Shule ipi nzuri kwa A level kwa ajili ya kijana wangu mwakani hususani za Serikali?

Mhigwa one

Member
Nov 5, 2016
60
46
Wadau naomba kujua shule nzuri kitaaluma hasa masomo ya sayansi na iwe ya serikali ili nipunguze makali ya ada nilizotumia o level! Tafadhari mchango.
 
Hakuna Shule inayoweza kuongeza akili ya mwanao. Hakikisha mwanao anauwezo wa akili, ari na shauku ya kujifunza, halafu mpeleke Shule yoyote ya A-level. Baada ya mtihami linganisha na ufaulu wa wengine.
 
Kama asipoenda special schools

Basi zifuatazo ndo zinamfaa zipo kaskazini mwa Tanzania mkoa wa Kilimanjaro

Kwa shule za wavulana mpeleke
Lyamungo, Umbwe au Old Moshi

Kama ni msichana mpeleke

Ashira, Mawenzi au Machame girls
 
Wadau naomba kujua shule nzuri kitaaluma hasa masomo ya sayansi na iwe ya serikali ili nipunguze makali ya ada nilizotumia o level! Tafadhari mchango.
Mwambie aende Mzumbe, Kibaha, Ilboru au Tabora Boys kama ni kidume kweli. Ukisoma ktk shule hizo unakuwa tofauti na hakuna spoon feeding. Mojawapo ya hizo skul Motto Yao ni "KULA KWA BIDII, KUSOMA KWA BIDII NA KUCHEZA KWA BIDII" halafu wanamalizia "USE YOUR COMMON SENSE"
 
Asanteni sana, nimegundua nilikosea kwenye ombi langu kwani sikua specific kuwa sio shule ya serikali kwani sina uwezo wakumuingiza shule ya serikali, hivyo ningepata kujuzwa shule za binafsi ingefaa zaidi. Shukrani
 
Mwambie aende Mzumbe, Kibaha, Ilboru au Tabora Boys kama ni kidume kweli. Ukisoma ktk shule hizo unakuwa tofauti na hakuna spoon feeding. Mojawapo ya hizo skul Motto Yao ni "KULA KWA BIDII, KUSOMA KWA BIDII NA KUCHEZA KWA BIDII" halafu wanamalizia "USE YOUR COMMON SENSE"

Sio yenye motto THE HEAD OF TANZANIA hahaaa umenikumbusha siku wamekimbiza dishi la wali form five wazima
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom