mwananchit
JF-Expert Member
- Oct 13, 2008
- 242
- 296
Imekuwa ni kawaida kwa watoto wanasoma Shule za Binafsi kuwabebesha watoto mafurushi ya kazi za kufanya wakiwa likizo almaarufu Kama HOLIDAY PACKAGES na wakati mwingine watoto wanaendelea kwenda shuleni wakati wa likizo kwa kile kinachoitwa HOLIDAY COACHING. Sasa hizi ni likizo?
Likizo zingeachwa huru ili watoto wawe huru kuwasaidia wazazi wao kazi za nyumbani au kusafiri kwenda kuwasalimia bibi zao huko vijijini ili wafahamu asili yao na pia kujumuika na ndugu zao wengine.
Tungeomba Serikali ilitazame hili jambo na ikiwezekana itoe mwongozo kuhusiana na jili jambo. Tusiwafanye watoto wetu kuwa kama ndondocha, kuna maarifa mengine ambayo watoto wanayahitaji zaidi ya hesabu, fizikia na jiorafia.
Naomba kuwasilisha.