Shule binafsi mwanafunzi anafundishwa mbinu za kufaulu mtihani na sio kupata elimu itakayompa maarifa

dennis_robert

dennis_robert

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2019
Messages
310
Points
500
dennis_robert

dennis_robert

JF-Expert Member
Joined Mar 7, 2019
310 500
Ukiangalia matokeo ya kidato cha nne na sita ni ukweli usiopingika wanafaulu sana, lakin ukiangalia shule binafsi nyingi wanafunzi wanafundishwa mbinu za kufaulu mtihani na sio kuelewa mazingira yaliyomzunguka.

Kwenye hizo shule msisitizo ni kufaulu Kwa sababu elimu ni biashara, matokeo yake huyo mwanafunzi akienda chuo akimaliza anakua hana uwezo sana Kwa sababu msingi wake alikuwa anapewa mbinu za kufaulu na sio kuelewa.

Ndo maana wanafunzi wengi wa kileo wanavyeti vizuri sana lakini vichwani hamna kitu, hawana maarifa.
 
No retreat no surrender

No retreat no surrender

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2018
Messages
368
Points
500
No retreat no surrender

No retreat no surrender

JF-Expert Member
Joined Apr 21, 2018
368 500
Nakubaliana na wewe asilimia mia, nimeliona hilo nimesomesha shule binafsi wanangu 3 na wanawasisitizia kufaulu mitihani sio kuelewa.

Nina binti yangu yuko darasa la 7 na katika mitihani yake anafanya vizuri hata hisabati anapataga A,
sasa hapa nyumbani nimechimba kisima kirefu mita 10 na upana mita 4.

Nikamuuliza maswali yafuatao:
Hiki kisima kina mita za ujazo ngapi? Je zitaingia ndoo kubwa za hapa nyumbani ngapi? Je kama kwasiku tunatumia pipa la ndoo 20 kumi, likijaa tutayatumia kwa siku ngapi?

Kama haya maji kwamfano tutayatumia kwa siku 200 kwa mwaka je kuna siku tutanunua maji?
Haya maswali yote darasani walishafundishwa ila kuhamisha alichofundishwa darasa na kukipeleka katika maisha ni sifuri kabisa kabisa.

Alivyoshindwa nikamwambia akamlete mwanafunzi darasani kwao ambaye anaongoza kwa hesabu, baada ya siku 2 akaja nyumbani nikamuuliza maswali yale yale kachemka.

Nikawapa viidokezo: katika maumbo mliyofundishwa hiki kisima ni umbo gani? ndo wakafumbuka macho na kusema ni CYLINDER! Wakafanya wakapata yote isipokuwa la mwisho nililouliza kama maji ya kisima yatatumika kwa siku 200 kwa mwaka je tutanununua maji? Wakasema ndio, Wakakosa jibu ni hapana kamwe hatutanunua maji kwasababu siku 200 ni kama miezi saba ambapo kabla haijaisha mvua itakuwa imenyesha na kujaza tena kisima tuna mvua za vuli, masika, n.k
.
Kwahiyo, hizi shule za binafsi wanatafuta hela tu na sio kuwapa watoto wetu maarifa. Wanakuwa wamefaulu mitihani sana hadi chuo lakini wakimaliza ndo wa kwanza kuitukana serikali iwaajili
 
uhurumoja

uhurumoja

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2014
Messages
2,120
Points
2,000
uhurumoja

uhurumoja

JF-Expert Member
Joined Mar 2, 2014
2,120 2,000
Nakubaliana na wewe %100. Nimesomesha shule binafsi wanangu 3 nimeliona hilo. Wanawasisitizia kufahulu mtihani sio kuelewa.
Kwamfano. Nina binti yangu yuko Grade 7 na katika mitihani yake anafanya vizuri hata Hisabati anapataga A.
Sasa hapa nyumbani nimechimba kisima kirefu mita 10 na upana mita 4. Nikamuuliza maswali yafuatao:
Hiki kisima kina ujazo cubic mita ngapi? Je zitaingia ndoo kubwa za hapa nyumbani ngapi? Je kama kwasiku tunatumia pipa la ndoo 20 kumi, likijaa tutayatumia kwa siku ngapi?
Kama haya maji kwamfano tutayatumia kwa siku 200 kwa mwaka je kuna siku tutanunua maji?
Haya maswali yote darasani walishafundishwa ila kuhamisha alichofundishwa darasa na kukipeleka katika maisha ni ZERO kabisa.
Alivyoshindwa nikamwambia akamlete mwanafunzi darasani kwao ambaye anaongoza kwa hesabu. Baada ya siku 2 akaja nyumbani nikamuuliza maswali yale yale kachemka.
Nikawapa hint: katika maumbo mliyofundishwa hiki kisima ni umbo gani? Ndo wakafumbuka macho na kusema ni CYLINDER! Wakafanya wakapata yote isipokuwa la mwisho nililouliza kama maji ya kisima yatatumika kwa siku 200 kwa mwaka je tutanununua maji? Wakasema NDIO. Wakakosa jibu ni HAPANA kamwe hatutanunua maji kwasababu siku 200 ni kama miezi saba ambapo kabla haijaisha mvua itakuwa imenyesha na kujaza tena kisima. Tuna mvua za vuli, masika, n.k.
Kwahiyo hizi shule za binafsi wanatafuta hela tu na sio kuwapa wanetu maharifa. Wanakuwa wamefaulu mitihani sana hadi chuo lakini wakimaliza ndo wa kwanza kuitukana serikali iwaajili
Je ulichukua wa shule ya serikali na kumuuliza maswali hayo akapata?kuwa sehemu ya elimu atakayopata mtoto wako wala usilaumu pale unapotimiza wajibu wako
 
M

mangatara

JF-Expert Member
Joined
Jul 6, 2012
Messages
12,930
Points
2,000
M

mangatara

JF-Expert Member
Joined Jul 6, 2012
12,930 2,000
Ukiangalia matokeo ya kidato cha nne na sita ni ukweli usiopingika wanafaulu sana, lakin ukiangalia shule binafsi nyingi wanafunzi wanafundishwa mbinu za kufaulu mtihani na sio kuelewa mazingira yaliyomzunguka.

Kwenye hizo shule msisitizo ni kufaulu Kwa sababu elimu ni biashara, matokeo yake huyo mwanafunzi akienda chuo akimaliza anakua hana uwezo sana Kwa sababu msingi wake alikuwa anapewa mbinu za kufaulu na sio kuelewa.

Ndo maana wanafunzi wengi wa kileo wanavyeti vizuri sana lakini vichwani hamna kitu, hawana maarifa.
Kwa mantiki hiyo shule za kata ndio bora zaidi kwa sababu hazifaulishi bali zinasaidiwa kufaulu ndo maana wanaosoma humo wana maujanja zaidi ya shule binafsi. Nadhani ulizomea kata
 
M

Marwa_J_Merengo

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2018
Messages
2,672
Points
2,000
M

Marwa_J_Merengo

JF-Expert Member
Joined Aug 6, 2018
2,672 2,000
Afadhari hizi shule za binafsi za bongo wanafundisha kupass mitihani kuliko za wakenya wanafundisha kuongea kiingereza
 
kiLimIlire

kiLimIlire

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2012
Messages
252
Points
500
kiLimIlire

kiLimIlire

JF-Expert Member
Joined Apr 8, 2012
252 500
Tatizo ni mfumo wa elimu, maana udhaifu wa private schools sio ubora wa gov.t schools... kote ovyo tu linapokuja suala la application ya knowledge katika maisha halisi
 
dennis_robert

dennis_robert

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2019
Messages
310
Points
500
dennis_robert

dennis_robert

JF-Expert Member
Joined Mar 7, 2019
310 500
Kwa mantiki hiyo shule za kata ndio bora zaidi kwa sababu hazifaulishi bali zinasaidiwa kufaulu ndo maana wanaosoma humo wana maujanja zaidi ya shule binafsi. Nadhani ulizomea kata
Hakuna sehemu ambayo nimeongelea shule za kata, au nimefanya comparison
 
D

delako

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2012
Messages
2,457
Points
2,000
D

delako

JF-Expert Member
Joined Oct 6, 2012
2,457 2,000
Hapo suala sio shule binafsi wala shule za nani hapo ni mtaala wetu wa elimu.
Mwanafunzi anapimwa na mtihani tu na mwisho wa siku akifaulu yeye anaakili na yule akifeli basi hana AKILI.Hats ukienda kuomba kazi wanakuambia tupe vyetu vyako vile vyeti sio vya application ya Yale uliyoyasoma ila ni ufahuli wako katika ngazi mbali mbali ukiwa shuleni
 
Root

Root

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2012
Messages
31,327
Points
2,000
Root

Root

JF-Expert Member
Joined Jan 23, 2012
31,327 2,000
Inabidi iwe hivyo ili waendelee kutawala. Wawafundishe kuhoji si mtaandamana kila siku.
Jiulize why zamani migomo ilikuwepo kuliko siku hizi
 
Bujoro

Bujoro

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2018
Messages
3,053
Points
2,000
Bujoro

Bujoro

JF-Expert Member
Joined Jan 30, 2018
3,053 2,000
We ukitaka wawafundishe kufanya nn kama sio kufaulu?? Ww ulimpeleka shule aferi???
 
