Shule bila ada sawa. Chakula cha mchana bado ni changamoto kwa wanafunzi

yumbu

Member
Mar 16, 2012
66
10
Katika vitu vinavyorudisha nyuma ktk elimu kwa watoto wetu wanaosoma shule za umma ni Ada lakini serikali imeliona hili tunashukuru.

Lakini kuna hili la CHAKULA CHA MCHANA. Hili ni janga kubwa kwa shule za vijijini. Wanafunzi wa shule hizi 95%+ hawana uwezo wa kupata walau chai majumbani mwao.

Kwa hiyo inawalazimu kurudi majumbani kupata chakula cha mchana, hata hivyo kuna wakati familia zinakuwa hazina chakula kabisa inapelekea wanafunzi kushinda njaa.

Ili kuondoa hii changamoto kuna haja ya kurudisha michango wazazi wachangie chakula au serikali ifanye chakula cha mchana bure kwa shule zetu.

Hii itamfanya mtoto wa atumie muda mwingi kuwaza masomo na siyo chakula.

Nawasilisha.
 
Elimu bure ni ghali sana, ona sasa vitu ambavyo havipaswi kulipiwa kodi kama vifaa vya hospitalini na dawa vinaanza kutozwa kodi, ona sasa kodi za m-pesa zinapanda, ona sasa bando langu la internet linaisha fasta kutokana na ongezeko la kodi e.t.c yote haya yanafanywa ili kugharamikia elimu bure!...... Shtuka sasa mkuu!
 
Back
Top Bottom