clouds kawaibua vijana wengi na wana maisha kwa kuwaangalia uwezo wao na kuwaaminisha Kuwa wanaweza wakijinoa zao.Dunia ya Leo inataka skills set zaidi kuliko ma degree.Na skills nyingi hupatikana bure cha msingi kijana awe na msingi mzuri tu ambapo hata kayumba msingi mzuri anaupata kwa sababu hapo kinachohitajika ni learning enthusiasm and growth spirit tu.

Sent from my SM-J610F using JamiiForums mobile app
 
Elimu ya sasa ni biashara, na ukiteleza na kuingia kwenye huo mtego, utajikuta unatumia gharama kubwa kwa kitu cha kawaida. Jiulize hawa maprofesa tulionao, walisoma huko? Ni sawa na duka A ununue mirinda kwa 500 huku duka B mirinda hiyo hiyo inauzwa 10,000. Kule watakachotofautiana zaidi ni lugha tu, lakini haina maana akisoma kule kuna uhakika wa kuja kuwa Director wa IMF/ world bank.
 
Japo sio guaranteed kusoma shule za bei juu na kufanikiwa kimaisha, ila ipo tofauti kubwa sana ya mwanafunzi wa shule ya msingi Keko na Breaburn international

Shule za kishua wanafundishwa kua na confidence ya hali ya juu, anaweza kusimama mbele ya mtu au watu popote pale duniani na akamwaga 'upupu' na huyo ni mtoto wa miaka 8 tu. Sasa mtoto wa Keko primary zaidi ya kucheza singeli hadharani, ukimuuliza swali lolote technical tena mbele ya watu, utasikilizia muziki wake.

All in all the word is not fair wapo wasindikizaji na wapo wanaoishi, ni vema kua na amani ya moyo tu.
 
Hao watoto wanasomeshwa waendeshe international companies. Au wanaendesha local companies with international exposure and connection.

Bakhresa amewapeleka watoto wake huko sahivi ndo wasimamizi wakuu wa makampuni yake. Yeye amekaa pembeni, unadhani hizo kampuni zitayumba?

Hata huyo mtoto ataanzisha kampuni leo, ndani ya miaka mitano yupo mbali kuliko huyo wako atakaekuwa anasimamia duka kkoo.

Wahindi, wazungu, waarabu wanatuzidi kwenye exposure and connection. Anzisha biashara leo na yeye aanzishe yake, 5 years atakuwa na revenue 10 times yako. Unadhani kwanini?

Kama ndo unachoamini sawa mkuu!! Ila acha kumleta bakhresa hapa aisee wewe baba ako anamzidi nini uyo bakhresa? Utajiri mwingine una historia mkuu kwaiyo wewe unaamini watoto wa bakhresa ndo wamefanya makampuni yao yafike hapo yalipo?

Kwann umewaza duka kkoo huo ndo mwisho wako wakufikiri umewaza duka tu mzee?

Watoto wa bakhresa akili zao kama za kibongo tu sema wamekuta tayari Mali ipo kwaiyo ni rahisi wao kufika mbali kwasababu pesa ipo, yusuph anasimamia kampuni yakupiga rangi magari, ujenzi wa apartment, na mahotel yao sasa wewe unaisi pesa ni zake yeye?

Nimesema nitawajengea manyumba yakisasa ma apartment yakutosha na za kisasa, nitawanunulia mashamba makubwa nakuanzisha kilimo wauze izo mazao itawasaidia, sasa wao kutaka watajirike zaidi waweke na izo elimu zao kwa icho nilichowaachia waboreshe watakavyo vikuta watakuwa na pesa tu..... mpango ni pesa mkuu wangu kila anaesomesha anataka mwanae awe na pesa mkuu, sio sijui Wazungu wakujue alafu ndo inakuwa nn mtoto anafanya kazi ulaya lakini hela hana ni ujiko tu wakijinga kuwa upo ulaya....

Huku unatafuta pesa uko ulaya unaenda kuzurura tu kushangaa unarudi maisha yanaendelea” izo mambo unaniambia sikubaliani na wewe milioni izo silipi sina na hata nikiwa nazo bado silipi nitawawekea mambo yao ya badae yawe mazuri
 
Back
Top Bottom