Waziri wa Kaskazini

Waziri wa Kaskazini

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2015
Messages
4,680
Points
2,000
Waziri wa Kaskazini

Waziri wa Kaskazini

JF-Expert Member
Joined Dec 12, 2015
4,680 2,000
Kwa mantiki hiyo shule za kata ndio bora zaidi kwa sababu hazifaulishi bali zinasaidiwa kufaulu ndo maana wanaosoma humo wana maujanja zaidi ya shule binafsi. Nadhani ulizomea kata
Mwaka huu ndiyo utabaki mdomo wazi, unaambiwa shule za serikali kidato cha nne mwaka huu watafaulu kwa asilimia 98%, ili hizi ni sifa za kisiasa ili Tanzania ionekane inafanya vizuri kila nyanja kuanzia Elimu, Afya, etc....

Mwanafunzi wa form 4 anapata div 2 Moku halafu hawezi kuandika barua yenye maneno 60 ya kingereza au hawezi kujielezea, ni kama vile wanafunzi watafaulu kwa kubahatisha bahati na sibu....
 
Waziri wa Kaskazini

Waziri wa Kaskazini

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2015
Messages
4,680
Points
2,000
Waziri wa Kaskazini

Waziri wa Kaskazini

JF-Expert Member
Joined Dec 12, 2015
4,680 2,000
We ukitaka wawafundishe kufanya nn kama sio kufaulu?? Ww ulimpeleka shule aferi???
Ni bora mtoto wangu afeli lakini shule atoke na maarifa... Mtoto anafaulu halafu kujieleza hawezi yaani kichwani empty... Ndiyo maana Magufuli hatoi tena ajira anajua bomu lililopo.... Akitoka atatoa ajira ya vichwa mabomu
 
Titicomb

Titicomb

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2012
Messages
5,968
Points
2,000
Titicomb

Titicomb

JF-Expert Member
Joined Jan 27, 2012
5,968 2,000
Nakubaliana na wewe asilimia mia, nimeliona hilo nimesomesha shule binafsi wanangu 3 na wanawasisitizia kufaulu mitihani sio kuelewa. Nina binti yangu yuko darasa la 7 na katika mitihani yake anafanya vizuri hata hisabati anapataga A,
sasa hapa nyumbani nimechimba kisima kirefu mita 10 na upana mita 4. Nikamuuliza maswali yafuatao:
Hiki kisima kina mita za ujazo ngapi? Je zitaingia ndoo kubwa za hapa nyumbani ngapi? Je kama kwasiku tunatumia pipa la ndoo 20 kumi, likijaa tutayatumia kwa siku ngapi?
Kama haya maji kwamfano tutayatumia kwa siku 200 kwa mwaka je kuna siku tutanunua maji?
Haya maswali yote darasani walishafundishwa ila kuhamisha alichofundishwa darasa na kukipeleka katika maisha ni sifuri kabisa kabisa.
Alivyoshindwa nikamwambia akamlete mwanafunzi darasani kwao ambaye anaongoza kwa hesabu, baada ya siku 2 akaja nyumbani nikamuuliza maswali yale yale kachemka.
Nikawapa viidokezo: katika maumbo mliyofundishwa hiki kisima ni umbo gani? ndo wakafumbuka macho na kusema ni CYLINDER! Wakafanya wakapata yote isipokuwa la mwisho nililouliza kama maji ya kisima yatatumika kwa siku 200 kwa mwaka je tutanununua maji? Wakasema ndio, Wakakosa jibu ni hapana kamwe hatutanunua maji kwasababu siku 200 ni kama miezi saba ambapo kabla haijaisha mvua itakuwa imenyesha na kujaza tena kisima tuna mvua za vuli, masika, n.k
.
Kwahiyo, hizi shule za binafsi wanatafuta hela tu na sio kuwapa watoto wetu maarifa. Wanakuwa wamefaulu mitihani sana hadi chuo lakini wakimaliza ndo wa kwanza kuitukana serikali iwaari.
Hahaa ..
Very interesting.
Ulitoa kipimo kizuri sana, sema swali la mwisho uliwaonea ni la kiwango cha elimu ya juu kifikiria na mazingira na tabia nchi ya eneo husika.

