Shule binafsi mwanafunzi anafundishwa mbinu za kufaulu mtihani na sio kupata elimu itakayompa maarifa

Hata za serikali wanafundisha kufaulu ili wapate sifa. Mwaka jana si umesikia wilaya moja yote huko Dodoma wameibamtihani chini ya maafisa elimu na wilaya yote wakaifutia matokeo?
 
Tatizo kubwa lipo kwenye mfumo mzima wa Elimu Tanzania maana mitaala inayotumika ni moja na wote mwisho wanafanya mitihani sawa,Hili eneo la elimu linatakiwa kufanywa mjadala mkuu wa serikali maana kuna madudu chungu nzima na serikali ya awamu hii kama inaegemea upande mmoja na haitaki ile tunasema ushirikishwaji wa wazazi ktk maendeleo ya mtoto shuleni
 
Ukiangalia matokeo ya kidato cha nne na sita ni ukweli usiopingika wanafaulu sana, lakin ukiangalia shule binafsi nyingi wanafunzi wanafundishwa mbinu za kufaulu mtihani na sio kuelewa mazingira yaliyomzunguka.

Kwenye hizo shule msisitizo ni kufaulu Kwa sababu elimu ni biashara, matokeo yake huyo mwanafunzi akienda chuo akimaliza anakua hana uwezo sana Kwa sababu msingi wake alikuwa anapewa mbinu za kufaulu na sio kuelewa.

Ndo maana wanafunzi wengi wa kileo wanavyeti vizuri sana lakini vichwani hamna kitu, hawana maarifa.
Mtaanza kunielewa taratibu nnaposema shule za kusomea ujinga.
 
Je ulichukua wa shule ya serikali na kumuuliza maswali hayo akapata?kuwa sehemu ya elimu atakayopata mtoto wako wala usilaumu pale unapotimiza wajibu wako
Mtoto tu alikuwa ndezi. Alichukua wengine wa shule binafsi na kuwauliza swali hilo hilo?
 
Nakubaliana na wewe asilimia mia, nimeliona hilo nimesomesha shule binafsi wanangu 3 na wanawasisitizia kufaulu mitihani sio kuelewa.

Nina binti yangu yuko darasa la 7 na katika mitihani yake anafanya vizuri hata hisabati anapataga A,
sasa hapa nyumbani nimechimba kisima kirefu mita 10 na upana mita 4.

Nikamuuliza maswali yafuatao:
Hiki kisima kina mita za ujazo ngapi? Je zitaingia ndoo kubwa za hapa nyumbani ngapi? Je kama kwasiku tunatumia pipa la ndoo 20 kumi, likijaa tutayatumia kwa siku ngapi?

Kama haya maji kwamfano tutayatumia kwa siku 200 kwa mwaka je kuna siku tutanunua maji?
Haya maswali yote darasani walishafundishwa ila kuhamisha alichofundishwa darasa na kukipeleka katika maisha ni sifuri kabisa kabisa.

Alivyoshindwa nikamwambia akamlete mwanafunzi darasani kwao ambaye anaongoza kwa hesabu, baada ya siku 2 akaja nyumbani nikamuuliza maswali yale yale kachemka.

Nikawapa viidokezo: katika maumbo mliyofundishwa hiki kisima ni umbo gani? ndo wakafumbuka macho na kusema ni CYLINDER! Wakafanya wakapata yote isipokuwa la mwisho nililouliza kama maji ya kisima yatatumika kwa siku 200 kwa mwaka je tutanununua maji? Wakasema ndio, Wakakosa jibu ni hapana kamwe hatutanunua maji kwasababu siku 200 ni kama miezi saba ambapo kabla haijaisha mvua itakuwa imenyesha na kujaza tena kisima tuna mvua za vuli, masika, n.k
.
Kwahiyo, hizi shule za binafsi wanatafuta hela tu na sio kuwapa watoto wetu maarifa. Wanakuwa wamefaulu mitihani sana hadi chuo lakini wakimaliza ndo wa kwanza kuitukana serikali iwaari.
Kumbe moderator wa hapa JamiiForums wanahack account za wajumbe. Mchangiaji #2 sio Mimi. Original ni jinsi alivyoniquote mchangiaji #3 'Uhurumoja". Haya mambo ya kuhack account za members na kubadilisha ujumbe ni uhalifu kama uhalifu mwingine!
 
