Shule 10 bora matokeo kidato cha sita 2021 hizi hapa

HKL wameupiga mwingi sana

Leocadia Mbukilo ndiye aliyeshika nafasi ya kwanza kutoka shule ya Sekondari Machame Girls (Kilimanjaro) katika mchepuo wa HKL, huku nafasi ya pili ikichukuliwa na Isack Sanga kutoka Kisimiri Sekondari (Arusha).

Nafasi ya tatu hadi ya kumi imechukuliwa na wavulana kutoka sekondari ya Dareda (Manyara) na nafasi ya tatu imechukuliwa na Deogratias Maendeleo, akifuatiwa na Rafael Daqaro, aliyechukuwa nafasi ya nne huku nafasi ya tano ikichukuliwa na Brayan Minja (HGL).

Giliad Msungu ameshika nafasi ya sita huku nafasi ya saba ikichukuliwa na Rashidi Behero na nafasi ya nane ikichukuliwa na Salimu Ismail wote mchepuo wa HKL.

Nafasi ya tisa amechukua Ibrahim Makongoro (HKL) huku Aidan Daniel kutoka HGL akichukuwa nafasi ya 10.
 
Hivi Ile nlisoma ilikua ni shule kweli ama madrasa tu....maana hata 100 bora huwa siioni ....πŸ€”
Enzi zile nilipambana sana walau niibebe shule lakini wapi ,nikaambulia four nzuri.
 
Hivi hii imekaaje, yani kitaifa Mkoa ulioongoza ni Singida,, lakini kwenye top ten hamna shule ya singida hata moja.
 
Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limetangaza matokeo ya kidato cha sita mwaka 2021 na kutaja shule kumi bora zilizofanya vizuri katika mtihani huo.

Akizungumza leo Jumamosi Julai 10, 2021 visiwani Zanzibar wakati akitangaza matokeo hayo, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), Dk Charles Msonde amesema shule iliyoshika nafasi ya kwanza ni Kisimiri ya mkoani Arusha iliyokuwa na watahiniwa 72.

Msonde amesema Kemebos ya Kagera yenye watahiniwa 35 imeshika nafasi ya pili ikifuatiwa na Dareda ya Manyara watahiniwa 101.

Nafasi ya nne amsema imechukuliwa na Tabora Girls yenye watahiniwa 100 ikifuatiwa na Tabora Boys yenye watahiniwa 120.

Nafasi ya sita imeshikwa na Feza Boys ya mkoa wa Dar es Salaam iliyokuwa na watahiniwa 71 ikifuatiwa na Mwandet ya Arusha yenye watahiniwa 53.

Zakia Meghji imeshika nafasi ya nane ikitokea mkoani Geita. Ilikuwa na watahiniwa 31, ikifuatiwa na Kilosa ya Morogoro yenye watahiniwa 91, na Mzumbe watahiniwa 135.

=====

Izi hapa shule 10 zilizofanya vizuri zaidi mwaka 2021

1.KISIMIRI
2.KEMEBOS
3.DAREDA
4.TABORA GIRL'S
5.TABORA BOY'S
6.FEZA BOY'S
7.MWANDET
8.ZAKIA MEGHJI
9.KILOSA
10.MZUMBE

LINK YA MATOKEO IYO APO


Mungu mwema binti yangu no.4 kalipa one ya baba yake kweli historia inajirudia. Tabora Girls
 
Pugu, azania, tambaza n.k zinazalisha vilaza tu siku hizi
Umeuliza swali nililotaka kuuliza nikiongezea Kibaha na Ilboru

NB: Nimeangalia raw data, inaonekana Kibaha na Iliboru pia walipiga ila walikuwa na walifyata wengie kidogo, kwa hivyo wastani ukawa chini. Hata hivyo baada ya kupitia data za shule nyingi, nina wasiwasi kuwa huenda standard imetelemka kidogo kupunguza failure rates kwani Div I ni nyingi sana kuliko wastani.
 
Back
Top Bottom