Shukuru Kawambwa: Mawaziri wasitokane na wabunge bali watoke nje ya Bunge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shukuru Kawambwa: Mawaziri wasitokane na wabunge bali watoke nje ya Bunge

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by dosama, Jul 30, 2012.

 1. dosama

  dosama JF-Expert Member

  #1
  Jul 30, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 786
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Waziri wa elimu bwana Shukuru Kawambwa kapendekeza kuwa katiba ijayo mawaziri wa serikali wasitoke ndani ya wabunge bali watoke nje ya vyama vya siasa ili kuleta dhana nzima ya uwajibikaji na utendaji mzuri katika wizara.

  Aliyasema hayo wakati akichangia kama mwananchi katika kutoa maoni ya katiba mpya na sera ya CCM ya kuwa na serikali mbili.

  Concern
  Hii ni dalili ya anguko la ccm baada ya mawaziri kushindwa kufanya kazi na maslai ya chama zaidi badala ya taifa.
   
 2. Blessed

  Blessed JF-Expert Member

  #2
  Aug 1, 2012
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 2,488
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  kufuatia uwajibikaji na ufanisi unaondelea kuonekana katika wizara ya Madini na Nishati,naamn ni vyema mawaziri wakawa wataalamu na sio wanasiasa,kwa ufanisi zaidi,na napendekeza hili liingie kwenye katiba mpya moja kwa moja!
   
 3. L

  Le Grand Member

  #3
  Aug 1, 2012
  Joined: Jul 28, 2012
  Messages: 70
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 15
  Point.......!
   
 4. i

  iMind JF-Expert Member

  #4
  Aug 1, 2012
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 1,907
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  Sasa kama mawaziri wasipokua wanasiasa then watakua na tofauti gani na makatibu kuu.
   
 5. gwakipanga

  gwakipanga JF-Expert Member

  #5
  Aug 1, 2012
  Joined: Dec 1, 2011
  Messages: 472
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 45
  Ni habari njema kwa raia wapenda haki. Maana waziri amedhubutu kuongea kile anacho amini na kinacho semwa na wengi. Mh Kawambwa kama mbunge na waziri anaona kwamba, mbunge ambaye ni waziri inakua vigumu kutoa hoja ambayo itaipa wakati mgumu serikali wakati yeye yupo huko huko serikalini. Na sio swala la mbunge kuwa waziri hata wakuu wa mikoa na wilaya ni mizigo nchi kwa katiba ya sasa. Kwa nchi zenye serikali zenye majimbo, wakuu wamikoa wanakuwa kama mapremia ambao wanakuwa wanawakilisha serikali za majimbo kwenye serikali kuu. Ila kwa sasa kwenye katiba mpya cheo cha wakuu wamikoa na wilaya kingeondolewa maana ni mzigo kwa nchi. Na tume ya katiba ya katiba iheshimu maoni yetu kwenye mitandao ya kijamii. Maana wengi wetu hatutapa muda wakuonana na tume kutokana na maeneo ya kijografia tuliopo. Mwisho kabisa viongozi wengine wawe huru kutoa maoni yao kama Mh Kawambwa maana unafiki wao ndiyo unaipeleka nchi yetu kubaya.
   
 6. M

  Mathematic Member

  #6
  Aug 1, 2012
  Joined: May 15, 2011
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Watakuwa tofauti mkuu,maana wao watakuwa mawaziri na hao wengine watabakia kuwa makatibu. Hizo ni post mbili tofauti zenye job description tofauti.
   
 7. M

  Morrison Senior Member

  #7
  Aug 1, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 102
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Ni hoja inayopaswa kuungwa mkono kwani inapelekea kuweka mazingira bora kwa dhana ya uwajibikaji na kuwezesha dhana ya ''check and balance'' miongoni mwa mihili mitatu ya serikali.
   
 8. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #8
  Aug 1, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,780
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Namuunga mkono. Mimi ktk kigezo cha umri wa mgombea wa Urais naomba kibakie kama kilivyo sasa,kuanzia miaka 40. Nitarudi kutetea hoja yangu.
   
 9. harakat

  harakat JF-Expert Member

  #9
  Aug 1, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 2,908
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  vizuri amefunguka iwe ajira tu na sio kitu cha kisiasa maana
  unakuta kilaza hajui hata majenerata yakoje ndio wa nishati
  akiletewa mafriji anajua ni majenerata
   
Loading...