Na yumkini hakuwa ndezi ila tu kwenye hili hakujua alipaswa kumuelekeza vizuri.ni muhimu kumshika mtu mkono bila kumkosoa na kumdharau kama alivyofanya
Mtoto tu alikuwa ndezi. Alichukua wengine wa shule binafsi na kuwauliza swali hilo hilo?
 
Ukiangalia matokeo ya kidato cha nne na sita ni ukweli usiopingika wanafaulu sana, lakin ukiangalia shule binafsi nyingi wanafunzi wanafundishwa mbinu za kufaulu mtihani na sio kuelewa mazingira yaliyomzunguka.

Kwenye hizo shule msisitizo ni kufaulu Kwa sababu elimu ni biashara, matokeo yake huyo mwanafunzi akienda chuo akimaliza anakua hana uwezo sana Kwa sababu msingi wake alikuwa anapewa mbinu za kufaulu na sio kuelewa.

Ndo maana wanafunzi wengi wa kileo wanavyeti vizuri sana lakini vichwani hamna kitu, hawana maarifa.
Sio shule binafsi tu ni elimu ya Tanzania kwa kiwango kikubwa kuanzia primary mpaka vyuoni,kunahitajika mabadiliko makubwa sana kwenye hili swala,unakuta mtu anasoma madaftari tu vitabu anavitumia kwa ajili ya michoro sasa hapo kuna kitu kweli...?
 
Kuna matatizo mengine zaidi ya unachosema kunahitajika research kwa kuwa iwe iwavyo ili ufaulu lazima ujue mbinu za kujibu ili ufaulu na utashindwaje kuelewa quadratic equation endapo umejibu swali LA quadratic na umelipata kwa usahihi bila msaada?au mtoa mada unamaanisha nini
 
Ukiangalia matokeo ya kidato cha nne na sita ni ukweli usiopingika wanafaulu sana, lakin ukiangalia shule binafsi nyingi wanafunzi wanafundishwa mbinu za kufaulu mtihani na sio kuelewa mazingira yaliyomzunguka.

Kwenye hizo shule msisitizo ni kufaulu Kwa sababu elimu ni biashara, matokeo yake huyo mwanafunzi akienda chuo akimaliza anakua hana uwezo sana Kwa sababu msingi wake alikuwa anapewa mbinu za kufaulu na sio kuelewa.

Ndo maana wanafunzi wengi wa kileo wanavyeti vizuri sana lakini vichwani hamna kitu, hawana maarifa.
Mkuu kidato cha sita shule za private hupigwa na shule za serikali.
 
Ukiangalia matokeo ya kidato cha nne na sita ni ukweli usiopingika wanafaulu sana, lakin ukiangalia shule binafsi nyingi wanafunzi wanafundishwa mbinu za kufaulu mtihani na sio kuelewa mazingira yaliyomzunguka.

Kwenye hizo shule msisitizo ni kufaulu Kwa sababu elimu ni biashara, matokeo yake huyo mwanafunzi akienda chuo akimaliza anakua hana uwezo sana Kwa sababu msingi wake alikuwa anapewa mbinu za kufaulu na sio kuelewa.

Ndo maana wanafunzi wengi wa kileo wanavyeti vizuri sana lakini vichwani hamna kitu, hawana maarifa.
Sio kweli.

Wanaofundishwa namna ya kufaulu ni hao wanafunzi wa serikalini ambao wanaishinda kwenye vibanda kusoma tuition na huko hakuna elimu bora zaidi ya kufundishwa njia za mkato ili wafaulu mfano kufoji practicals .
 
Njia wanayotumia wanafunzi wa kata mtaani, private school wanafundishwa darasani
 
Back
Top Bottom