Shule Binafsi za Sekondari zipo hoi

Kuna ka ukweli hapa.
Hali hii imetokana na wanafunzi wanaopata mikopo ya elimu ya juu ni wale waliosoma shule za Serikali, Pia ukata mkali huku mtaani nao unachangia wazazi kuwaacha watoto wao wasome shule za kata.
Mkuu kama unawaza kumsomesha kijana wako shule ya serikali ili akifika chuo kikuu apate mkopo.NAKUHURUMIA SANA
 
Kikubwa unakubaliana na mimi kwamba upepo sasa hivi unavuma. Hivyo niko sahihi.

Wewe ni mwalimu bila shaka. Kikubwa fanya kazi kwa bidii utabiri wako hautotimia. Matajiri huwa wanaenda na upepo, hivyo inawezekana muda huu upepo unaovuma sio mzuri lakini punde tu upepo ukapungua kasi ukawa upepo mzuri unao safirisha majahazi.
 
Nimekwambia zitabaki za kanisa tu. Jitegemee ni ya Jeshi, St. Francis ni ya kanisa kama nilivyosema.

Upo wapi wewe? Weka idadi katika shule hizo na majina yao!!

Jaribu kutembelea Jitegemee na St Francis utuwekee idadi ya mwanafunzi.
 
Umelogwa na kichaa juu, rudia? Taja zilizofungwa kwa kukosa wanafunzi.

Hata kama ni hivyo, sababu ni IPI? Watu hawana hela kwa sababu ya mismanagement of economy by this regime.
Mis-management of the economy? Kweli wewe unajua sana mambo ya uchumi wa Facebook.
 
sasa hapo umekubaliana nae au umepingana nae!?
yeye point yake ilikuwa by necessary implication, eti za serikali zinafanya vema hivyo watu wanawapeleka watoto kule..... hilo ndilo nalikataa...... Lumumba wanasema hivyo, wanajenga hoj hiyo
 
Nyingi Sana labda wewe Kama uko nje ya nchi. Mfano kifai sec school kiluvya, perfect vision ubungo, mzinga sec banana, abc capital kinyerezi, right wing majumba sita n.k zote zimefungwa chini ya dictator magufuli
Ila nazo duh! Huwezi kuzilinganisha na St. XXX hizo bado zinafurika.
 
Shule za private chache Sana zinazosurvive na ambazo zpo well organised....nyingi zinapumulia mashine , walimu wanakopwa mwanzo mwisho, kuacha hawawez mana wakija huku hata hcho watakosa mana jiwe kafunga .lango la Ajira
Sijui unazungumzia shule zipi, hapa Moro ukienda pale St Ann's kuuliza nafasi za kindergarten zimejaa tokea Disemba, std one ndiyo wala usiseme..
 
..vyuma vimekaza ppl can not afford private schools anymore.

..watu wanatoa watoto private schools wanawahamishia govt' schools kwenye elimu bure.
 
Sijui unazungumzia shule zipi, hapa Moro ukienda pale St Ann's kuuliza nafasi za kindergarten zimejaa tokea Disemba, std one ndiyo wala usiseme..
Nazungumzia sekondary mkuu, serikal haina kindergarten thus why
 
Mambo yamebadilika. Miaka sita iliyopita watu walikuwa wanazikimbia shule za serikali wanagombania shule za private.

Hali imekuwa kinyume miaka hii na hasa mwaka huu. Sasa shule za serikali zimefurika wanafunzi wakati sekondari za private zina wanafunzi kiduchu.

Ukizingatia kwamba sekondari za private zina wawekezaji wababaishaji yaani hawaja invest wanategemea mapato kutoka kwenye ada ya wanafunzi.

Sasa kama una wanafunzi hawazidi 20 darasani maana yake hiyo shule inasuasua hata kama wanafunzi wanalipa ada kwa wakati.

Sasa huwa hawalipi kwa wakati na hivyo kuongeza tatizo.

Matokeo yake shule haziendesheki na hata kulipa mishahara walimu ni tabu tupu.

Matokeo yake ni kufeli wanafunzi na shule kukosa mvuto kabisa.

Hali ikiendelea hivi miaka miwli ijayo basi private secondary schools zitafungwa na zitabaki za kanisa tu.
Waambie wenye Shule binafsi kuwa Kutesa kwa zamu!
 
Back
Top Bottom