Shukurani za ccm - ccm wekeni utaifa mbele


Sikonge

Sikonge

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2008
Messages
11,550
Likes
642
Points
280
Sikonge

Sikonge

JF-Expert Member
Joined Jan 19, 2008
11,550 642 280
Wahenga wetu walisema zamani sana kuwa ukipanga pilipili basi utavuna pilipili. Hii ni methali ambayo wengi wanaifahamu ila wamekuwa kama vile hawataki kukubali kuwa inaweza kutokea kwao pia.

Viongozi wengi wa Chama cha CCM, wamekuwa vipofu na matatizo ya wananchi wa kawaida kwa sababu tu wao kil siku meza yao imejaa vyakula ingawa maghala ya kuhifadhi vyakula yako tupu. Kwa kujilinganisha na wengine ambao hata meza zao za vyakula iko tupu, wamekuwa vipofu kabisa wa kufikiri ni jinsi gani wafanye wao kama viongozi ili maghala ya vyakula yawe na vyakula vya kutosha.

Kwenye Umoja wa Vijana wa CCM, alikuwepo kiongozi wao mmoja na baadaye akagombea Ubunge huko Kyela na akashindwa. Marehemu Samson Kipepe alikuja akaugua na alipouguwa tu, CCM wakamuweka pembeni na kumsahau. Walewale aliokuwa akiwatukana kwenye majukwaa wakati wa kampeni, walewale Wanyakyusa wenzake huku wengine wakiwa wanatoka upinzani, wengine wakiwa hawana vyama, ndiyo wakaanza kukusanya pesa ili akatibiwe India. Bahati mbaya hawakuwahi na akawa amefariki. CCM bado walikaa kimya na kuendelea na biashara zao huku mwenzao akiuguwa hadi kufa.

Sasa hivi kuna huyu mama anaitwa Hawa Ngulume. Huyu na yeye alikuwa mpiga debe za CCM mzuri sana na huku akishika nyadhifa mbalimbali za CCM. Alikuwa akifurahia siku zote kula vyakula vya kwenye maghala bila kuhakikisha wanaleta vyakula vingine. Sasa hivi ni mgonjwa mahututi na akienda Muhimbili wanamwambia "ghala halina vyakula" na inabidi aende India kutibiwa. Wenzake sasa hivi wamemaliza VYAKULA vyote kwenye maghala kwani Uchaguzi ni hela nyingi. Na yeye alivyo na bahati mbaya, anauguwa wakati wa kampeni za uchaguzi huku akifahamu kabisa kuwa kipindi hiki, CCM huwa inasafisha maghala yote ili washide.

Sasa mama kabaki akilalamika hadi magazetini. Kama wangelikuwa wamekula na kuweka vyakula magahalani, leo hii angelikuwa anatibiwa Bugando au Muhimbili. Kwa wizi wao na kutaka kutembelea mashangingi na kulipana mishahara na allowance kubwa, leo Muhimbili haina vifaa ambavyo Ngulume angelisaidiwa.

Hii iwe ni ONYO kwa wana CCM wote kuwa mnapokula hadi mbegu, mtakaoumia ni nyie. Wenzenu wakiuguwa basi wanapelekwa nje, watoto wao wanasoma nje, nyie je? Hata kama mnaushabiki wa Chama, basi wekeni maslahi ya Taifa mbele na chama nyuma. Hata muwe na Mashangingi na majumba ya kifahari, kama nchi haina pesa ili kujenga huduma za jamii, basi mjuwe hamna kitu.

Tunataka Serikali imara, itakayofahamu kuwapa watu chakula na kukumbuka pia kuna kesho na kuna kuuguwa. Ijenge barabara zetu vizuri, kutafuta usafiri kwa ajili ya Wanafunzi mijini, huduma za hospital, watoto yatima, shule nk.
Huu ushabiki wenu wa kuweka chama mbele hata kama kina makosa, mwisho wa siku mtaishia chini kama mwenzenu Hawa Ngulume.....

6003571.jpg?406


Wanaofaidika hadi uzeeni na hata wakiuguwa ni wachache sana. Nyie wengine wote mtabaki kuwa Chambio la Mafisadi. Sisemi uiache CCM yako, hapana. Ila muwabane hao viongozi wenu ili wakumbuke na kesho.
 
Sikonge

Sikonge

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2008
Messages
11,550
Likes
642
Points
280
Sikonge

Sikonge

JF-Expert Member
Joined Jan 19, 2008
11,550 642 280
Niweke swali:

Kwa nini hapa mama hana NJANO au KIJANI? Kwa nini hana Njano na Kijani?
 
Ndibalema

Ndibalema

JF-Expert Member
Joined
Apr 26, 2008
Messages
10,941
Likes
230
Points
160
Ndibalema

Ndibalema

JF-Expert Member
Joined Apr 26, 2008
10,941 230 160
Huyo mama alivunja miiko ya kifisadi ya CCM ndio maana wakamtupa.
 
Sikonge

Sikonge

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2008
Messages
11,550
Likes
642
Points
280
Sikonge

Sikonge

JF-Expert Member
Joined Jan 19, 2008
11,550 642 280
Mkuu,

Lakini Marehemu Kipepe wa Kyela yeye hakuvunja miiko. Au ukiuguwa ndiyo kuvunja miiko kwenyewe?
Huyo mama alivunja miiko ya kifisadi ya CCM ndio maana wakamtupa.
 

Forum statistics

Threads 1,236,542
Members 475,191
Posts 29,261,696