Ilo swali la mwisho hata wahandisi waliosanifu mradi wa BRT wangefeli sababu hawakuangalia vigezo vya tabia nchi ya eneo la mradi ni vile unakuta maji yanafurika jangwani na barabara inafungwa.
 
M

mbu wa dengue

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2014
Messages
1,744
Points
2,000
M

mbu wa dengue

JF-Expert Member
Joined Jun 2, 2014
1,744 2,000
Afadhari hizi shule za binafsi za bongo wanafundisha kupass mitihani kuliko za wakenya wanafundisha kuongea kiingereza
Mkuu usichanganye mambo ya Kenya.
Wako vzr kila upande hata mambo ya engineering na udaktari.
Ukitaka kuprove ingia Google Kisha ulizia vyuo bora Africa halaf uone vya Kenya vimeshika namba ngapi na vya Tanzania vimeshika namba ngapi halaf ndipo utaelewa.
 
M

mangatara

JF-Expert Member
Joined
Jul 6, 2012
Messages
12,930
Points
2,000
M

mangatara

JF-Expert Member
Joined Jul 6, 2012
12,930 2,000
Hakuna sehemu ambayo nimeongelea shule za kata, au nimefanya comparison
Soma vizuri ulichoandika na mantiki yako. Umesema, shule binafsi zinafundisha kushinda tu. Hivyo, kwa kuwa hizo shule binafsi zinafundisha kushinda tu, zile zingine ndio zinafundisha elimu bora.
 
N

nyamwingi

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2016
Messages
376
Points
500
N

nyamwingi

JF-Expert Member
Joined Mar 10, 2016
376 500
Ukiangalia matokeo ya kidato cha nne na sita ni ukweli usiopingika wanafaulu sana, lakin ukiangalia shule binafsi nyingi wanafunzi wanafundishwa mbinu za kufaulu mtihani na sio kuelewa mazingira yaliyomzunguka.

Kwenye hizo shule msisitizo ni kufaulu Kwa sababu elimu ni biashara, matokeo yake huyo mwanafunzi akienda chuo akimaliza anakua hana uwezo sana Kwa sababu msingi wake alikuwa anapewa mbinu za kufaulu na sio kuelewa.

Ndo maana wanafunzi wengi wa kileo wanavyeti vizuri sana lakini vichwani hamna kitu, hawana maarifa.
Mbona siku hizi private na gavmnt.wanafanya mitihani sawa ya moko,kata ,wilaya n.k
 
Smart911

Smart911

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2014
Messages
29,943
Points
2,000
Smart911

Smart911

JF-Expert Member
Joined Jan 3, 2014
29,943 2,000
Ni kweli... ila kaa ukijua...

Maarifa ni sekta binafsi ila serikalini ni vyeti tuu...

Cc: mahondaw
 
M

mbu wa dengue

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2014
Messages
1,744
Points
2,000
M

mbu wa dengue

JF-Expert Member
Joined Jun 2, 2014
1,744 2,000
Mtoa mada yupo sahihi kwa asilimia 70.
Ila amekosea kidogo kwenye kupresent.
Ninachojua Mimi elimu ya siku hizi kuanzia shule za private Hadi za serikali/kata wote uelewa wao upo chini sana.
Utofauti wao Ni kwamba wale wa private wanapewa mbinu za kufaulu mitihani na pia walimu wao Kuna njia zingine za siri huwa wanazifanya kimya kimya ikiwa ni pamoja na kuyatafuta maswali yatakayotoka kwenye mtihani wa mwisho kwa gharama yoyote na mwisho wa siku wanamezeshwa siku chache kabla ya pepa.
Ndio maana utashangaa Kama umesoma shule ya government na jirani Kuna shule ya private mkiomba kufanya nao mtihani wa ujirani mwema au mock utashangaa mnawazidi/mnawamudu vzr tu lkn ikifika kwenye necta wanafanya maajabu na kuwa vinara huku st kayumba mkiungaunga.
Ila kitu kingine nilichopendea kwenye shule za government especially za boarding mtoto anakuwa ngangari tofauti na wale wa private ambao wamezubaa zubaa Kama broilers.
Yaani utakuta mtu ana degree halaf unamtumia tangazo la kazi ambalo Lina instructions zote halaf badae anakuuliza eti tunaombaje?barua tunaandikaje ya kuomba kazi?tunatuma na vyeti au cv tupu?
Sasa Hadi mtu unajiuliza je instructions za mitihani ya shule alikuwa anaelewaje na kufaulu mtihani?
 
Forum statistics

Threads 1,325,729
Members 509,278
Posts 32,201,078
Top